Fedha za maafa kagera zakarabati shule ya ccm

Hivi huwa hamuoni mnatenda dhambi za uongo? Ccm inamiliki shule wapi? Mwogopeni mungu wenu ndugu zangu mn siasa za kinafki zitatupeleka pabaya.
Mfano, Meta Sec School-Mbeya, Sangu Sec School-Mbeya na Ivumwe? Sec School hapo ni kwa Mbeya jiji tu.
 
Kama ni kweli itakuwa kituko cha karne hii. Ingawa ukimuangalia mkuu wa mkoa wa Kagera kwenye hotuba zake anaonekana kama mtu asiye na maamuzi na vitu vingi anasikiliza toka juu.
Mkuu huko juu walichoshindwa ni kutupangia chakula cha kula, nguo za kuvaa na ndoto za kuota.
 
Mbn hujawahi toa mchango hata siku moja maana huwezi msidia mtu kwani wewe mwenyewe hujitosherezi na huwezi kujisimamia unatumika na mbowe kwa kila kitu utawezaje kuchangia
Wewe toa maoni yako kwa kujitegemea acha kunukuu maoni ya wanaume
 
Inakuaje mtu na akili zako unaliamini gazeti la Mwananchi? Kama ni habari ya kweli, hiyo shule wanasoma kina nani? Chadema hamuwezi pata kura za wananchi kwa mtindo huu maana mnaponda hii ila wananchi huko wanapeleka watoto wao kwenye hiyo hiuo shule, point mmapata wapi hapo??
Usipende kudharau watu mkuu, Mwananchi ni gazeti linalosomwa na watu wengi, kwahiyo watu hao unawazidi akili? Jenga hoja na usipende kuweka Uchadema na Uccm wenu kutukana watu
 
Tumeshachoka na hizi habari za kagera na tetesi za uongo muda wte, ukifatilia utakuta cyo kweli...hiyo hela si ni kwa ajili ya maafs kama shule iliharibiwa na ipo ile sehemu hata ikiwa ni mtu binafsi kwa nini usikarabatiwe? Sitetei uozo ila Hii sasa imekuwa too much.

Utumbo
 
Na hiyo shule wanasoma watoto wa wana ccm tu?...nieleweshe kwa hoja cyo kwa ushabiki wa vyama.
Wanasoma watoto wote lakini mapato yatokanayo na mapato ya ada na michango mingine ni mali ya ccm. Ni sawa na shule yoyote ya private kwa lugha rahisi. Kwa maana hiyo kama habari hii ni ya kweli basi hata wamiliki wengine wa shule binafsi kama zilivyo za ccm wana haki ya kupelekewa hizo pesa ili wafanyie ukarabati. Issue sio nan anasoma bali inaumiliki wa umma ama wa binafsi (private)
 
Ni ujinga kubisha kwamba ccm hawamiliki shule wanazoziweka chini ya " Jumuiya ya wazazi " Kaole sec., Meta sec. Mbalizi sec. Itende sec. Tegeta sec. Shule ya sekondari na ufundi Boza- Pangani , Ccm inamiliki shule 70 nchi nzima baadhi zikiwa na O' to A' level, utaratibu wa kujiunga na shule hizi ni ule ule sawa na utaratibu wa Private hivyo shule zao hazipo kwenye mfuko wa shule za umma, maana ili upate nafasi utatakiwa kutuma maombi kwa kujaza form na kuilipia,
Kwa maana hiyo kama serikali wamepeleka fedha za maafa wafute kauli yao ya kutuaminisha kuwa fedha za maafa zinakarabati miundombinu ya umma waseme tu kuwa fedha zinakarabati Miundombinu yote na si ya umma tu, shule hizi zipo chini ya chama kama zilivyo shule zingine zilizo chini ya watu binafsi,
Tufungue akili vijana, tusipelekeshwe kwa mgongo wa uvyama ni aibu kwa Taifa kuweka chama Mbele kuliko maumivu ya ndugu zako
 
ubinaadamu Ni muhimu kuliko Mali,chakwanza kufikiriwa ilitakiwa iwe maisha salama...food,clothing,shelter and health kwanza mengine yafuate taratibu
 
Majungu sio mtaji ila ninavyojua mimi shule zote zilizoharibiwa zimepewa fedha ya ukarabati nothing else. Mi natokea huko mkuu
Kwaiyo mkuu ile kauli ya awali ya kutuambia kuwa fedha za maafa zimekwenda kurejesha miundombinu na ofisi za umma (Public properties) ni uongo tulidanganywa!? Kwaiyo sasa hvi ni kuwapa tu fedha hadi miundombinu ya watu binafsi wenye uwezo wa kuikarabati kuliko mwanamke yule mjane anayelala nje na wajukuu zake, tuwe wakweli ccm kwa vitega uchumi tulivyonavyo hatushindwi kuibomoa shule yoote na kuijenga upya achilia mbali kuikarabati tu
 
Kwani hiyo shule ya ccm wanasoma wanachama wa ccm tu?mimi ni mwanachama wa CHADEMA lakini mwanangu anasoma hapo na anafanya vizuri darasani kuliko hata watoto wa wanachama wa CCM.
Tatizo sio anasoma nani na nani! Tatizo je ccm kwa upana wake wa vitega uchumi ingeshindwa kukarabati shule hizo badala ya kutumia vijifedha vya maafa ambavyo vingeweza kuwasaidia vikongwe kupata hata bati 10 kumi wajenge nyumba za tope! Tulisema kwa kauli yetu kuwa fedha zitajenga miundombinu ya umma shule zilizopo chini ya jumiya ya wazazi ccm sio shule zilizochini ya umma, kama unasomesha mtoto shule mojawapo nadhani unafahamu utaratibu wa kujiunga na shule hizo ukoje sins haja ya kukueleza, muda mwingine tuwe wakweli kama tuligawa 10M tusingeshindwa kuibomoa shule na kuijenga upya achilia mbali kuikarabati tu!
 
Wanasoma watoto wote lakini mapato yatokanayo na mapato ya ada na michango mingine ni mali ya ccm. Ni sawa na shule yoyote ya private kwa lugha rahisi. Kwa maana hiyo kama habari hii ni ya kweli basi hata wamiliki wengine wa shule binafsi kama zilivyo za ccm wana haki ya kupelekewa hizo pesa ili wafanyie ukarabati. Issue sio nan anasoma bali inaumiliki wa umma ama wa binafsi (private)
Nimekuelew mkuu...lkn kma shule imeharibiwa ya private...hairuhusiwi kukarabatiwa na hizi hela za maafa hadi iwe ya serikali?
 
Utumbo ni uliyeuandika sbu huna hojs yyte ys kuchangia...inabidi uni chalenji kwa kile nilichokuandika kwa hoja...kwa kuandika neno utumbo ni rahisi sana ila kitiririka kws hoja ndo ishu ngumu kwsko. Kma utumbo lete ubungo wako kwa hoja cyo kwa matusi...hapa ni majadiliano kwa hoja cyo kwa matusi
.
 
Back
Top Bottom