Ni ujinga kubisha kwamba ccm hawamiliki shule wanazoziweka chini ya " Jumuiya ya wazazi " Kaole sec., Meta sec. Mbalizi sec. Itende sec. Tegeta sec. Shule ya sekondari na ufundi Boza- Pangani , Ccm inamiliki shule 70 nchi nzima baadhi zikiwa na O' to A' level, utaratibu wa kujiunga na shule hizi ni ule ule sawa na utaratibu wa Private hivyo shule zao hazipo kwenye mfuko wa shule za umma, maana ili upate nafasi utatakiwa kutuma maombi kwa kujaza form na kuilipia,
Kwa maana hiyo kama serikali wamepeleka fedha za maafa wafute kauli yao ya kutuaminisha kuwa fedha za maafa zinakarabati miundombinu ya umma waseme tu kuwa fedha zinakarabati Miundombinu yote na si ya umma tu, shule hizi zipo chini ya chama kama zilivyo shule zingine zilizo chini ya watu binafsi,
Tufungue akili vijana, tusipelekeshwe kwa mgongo wa uvyama ni aibu kwa Taifa kuweka chama Mbele kuliko maumivu ya ndugu zako