Fedha...

Hapana kiongozi me nitatofautiana na wewe hapo umetafafasiri matumizi ya neno pesa linabadilika kutokana na mazingira ila haujatueleza pesa linamajina gani tofauti na neno lenyewe pesa mfano mzuri ni wa Nyani Ngabu hapo juu ametoa majina ya mtaani ni sahihi kbs na mimi nitakupa yangu km vile mavumba, njuruku na mengine mengi sana.

Hapo kwenye NJURUKU piga ua wewe ni chinga
 
PESA INA MAJINA MENGI KULINGANA NA MAHALI NA MATUMIZI
1.Kwenye ibada inaitwa Zaka/sadaka
2.Msibani inaitwa rambirambi
3.Shule inaitwa Ada au Karo
4.Kwenye vyombo vya usafiri inaitwa nauli
5.Ukiinunulia haki inaitwa rushwa
6.Kumdhamini mtu mahakamani inaitwa dhamana
7.Kwenye uchaguzi inaitwa takrima
8.Ukiwapa kina Preta snowhite inaitwa hongo

Mengine tukumbushane....
mh, mkono wa kidhungu manoti ya kialbaino,,,,
 
Uzuri wa pesa, Pamoja na majina yake yoooote hayo hata sisi tusiojua kusoma na kuandika Hesabu za ela tunazijua. Usione mtu hajui kusoma ukampa chenji pungufu weee....
 
Pesa ni maua huchanua na hunyauka,
Ukiwa nazo utaitwa bos,mkuu, n.k,
Ukiishiwa utaambiwa umefulia,chokambaya,murere.
 

Similar Discussions

11 Reactions
Reply
Back
Top Bottom