Ferouz: Inaniwia vigumu kuacha madawa ya kulevya

Msanii mkongwe wa muziki Ferooz Mrisho ambaye katika miaka ya 2000 alitamba na wimbo wa Starehe ambaye kwa sasa ameathirika na dawa na matumizi ya Madawa ya kulevya, amedai inamuwia vigumu kuachana na matumizi ya dawa hizo. Muimbaji huyo amedai amejikuta akitenga bajeti kubwa ya fedha kwa matumizi ya kutumia dawa.

“Ninawaomba wasanii wenzangu wasitumie dawa maana ni vigumu kuacha. Natamani sana kurudi kama zamani ili heshima yangu iwepo ila inanisumbua, lakini naamini iko siku,” Ferooz aliliambia gazeti la Mtanzania.

Hata hivyo muimbaji huyo alipoulizwa ni wapi anaponunua Madawa hayo hakuwa tayari kutaja.
When you fail to plan, you plan to fail.
 
Hii starehe ni kwa ajili ya wasanii tu sio..Mbona sioni ma Prof,ma Dr na wengine wakila hii kitu
 
Nenda Muhimbili Hospital kitengo cha akili kuna watu wa kila aina mpaka madaktari waliokuwa na matatizo ya ulevi wa kupindukia wapo na wenyewe wapo katika kundi ilo la akili
 
Msanii mkongwe wa muziki Ferooz Mrisho ambaye katika miaka ya 2000 alitamba na wimbo wa Starehe ambaye kwa sasa ameathirika na dawa na matumizi ya Madawa ya kulevya, amedai inamuwia vigumu kuachana na matumizi ya dawa hizo. Muimbaji huyo amedai amejikuta akitenga bajeti kubwa ya fedha kwa matumizi ya kutumia dawa.

“Ninawaomba wasanii wenzangu wasitumie dawa maana ni vigumu kuacha. Natamani sana kurudi kama zamani ili heshima yangu iwepo ila inanisumbua, lakini naamini iko siku,” Ferooz aliliambia gazeti la Mtanzania.

Hata hivyo muimbaji huyo alipoulizwa ni wapi anaponunua Madawa hayo hakuwa tayari kutaja.
Ngoma inogile....wananunua kwa pusha kisha wanaenda Dago
 
ba8047093f1291999202165ca3629c8a.jpg
 
Hii starehe ni kwa ajili ya wasanii tu sio..Mbona sioni ma Prof,ma Dr na wengine wakila hii kitu
Tembea uone.

Wapo kibao ila wanazungumziwa wasanii kwa sababu ni watu mashuhuri kwenye jamii na wanajulikana kabla hawajaanza kunyonya
 
Back
Top Bottom