Fasihi ya Mtandaoni ya China yaleta mageuzi makubwa na kupanua soko lake la wasomaji hadi nje ya nchi

ldleo

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
1,010
1,035
微信图片_20230529140722.jpg


微信图片_20230529140716.jpg


微信图片_20230529140728.jpg


Fasihi ya Mtandaoni ya China imefanikiwa kukonga nyoyo za wasomaji duniani kote kutokana na mtindo wake wa kipekee wa kusimulia hadithi, mandhari na kuchanganya mambo tofauti ya kitamaduni. Inatoa mtazamo mpya na unaovutia juu ya fasihi ya China, inayozingatia mambo mbalimbali yanayoteka wasomaji wa ndani na nje. Kutokana na kuongezeka kwa umaarufu wa fasihi za mtandaoni za China, wachapishaji na waandishi wanachunguza njia mpya za kutangaza kazi zao na kufikia hadhira pana, na hivyo kutengeneza soko linalozidi kupanuka la fasihi mtandaoni.

Kutokana na juhudi kubwa za waandishi wengi wa riwaya za mtandaoni wa China sasa utamaduni wa China umekuwa ukijulikana zaidi nje. Waandishi hawa wa vitabu wanajivunia kwa kuipaisha fasihi ya China na kuifanya historia ya kale kuvutia wasomaji wengi wa mtandaoni.

Akielezea sababu ya kupata mafanikio katika utungaji na uandishi wa riwaya zake kwenye mtandao, mwandishi wa kitabu cha Maktaba ya Njia ya Mbinguni Library of Heaven's Path” Bw. Yang Hanliang anasema yeye katika mchakato wa uumbaji wa hadithi zake, kwanza huwa anahakikisha anatengeneza hadithi iliyo bora zaidi, kwani hadithi ikiwa nzuri ndio inawavutia wasomaji wengi zaidi kuendelea kuifuatilia. Lakini muhimu zaidi ni mtindo wa waandishi wa China kuingiza kipengele cha utamaduni wa China ambacho kimekuwa kama lulu na kuvutia zaidi hisia za wasomaji.

Akifafanua zaidi kuhusu kitabu chake cha Maktaba ya Njia ya Mbinguni Bw. Yang anasema wakati alipoandika riwaya hii, aliona jukumu lake kubwa wakati huo ni kama mwalimu ambapo ni lazima afundishe na kuondoa mashaka ya wanafunzi wake. Kwenye kitabu hicho alimtumia mhusika
Zhang Xuan ambaye alizaliwa katika ulimwengu mwingine na kuwa mwalimu, na baadaye maktaba ya ajabu ghafla ikaja ubongoni mwake, na tangu hapo akaanza kujua mapungufu na udhaifu wa kila mtu na kila kitu. Bw. Yang pia anasema Fasihi ya mtandaoni ya China inabeba jukumu muhimu katika mawasiliano ya kitamaduni kati ya China na nchi za nje. Kwani inatoa fursa kwa wasomaji wa kigeni kuweza kujua historia, mila, desturi, itikadi na utamaduni wa China.

Maendeleo ya riwaya za mtandaoni za China, yamepelekea soko lake lipate mabadiliko makubwa, ambapo sasa tunashuhudia tamthilia, katuni na hata filamu nyingi zinazotokana na riwaya hizo zikizalishwa. Wakati huo huo, kwa mujibu wa ripoti, fasihi za mtandaoni zimekuwa chanzo kikubwa zaidi cha bidhaa za hakimiliki za kitamaduni za China zinazouzwa nchi za nje, na hata upatikanaji wake umepanuka kutoka Kusini-Mashariki mwa Asia, Kaskazini-Mashariki mwa Asia, na Amerika Kaskazini hadi Ulaya na Afrika, na kutoa fursa kwa waandishi wa China na wachapishaji kupanua soko lao la wasomaji nje ya China.
 
Back
Top Bottom