China yapinga na kulaani vikali Uingereza kuingilia mambo yake ya ndani

ldleo

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
1,061
1,070
1713408198840.png


Hivi karibuni, China ilipinga vikali ziara zilizofanywa na ujumbe wa “Marafiki wa Taiwan” uliojumuisha baadhi ya wabunge wa Chama cha Leba cha Uingereza kisiwani Taiwan. China imesema, ziara hiyo ni ukiukaji wa wazi wa kanuni ya China moja na uingiliaji wa ndani wa mambo ya China, na kwamba ziara hiyo inatoa picha hasi kwa nguvu za ufarakano kisiwani humo zinazotaka kile wanachokiita “Uhuru wa Taiwan.”

Ziara hiyo ambayo inafanyika baada ya Uingereza kuituhumu China kwa walichokiita udukuzi wa mtandaoni na kuilaumu China kwa utekelezaji wa Kifungu cha 23 cha sheria mkoani Hong Kong na pia suala la Bahari ya Kusini ya China, inachukuliwa kama mbinu nyingine ya kisiasa ambayo baadhi ya wanasiasa wa Uingereza wamekuwa wakiitumia kama kigezo cha kujitafutia uhalali, na kutoa ishara ya athari hasi kwa uhusiano wa China na Uingereza.

Ubalozi wa China nchini Uingereza umelaani vikali ziara hiyo, na kuwataka wanasiasa wa Uingereza kuacha kukiuka kanuni ya China moja na kuingilia kati mambo ya ndani ya China. Ubalozi huo pia umesema, wanasiasa husika wa Uingereza wanapaswa kufahamu kuwa, vitendo vinavyoathiri maslahi ya China vitajibiwa kwa nguvu inayostahili.

Ujumbe wa watu saba ukiongozwa na Bwana Sonny Leong, mwenyekiti mwenza wa Marafiki wa Taiwan kutoka chama cha Leba, uliwasili Taiwan Machi 30, na kupanga kukutana na kiongozi wa Taiwan, Tsai Ing-wen, kuzungumzia uhusiano wa biashara na uvumbuzi wa teknolojia kati ya Uingereza na kisiwa cha Taiwan.

Ziara hiyo pia inafanyika baada ya onyo lililotolewa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza David Cameron kuwa kukifungia kisiwa kutaathiri uchumi wa dunia wakati wanasiasa wa Uingereza wakitumia kauli isiyo ya kweli ya “tishio la China” kwa kudai kuwa “watu wenye uhusiano na serikali ya China” wanahusika katika mashambulio ya udukuzi dhidi ya taasisi za kidemokrasia za Uingereza na wabunge, na hii ni baada ya Uingereza kutangaza vikwazo dhidi ya watu binafsi na kampuni za China.

Mkurugenzi wa Kituo cha Elimu ya Uingereza katika Chuo Kikuu cha Elimu ya Kimataifa cha Shanghai, Gao Jian anasema, Uingereza inapaswa kutambua kikamilifu kuwa, haina nguvu na utayari wa kweli wa kuingilia suala la Taiwan na Bahari ya Kusini ya China, na kwamba, vitendo hivyo vya uchochezi havitaweza kufanikiwa wala kuwa na athari halisi katika maslahi makuu ya kidiplomasia ya China. Pia anasema, Uingereza inafahamu fika kwamba sualala Taiwan ni nyeti sana katika sera ya nje ya China na halipaswi kuguswa, hivyo Uingereza haiwezi kuhatarisha maslahi yake yenyewe ya kidiplomasia kwa kugusa mstari mwekundu wa China, ambao ni suala la Taiwan, hivyo, vitendo vidogo vya uchochezi vinaweza kuonekana kuwa havina maana, na pia havina nikakati wala kanuni yoyote halisi ya kidiplomasia.

Profesa Cui Hongjian wa Academia ya Uongozi wa Kikanda na Dunia katika Chuo Kikuu cha Mambo ya Kigeni cha Beijing anasema, sababu ya baadhi ya wanasiasa wa Uingereza kutoa kauli ama kufanya vitendo vya uchochezi kuhusu suala la Taiwan ni kwamba wanataka kuwa na kigezo cha kujitafutia uhalali wa vitendo na kauli zao hizo.

Pia Profesa Cui amesema, licha ya Uingereza awali kuonyesha ishara ya kushirikiana na China, ikiwemo katika Nyanja za uchumi na biashara ambako wana mahitaji makubwa, msimamo mzima wa sasa kwa upande wa Uingereza unaonekana kutotoa kipaumbele katika dimplomasia.

Anasema, hata ndani ya uwanja wa masuala ya kigeni, masuala kama vile uhusiano na Marekani, vita ya Russia na Ukraine, na uhusiano na Ulaya, yanaweza kuonekana kuwa muhimu sana kwa Uingereza. Hivyo, kama hakuna kitu kikubwa kitakachotokea, uhusiano kati ya China na Uingereza utaendelea kuwa wa baridi katika mwaka huu.
 
Back
Top Bottom