Fastjet, mkiendelea na tabia hii, mtapoteza wateja

and 300

JF-Expert Member
Jun 27, 2012
26,325
36,121
Duniani usafiri wa ndege ni usafiri salama na wafanyakazi wake ni watu wenye weledi wa hali ya juu na kumjali mteja.

Lakini ghafla shirika hili la ndege (Fastjet) wameamua kwa makusudi kuingiza uswahili katika biashara hii ikiwemo KUAHIRISHA/KUFUTA SAFARI bila taarifa za mapema, kuchelewa kupokea simu ya huduma kwa wateja (+255784108900) na kutokutoa majibu sahihi kulingana na tatizo la mteja, lugha mbovu kwa wateja.

Naiona Fastjet kama kampuni ya daladala kwa sasa.
 
Mleta mada nakupa pole Kama bado unapanda hiyo basi ya angani,
Nimepanda mara kadhaa kwenda South Africa yaani utafikiri nipo kwenye basi tu, kila kitu kinauzwa ndani ya ndege yaani hakuna utofauti utadhani Sio international route

Kiufupi fastjet si ndege ya kupanda labda waboreshe management yao ya sasa hivi la sivyo itafikia hatua watu hawatapanda kabisa ndege zao.
Mjirekebishe fastjet nyie ni kampuni ya nyumbani tunawategemea mfike mbali na kutanua anga za kuvuka Africa
 
Mleta mada nakupa pole Kama bado unapanda hiyo basi ya angani,
Nimepanda mara kadhaa kwenda South Africa yaani utafikiri nipo kwenye basi tu, kila kitu kinauzwa ndani ya ndege yaani hakuna utofauti utadhani Sio international route

Kiufupi fastjet si ndege ya kupanda labda waboreshe management yao ya sasa hivi la sivyo itafikia hatua watu hawatapanda kabisa ndege zao.
Mjirekebishe fastjet nyie ni kampuni ya nyumbani tunawategemea mfike mbali na kutanua anga za kuvuka Africa
Kampuni ya uingereza
 
Mkuu Fastjet ni jipu linalijitegemea. Sasa hivi ukibook tiketi online wanatoza dola tano ili wakuwekee nafasi afu baada ya mda mfupi wanafuta booking afu vituo vyao vya kulipa kwa cash ni vichsche na hawataki kulipia kwa mtandao. Ni wahuni hao .
 
Kwa sasa napanda kwa vile ndiyo ndege kubwa huko juu haizingui sana na unatumia muda mfupi kufika. Kungekuwa na mbadala wangeisoma namba:D:D
 
Uswahili maana yake nini?
Huna tofauti na wale wanaovaaga tisheti zimeandikwa "NO HURRY IN AFRICA"
 
Scandinavia pia mwanzoni ilikuwa raha sana, baadaye ikaja kuwa ovyo kabisa, mwishowe ikafa
 
hii ni shida unabook on line wanacharge dola 5 ukienda kununua tikete kwa wakala elfu tano tsh. ukiingiia kwenye ndege unauziwa vitu wanaboa sanaa
 
Jamani Specificity nimependa hapo 'Mkuu Fastjet ni jipu linalojitegemea'!?! Management irekebishe hayo jamani maana inasaidia sana kwa upande wa bei!
 
Duniani usafiri wa ndege ni usafiri salama na wafanyakazi wake ni watu wenye weledi wa hali ya juu na kumjali mteja, lakini ghafla shirika hili la ndege (Fastjet) wameamua kwa makusudi kuingiza uswahili katika biashara hii ikiwemo KUAHIRISHA/KUFUTA SAFARI bila taarifa za mapema, kuchelewa kupokea simu ya huduma kwa wateja (+255784108900) na kutokutoa majibu sahihi kulingana na tatizo la mteja, lugha mbovu kwa wateja. Naiona Fastjet kama kampuni ya daladala kwa sasa. Mnaboa.
Hawa hawakuanza leo mbona???
 
Jamaa wanazingua kweli kweli nililipa ticket tangu mwezi wa 12 mwaka Jana kwa Mpesa sikupata ticket wakaanza kunizingua ikabidi nikate nyingine wakasema pesa itarudi mpaka Leo bado wananizungusha Mara tunawasiliana na voda Mara hv kila siku drama sasa natafuta dawa yao iko jikoni
 
yaani wamekuwa na mambo ya kipuuzi , kupindukia . Tiketi unayotaka kuinunua kwa kutumia mtandao imepewa expire ya dakika 12, na hii network yetu!, upuuzi mwingine ukiisha maliza lipa hela baada ya expire time pesa hairudishwi kwa wakati.

yaaani hawa nao kweli ni JIPU LINALOJITEGEMEA
 
Hawa fastjet wababaishaji.. nilifanya booking ya mbeya dar nikapewa reference number ba time limit ya kulipa ambayo ilikuwa inaisha leo saa tano. Jana jioni nikaweka ela mpesa ili nilipie maana ndivyo uwa ninafanya nikalipa ela ikakatwa. Baada ya muda nikapikea msg kuwa wrong reference number your money will be refunded within a few days.
Ikabidi niwapgie customer care akapokea dada flani nikamueleza. Akaniambia sijakosea reference number ila ni kwamba system yao ya malipo ina shida hivyo nifanye booking upya na nikalipie kwa wakala au ofisini kwao; kuhusu ela yangu itarudi ndani ya siku tatu.
Kufanya booking upya malipo ni mara mbili ya awali na je wana hakika gani kuwa mimi nina ela. Nilipomuuliza hilo swali akanijibu kuwa hawezi nisaidia.
Fastjet hawafai
 
Back
Top Bottom