FC Barcelona (Barça or Blaugrana) | Special Thread



Moja ya makosa waliyoyafanya barca ni kumsajili Griezman na kumuachia Coutinyo, baada ya kuumia dembele sasa hivi coutinyo angekua anasaidia kupeleka mashambulizi mbele tofauti na griezman. Sasa hivi mbali na Mess barca hakuna mshambuliaji wa kumminya beki na akachomoka na mpira matokeo yake ukifanikiwa kumdhibit mess bashara imeisha. Barca miaka mingi haikua timu ya kuishambuliwa kirahisi rahisi, walikua na mfumo wao wa kuweka washambuliaji wanaokimbiza mpira na kuwafanya wachezaji wa timu pinzani kubaki kwenye nusu ya uwanja wao wakilinda mambo yasiharibike. Jana beki za barca ziliteseka sana kuzuia mashambulizi ya Madrid hasa upande wa vinicius.
 
Uongozi nao wamekua wazito sana katika swala zima la usajiri..tunahitaji difenders at least viwango vya Carles puyor na Dani alves angalau watatu..kule mbele Messi aletewe wasaidizi wawili watatu matata...
Sajiri Neymar Jr,Martinez hata Mbappe....hii itasaidia hata messi anapumzika siku moja moja kuliko ilivyo sasa kila kitu,kila game ni messi tu tunamchosha na kumchakaza
Mbona Pep Guardiola ameweza kuweka kikosi imara?tatizo lipo wapi barca?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Barça kwa sasa inahangaika, ni kama inabahatisha kwenye usajili yaani haielewi inachofanya


Kila sajili wanayofanya inakuwa ina mshaka....

Ni ajabu sana kuona Barça ya sasa haijui ubora wa wachezaji wenye sifa ya kucheza Barcelona

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kinachofanyika barca sasa hivi ingekua bongo tungesema kuna mamluki katika benchi la Ufundi. Msimu ulioisha timu ilikua vizuri katika ushanmmbuliaji na tatizo ktk ulinzi ila cha kushangaza timu imesajili mshambuliaji badala ya beki . Mpaka sasa hivi sijajua greazman alisajiliwa ili iweje .
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Politician wanatuharibia timu... hakuna project .... victor font achukue tu timu
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hahahahahaha nimempenda huyu jamaa... ana gut..


'Children'
Eder Sarabia (assistant coach): "My way of living football will not change, I will always do it with intensity. But it's true that we must set an example for children. I will stay the same."

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tayari mkuu tusharejea kileleni
Wale wakamia mechi wameshaliwa uko.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…