Wengi wetu tunadhani kuingia kwenye biashara kubwa ni LELEMAMA; Kila kazi inahitaji kufuata KANUNI na TARATIBU za kufuata ili kuweza kuduma na kuwa RELIABLE, vinginevyo tutasikia inakuwa HISTORIA.
Wengi wetu sio wote kama ni Watanzania tumeshasikia juu ya huduma na mashirika yaliyovuma sana kwa nguvu ya kiutendaji na kiuchumi enzi za miaka ya 1970's na 80's ila leo hayapo, km TAZARA, NASACO, AIR TANZANIA, na hata TANESC0 enzi hizo, bila kusahau NATIONAL PANASONIC MATSUSHITA sina maana hii ya Japan (ni ile iliyokuwa Nyerere Rd, zamani Pugu Rd karibu na TCC.)
Leo hii havipo kabisa imebaki historia tena ya kutafuta.
Mafanikio ya kudumu iwe kwa kiwango cha mtu binafsi, jumuia, nchi au hata kampuni huhitaji NIDHAMU isiyoteteleka na ya kudumu itakayofanywa kama mtindo wa maisha ya kila siku au utamaduni wa watu/mtu/taasisi husika.
Vinginevyo, tutafanya mambo kwa kukurupuka au kuiga au kuigilizia ambayo hupelekea kushindwa vibaya sana na kupotea kabisa katika ulinwengu wa tasnia husika.