Ficha IP Adress yako kwa kutumia VPN (Android users)

Asante mkuu na hili neno LCD ktk monitor huwa linamaanisha nini na nini hasa hii maana utaskia hii ni LCD Mara LED,
Lecd na led ni aina ya display yani nia iana ya kioo chako kilivyotengenezwa.
Led kinaonyesha vizuri zaidi kuliko LCD.
Na LED ina aina pia ndani yake
 
Asante mkuu na hili neno LCD ktk monitor huwa linamaanisha nini na nini hasa hii maana utaskia hii ni LCD Mara LED,
LCD inasimama kama Liquid Crystal display ni old method iliyokuwa inatumia screen zenye liquid kudisplay mbali mbali na LED ni currently tech ambayo ni Light Emitting diode LED
 
Virtual private network ni mfumo ulioanzishwa mwanzo kwajili ya biashara kubwa baadae hata watumiaji binafsi walilazimika kutumia ,
Mfano: coca cola company iko karibu dunia nzima bila kutumia vpn wangelazimika kutumia cables kuunganisha office zao mfano Canada, Georgia, Tanzania ila haiwezekani kwaiyo watatumia internet na vpn itahusika hapo ili kulinda taarifa zao kutoka kwa hackers.
Mfumo huu unaosaidia ukiwa kwenye mtandao usionekane uko wapi(hide your location), pia unakusaidia kuficha taarifa zako (data encryption), pia unakusaidia kuingia website zilizofungiwa(unblock site) sehemu uliopo mfano ukiwa china sites kama YouTube, google, facebook, zimefungiwa ukitaka kiziacces lazma utumie vpn,
Vpn pia inauwezo wakuficha I.p address yako isijulikane iko wapi?
Vpn zipo nyingi na kila moja ina idadi ya servers , zipo za free na zipo zakulipiwa kwa jinsi yakutumia vpn ingia YouTube kila moja ina jinsi yaku install + configuration. .
Nawezaje kutumia VPN? Process zake
 
LCD inasimama kama Liquid Crystal display ni old method iliyokuwa inatumia screen zenye liquid kudisplay mbali mbali na LED ni currently tech ambayo ni Light Emitting diode LED

LCD zinatumika mpaka leo, ni back-lighting system ambayo hutofautisha kati ya 'CCFL lit LCD' na 'LED lit LCD', ni sawa na useme 'diesel powered engine' na 'petrol powered engine' zote zina engine ila mfumo wa ignition ni tofauti

LED vs. LCD TVs explained: What’s the difference?
 
Jaribu tor browser ipo vizuri hii ni km vpn (lkn siyo vpn) km ww ni mdau wa deep web hii ndiyo browser
Vpn zipo nying ila za bure siyo nzuri sana.
Umenikumbusha mambo ya chuo, walifunga cyber roam, huwezi kuingia youtube facebook wala torrent site, Ilikuwa inanifaa sana hiyo.
 
How? Unaweza kutuelezea hapa,? Je mim mtumiaji wa cm ya kawaida nawezaje kutumia hyo VPN
nazani ushasoma kwenye comment za watu wengine ila Kwa kuongezea tu hizi ni application na zipo play store .
kupata free internet sio vpn zote zinatoka ila ni baadhi na sio Kwa mitandao yote
 
Ni mpango unaowezesha kifaa chako sim au computer kuwa na mtandao binafsi, kina faida nyingi sana ikiwemo kuhamisha location uliopo , kwa mfano upo dsm tz, lakini kifaa hiki kikakuonyesha upo new delhi india, new york USA, London uk, pia kinauwezo wakuficha ip address yako hata ISP wako anaye kupa huduma ya internet ashindwe kuku track nk
 
Virtual private network ni mfumo ulioanzishwa mwanzo kwajili ya biashara kubwa baadae hata watumiaji binafsi walilazimika kutumia ,

Mfano: coca cola company iko karibu dunia nzima bila kutumia vpn wangelazimika kutumia cables kuunganisha office zao mfano Canada, Georgia, Tanzania ila haiwezekani kwaiyo watatumia internet na vpn itahusika hapo ili kulinda taarifa zao kutoka kwa hackers.

Mfumo huu unaosaidia ukiwa kwenye mtandao usionekane uko wapi(hide your location), pia unakusaidia kuficha taarifa zako (data encryption), pia unakusaidia kuingia website zilizofungiwa(unblock site) sehemu uliopo mfano ukiwa china sites kama YouTube, google, facebook, zimefungiwa ukitaka kiziacces lazma utumie vpn,

Vpn pia inauwezo wakuficha I.p address yako isijulikane iko wapi?

Vpn zipo nyingi na kila moja ina idadi ya servers , zipo za free na zipo zakulipiwa kwa jinsi yakutumia vpn ingia YouTube kila moja ina jinsi yaku install + configuration. .

Kwa nini inaitwa VIRTUAL network wakati ni network ya ukweli?

Kwa mfano uliotumia wa COCA COLA Company, wafanyakazi au ofisi za kampuni popote duniani wanaweza kukutana ( kuwasiliana na ku access data za kampuni kwenye network moja), at the exclusion of all other unathorized guests, which means ni network ya ukweli.

Why VIRTUAL?
 
Vitual Private Network (VPN) kazi yake kubwa ni kuficha IP adress yako ya kifaa unachotumia na unaweza change location unayotaka kulingana na mahali kuna sever zao mfano unaweza onekana unachati toka marekani kumbe uko olmatejoo au ngarenaro arusha au kambi ya fisi
 
Somo kuhusu VPN
Kirefu cha vpn ni virtual private network.Hii ni private network inayokuwezesha kutumia public network pasipo kutambulika.Private network ya kawaida huwa inakosa Usalama wa data.Unapokuwa kwenye public network watu wote mnaotumia hiyo network mnakuwa connected kiasi cha kwamba yoyote kwenye network haswa provider anaweza ku access data za mwengine.Kwa wale watumiaji wa tigo mfano utaona ukiwa una surf link yoyote kutokea facebook unakuja ujumbe wa kukumbusha unatoka facebook hiyo inaonesha Tigo wana access na data zako na wanaweza kufanya chochote
Jinsi VPN inavyofanya kazi
Kila kifaa kinachotumia network huwa na utambulisho wake unaoitwa IP address,VPN hufanya kazi ya kubadilisha IP address ya kifaa chako na kukupa nyengine ambayo sio ya kweli yani Virtual IP address ambayo inakuwezesha kutokutambulika ukiwa kweny network.
IP address hubeba utambulisho unaonesha nini unatafuta kwenye network,wapi ulipo na jinsi ya kufikia unachokitaka
Faida za VPN
VPN huweza kubadilisha IP address na kuwezesha kukufanya uonekane popote utakapo duniani,kukufanya uingie kwenye websites zinazozuiwa na kukufanya uepuke michujo yoyote kwenye internet
Usalama ni mkubwa na ni ngumu mtu kujua utambulisho wako halisi
Inapunguza gharama za ku surf
Jinsi ya kutumia VPN
Kuna njia nyingi za kutumia VPN lakini rahisi zaidi ni ile ya kutumia software inayobadilisha IP address yako kila unapoanzisha network
Kwa watumiaji wa simu hili ni rahisi zaidi kwani kuna apps zinazofanya kazi hii
App unayopaswa kuichagua inategemea unataka kuitumia VPN kwenye matumizi gani
Zifuatazo ni Apps bora za VPN kwa watumiaji wa Android
1.Hotspot Shield VPN&Proxy
Kitu cha pekee kuhusu app hii ni kusupport 4G na ina features nyingi kuliko vpn app nyenginezo
2.Unlimited free VPN-berrenet
3.Hideman VPN
4.SurEasy VPN
5.FinchVPN
6.Hola free VPN
7.Tunnel bear
 
Back
Top Bottom