Ferouz: Inaniwia vigumu kuacha madawa ya kulevya

brave one

JF-Expert Member
Feb 5, 2013
4,847
2,000
Msanii mkongwe wa muziki Ferooz Mrisho ambaye katika miaka ya 2000 alitamba na wimbo wa Starehe ambaye kwa sasa ameathirika na dawa na matumizi ya Madawa ya kulevya, amedai inamuwia vigumu kuachana na matumizi ya dawa hizo. Muimbaji huyo amedai amejikuta akitenga bajeti kubwa ya fedha kwa matumizi ya kutumia dawa.

“Ninawaomba wasanii wenzangu wasitumie dawa maana ni vigumu kuacha. Natamani sana kurudi kama zamani ili heshima yangu iwepo ila inanisumbua, lakini naamini iko siku,” Ferooz aliliambia gazeti la Mtanzania.

Hata hivyo muimbaji huyo alipoulizwa ni wapi anaponunua Madawa hayo hakuwa tayari kutaja.
 

igwee frm anambra

JF-Expert Member
May 16, 2015
645
1,000
Kuna msanii fulani maarufu anastua hii mambo kiaina , ....hii 2017 sidhani kama ataimaliza bila kuwa publicly. ...
 

Rais2020

JF-Expert Member
Jul 14, 2016
3,260
2,000
Msanii mkongwe wa muziki Ferooz Mrisho
ambaye katika miaka ya 2000 alitamba na wimbo
wa Starehe ambaye kwa sasa ameathirika na
dawa na matumizi ya Madawa ya kulevya,
amedai inamuwia vigumu kuachana na matumizi
ya dawa hizo.
Muimbaji huyo amedai amejikuta akitenga bajeti
kubwa ya fedha kwa matumizi ya kutumia dawa.
“Ninawaomba wasanii wenzangu wasitumie dawa
maana ni vigumu kuacha. Natamani sana kurudi
kama zamani ili heshima yangu iwepo ila
inanisumbua, lakini naamini iko siku,” Ferooz
aliliambia gazeti la Mtanzania.
Hata hivyo muimbaji huyo alipoulizwa ni wapi
anaponunua Madawa hayo hakuwa tayari kutaja
Dawa za kulevya tishio kwa
wasanii, vijana
NI mtihani. Ndivyo unaweza kusema, hasa
baada ya kundi kubwa la vijana wenye umri wa
miaka 15 hadi 30 kujikuta likiteketea kutokana
na matumizi ya dawa za kulevya.
Kutokana na hali hiyo, kundi la wasanii wa
muziki wa kizazi kipya na vijana wa kimaskini
wamekuwa ni waathirika wakubwa hali
inayotishia nguvu kazi ya Taifa.
Kundi la hilo la wasanii sasa limegeuka mateka,
huku hali hiyo ikichangiwa na wafanyabiashara
wakubwa nchini, ambao wamekuwa
wakiwashawishi kwa fedha na hata kuwahonga
magari ili waweze kutumia mihadarati.
MTANZANIA ilizungumza na baadhi ya wasanii
ambao sasa wamejikuta katika matumizi ya
mihadarati hiyo na hata kuonekana kuwaumiza
huku wengine wakiwa kama wendawazimu.
Mmoja wa wasanii wa muziki wa kizazi kipya,
Abubakari Katwila, maarufu Q-Chief, ambaye
anatajwa katika matumizi ya dawa za kulevya,
alisema kwa sasa ameacha baada ya kukubali
kuwa alipotea.
Alisema wakati anaingia katika matumizi hayo
ya mihadarati hakushawishiwa na mtu, bali
alijikuta ametumbukia katika hali hiyo.
“Nilikuwa muathirika wa dawa za kulevya,
nimejitambua nimeacha mimi mwenyewe bila
kulazimishwa na mtu, huwezi kumtibu mtu
ambaye hajajikubali hili ni tatizo,” alisema.
FEROOZ
Ferooz Mrisho ambaye katika miaka ya 2000
alitamba na wimbo wa Starehe ambao ulikuwa
ukihamasisha mapambano dhidi ya Ukimwi,
ambaye kwa sasa ameathirika na dawa hizo,
alisema inamuwia vigumu kuachana na
matumizi ya dawa hizo.
Alisema pamoja na hali hiyo, amejikuta akitenga
bajeti kubwa ya fedha kwa matumizi ya kutumia
dawa, ingawa alipoulizwa ni wapi anaponunua
hakuwa tayari kutaja.
“Ninawaomba wasanii wenzangu wasitumie
dawa maana ni vigumu kuacha. Natamani sana
kurudi kama zamani ili heshima yangu iwepo ila
inanisumbua, lakini naamini iko siku,” alisema
Ferooz.
Wasanii wengine ambao wanahusishwa na
tuhuma za matumizi ya dawa za kulevya ni
pamoja na Geez Mabovu, Daz Baba, T.I.D, Ray
C, Lord Eyez, Rashidi Makwilo ‘Chid Benz’, 20%,
Terry Fanani, Sister P, Msafiri Diouf, Rachael
Kiuno, Mandojo, Domokaya, Rose Mhando na
Nando ambaye hivi karibuni alishiriki
mashindano ya Big Brother (BBA).
Mmoja wa wasanii hao ambaye hakuwa tayari
kutajwa jina lake gazeti, alisema kuwa pamoja
naye kujikuta anatumia dawa za kulevya, lakini
bado Serikali inajua watu wanaoingiza dawa
hizo na wameshindwa kuwachukulia hatua.
“Kula dawa inahitaji gharama, maana inafika
mahali ili niweze kupata kete walau moja kila
siku asubuhi inanibidi nitafute Sh 3,000. Lakini
pia hufika mahali natumia hadi Sh 15,000 kwa
siku.
“Wapi napata pesa? Unajua licha ya hii kazi
yangu ila bado kuna jamaa zangu wanene
(wafanyabiashara) ambao nao hutumia,
ukiwapigia simu hukosi 20,000 au hata 100,000.
Na mimi nilipoingia katika matumizi haya jamaa
yangu mmoja alinishawishi kuwa nikitumia hii
atanipa safari, kumbe nilikuwa naonja ili kujua
ubora, basi hadi leo nimejikuta natumia,”
alisema msanii huyo.
Matumizi ya dawa za kulevya yanatajwa
kusababisha vifo vya wasanii kadhaa wakiwamo
Ramadhani Masanja ‘Banza Stone’, Aisha
Mohamed ‘Aisha Madinda’, Albert Mangwea
‘Ngwea’, Langa, Grace Mbawala na Esther
Bondia.
Licha ya hilo, taarifa za ndani zinaeleza kuwa
aliyekuwa msanii nyota wa Bongo Movie,
marehemu Steven Kanumba pia anahusishwa na
matumizi ya dawa hizo.
Inalezwa kuwa baada ya kifo chake, alikutwa
katika kucha akiwa na chembe za unga
unaosadikiwa kuwa ni dawa za kulevya, ambazo
baada ya kutumia alikunywa pombe kabla ya
kuingia katika ugomvi unaodaiwa kusababisha
mauti yake.
VITA DHIDI YA DAWA ZA KULEVYA
Kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa na Tume
ya Kudhibiti Dawa za Kulevya, vita dhidi ya
matumizi ya dawa hizo imeendelea kupata
changamoto nyingi kutokana na kukithiri kwa
uingizaji wake.
Tume hiyo ilidai kuwa kiwango cha dawa
zinazoingia na kukamatwa kimepanda kutoka
kilo tatu za dawa aina ya Heroin mwaka 2008
hadi kilo 265.54 mwaka 2011 na kilo nne za
dawa aina ya cocaine hadi kufikia kilo 128.30
kwa mwaka huo.
MSAKO WA WASANII WABWIA UNGA
Akizungumza na MTANZANIA, Kamishna wa
Tume ya Kudhibiti Dawa za Kulevya, Mihayo
Msikhela, alisema hivi sasa wapo kwenye msako
dhidi ya wasanii ambao wamekuwa
wakisambaza ujumbe wa matumizi ya
mihadarati hiyo.
Alisema wasanii hao ambao ndio kioo cha jamii,
sasa wamekuwa wa kwanza katika kusambaza
ujumbe wa matumizi hayo.
“Mimi binafsi simfahamu Chid Benz kama ni
mtu maarufu aliyekuwa akifahamika kwa kiasi
hicho, lakini baada ya kumuona kwenye
mitandao ya kijamii ndipo nikaanza kumfuatilia,”
alisema Kamishna Msikhela.
Alisema endapo wakipata taarifa ya kwamba
wanatumia hadharani na kuwakamata, basi
watachukuliwa hatua kama wahalifu wengine.
“Hawa wasanii tunawasaka nao watuhumiwe
kama wahalifu wengine na wakichukuliwa hatua
itakuwa fundisho kubwa kwa vijana ambao
walikuwa na nia ya kujiingiza katika mtandao
huo,’’ alisema.
Alisema ni vema kwa vijana wasiwafuate watu
maarufu ambao kwa namna moja ama nyingine
wanaushawishi mkubwa kiasi katika matumizi
ya dawa hizo.
Kamishna Msikhela alisema wimbi kubwa la
vijana wenye umri kati ya miaka 15 na 30 ndilo
ambalo linajiingiza katika matumizi ya dawa za
kulevya jambo ambalo ni hatari kwa Taifa.
“Vijana hawa ndio ambao wangekuwa tegemeo,
vijana wa umri huo ndio ambao wangekuja kuwa
viongozi wa baadaye, yaani kwa umri huo ndiyo
wanaandaliwa kuwa madereva, mawaziri,
wakulima, lakini leo wanakuwa mateja, ni jambo
la hatari sana,’’ alisema.
MIKAKATI
Kamishna Msikhela alisema Jeshi la Polisi kwa
sasa liko katika mkakati maalumu wa
kuhakikisha elimu katika jamii inatolewa ili
wananchi waweze kuelimika.
Alisema ulimaji wa bangi mashambani ni
mkubwa kuliko mirungi, lakini aliongeza kuwa
kama mateja mitaani wanapungua basi hata
uingizaji wa dawa hizo kwa sasa nao
umepungua.
KAULI YA WAZIRI
Juzi Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,
Mwigulu Nchemba, alisema wimbi la magenge,
wauzaji na wasambazaji wa dawa za kulevya
wameongezeka kwa kasi.
Kutokana na hali hiyo, alisema kuwa kwa wale
wanaojihusisha kwa namna yoyote ile ni vyema
wakaamua kuachana nayo kabla hawajakumbwa
na mkono wa dola.
Alitoa kauli hiyo baada ya kufanya mazungumzo
na mama mzazi wa msanii Chid Benz, ambaye
amepatwa na tatizo la matumizi ya dawa za
kulevya.
“Inasikitisha na haivumiliki kuona nguvu kazi ya
Taifa inapotea huku wauzaji wakinufaika kwa
pesa haramu, ifahamike wazi vita ya Serikali
dhidi ya wauzaji ni kubwa kuliko wanavyofikiria,”
alisema.
VIONGOZI WA DINI
Wakizungumza na MTANZANIA, viongozi
mbalimbali wa dini walisema kuwa ipo haja kwa
jamii na Serikali kuwa na hofu ya Mungu.
Askofu Msaidizi wa Kanisa Katoliki, Jimbo la
Bukoba, Dk. Method Kilaini, alisema kama
viongozi wa dini inabidi watoe elimu ya dini kwa
nguvu zote na kuwaweka vijana wawe na hofu
ya Mungu.
“Elimu ya kumweka kijana katika maombi awe
karibu na Mungu hili litasaidia sana kujitoa
katika mtego huo wa shetani na si vinginevyo,”
alisema Askofu Kilaini.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Halmashauri
Kuu ya Taifa ya Baraza Kuu la Waislamu
Tanzania (Bakwata), Sheikh Hamis Mataka,
alisema Serikali haitakiwi kumwacha mtumiaji
wa kawaida kwani naye ni muhalifu pia.
Alisema vita hivyo ni vema vikafanyika kwa
kuangalia kila eneo badala ya sasa kupambana
na waingizaji, huku watumiaji wakiachwa kwani
suala hilo haliwezi kumalizika.
“Kwa upande wa dini tunatakiwa kuanza
kuwaelimisha watoto wetu juu ya dhambi hii
huko kwenye madrasa sio kufundisha Kuran tu,
wazazi sasa hivi wanalea kidigitali, hivyo mtoto
kufanya dhambi anaona ni kitu cha kawaida.
“Tuanze kuwaonyesha watoto wetu namna ya
kumnyenyekea Mwenyezi Mungu, hii naona
itapunguza, pili hata hao vijana walioathrika
wasipelekwe tu ‘Sober House’ kwa sababu ya
matibabu, pia wapate nasaha kutoka kwa
viongozi wa dini ili wakibadilika wabadilike
kiuhakika,’’ alisema Sheikh Mataka.
Mwenyekiti wa Kamati ya Maadili
inayoshirikisha viongozi wa dini, Askofu William
Mwamlanga, alisema Taifa linahitaji maombi
mazito kwani Serikali imeshindwa kudhibiti hali
hiyo na vijana wanaendelea kuangamia.
“Pia kesho (leo) tuna kikao cha wajumbe wa
dini zote ambao mimi ni mwenyekiti wao,
tutajadili hali hii kwani tulikubaliana sekta za
dini zisiwe chaka la kubebea dawa hizo haramu
ambazo pia ni katazo la Mungu,” alisema Askofu
Mwamalanga.
VIONGOZI WA WASANII
Akizungumzia hali hiyo, Rais wa Shirikisho la
Wasanii wa Filamu Tanzania (TAFF), Simon
Mwakifamba, alisema dawa za kulevya ni janga
la Taifa.
Alisema ni vyema kila mmoja anapoona
mwenzake ameathirika afikirie kwa makini kuwa
na yeye kesho anaweza kufika hapo alipo
mwenzie.
Rais wa Shirikisho la Madansa, Super
Nyamwela, alisema baada ya kifo cha wasanii
wenzao, akiwamo Aisha Madinda, walichukua
tahadhari kubwa ikiwamo kufanya utafiti na
kubaini kuwa wengi waliotumbukia katika
matumizi hayo walitumia sigara wakiwa kazini.
WALIONASULIWA WAKAKWAMA
Mara kadhaa viongozi wa kitaifa wamekuwa
wakichukua juhudi mbalimbali ikiwamo
kuwasaidia wasanii hao, akiwamo mwanamuziki
Rehema Chalamila ‘Ray C’ ambaye alisaidiwa
na Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne, Jakaya
Kikwete kwa kuhakikisha analipia matibabu yake
ili aweze kuachana na dawa za kulevya.
Mbali na huyo pia Chid Benz alisaidiwa na
Meneja wa Dimond, Babu Tale kwa kumpelea
Sober House mjini Bagamoyo ambako
alifanikiwa kuacha na baada ya muda alirudia
tena kutumia mihadarati hiyo.
Source: Mtanzania
 

shiu yang

JF-Expert Member
Sep 16, 2016
3,171
2,000
Ile kitu ukisha itumia ndani ya wiki kiacha tena ni balaa yani unaweza jitahidi uache lakini huwezi coz mwili ukikosa unahisi kina kitu kimepungua.
Inakuwa addictive
 

Da Asia

JF-Expert Member
Sep 25, 2011
732
1,000
ukipita uswahilini maeneo kama mtogole na kwingineko unakuta kuna viatu vimetundikwa juu wa nyaya, niliwahi kuuliza maana yake nini nikaambiwa ni maeneo ambayo madawa ya kulevya yanauzwa. Kama ni kweli, nina imani kama kweli polisi kitengo cha madawa ya kulevya wana nia ya dhati kutokomeza basi wangeanza kutokomeza haya maeneo pamoja na wauzaji wake. ku deal na mtumiaji wakati muuzaji anaachwa sio solution.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar threads

Top Bottom