Fedha...

Fedha...

Boflo

JF-Expert Member
Joined
Jan 20, 2010
Posts
4,383
Reaction score
4,413
PESA INA MAJINA MENGI KULINGANA NA MAHALI NA MATUMIZI
1.Kwenye ibada inaitwa Zaka/sadaka
2.Msibani inaitwa rambirambi
3.Shule inaitwa Ada au Karo
4.Kwenye vyombo vya usafiri inaitwa nauli
5.Ukiinunulia haki inaitwa rushwa
6.Kumdhamini mtu mahakamani inaitwa dhamana
7.Kwenye uchaguzi inaitwa takrima
8.Ukiwapa kina Preta snowhite inaitwa hongo

Mengine tukumbushane....
 
Kitaani inaitwa mpunga, mkwanja, kisu, mawe,........

Tukiwa na Majita Home tunaita FUBA.

Nyani Ngabu .. ongezea na hizi

Mpango, michuzi pesa (money), michuzi, + mikwanja, mapene, masimbi, chambi chambi, bingo, chapaa, dola, famba, faranga, fuba, goto, jiwe, mafweza, mapene, mavumba, mbumba, michuzi, mkwanja, mshiko, ngawila, ngudongudo, uchache, vumba;

Baba wa taifa, bluu, buku, buku teni, kifaru, kilo, kisu, majani, mkoba, nusu kilo, pochi, tenga, vifaru viwili, wekundu wa msimbazi;

Bati, dala, doma, fisi, gobole, gwala, hais, jero, jiti, karume, mbala, njoroge, nyanga, nyento, nyomi, paundi, pini.
 
Umemaliza kila kitu umesahau lakaki(buku tali aka buku 5)
 
ukiikusanya nyingi inaitwa utajiri

ukiikusanya kidogo inaitwa umaskini

ukiikusanya nyingi kwa njia mchanganyiko wa hongo na rushwa inaitwa ufisadi

Apeche alolo, arosto, waya, mabaga, majalala, ukapa, chacha, chalala, kalukwa, kauka, pigika, rosti, uawa kishenzi, ungua jua, waka;
 
Back
Top Bottom