Farewell-Kwaheri Regia: A Tribute Page

Farewell-Kwaheri Regia: A Tribute Page

KWA KUA NILIKUA NAMFAHAMU Regia akiwa anasoma pale forodhani, kweri ni mtu ambaye hakua na woga wala kujiona ni tofauti na watu wengine sababu ya ulemavu wake, ni kweri tanzania hasa vijana tumepata pigo jingine kwa kuondokewa na mpendwa wetu Regia, pole nyingi sana kwa pacha wake (kulwa)
 
Kweli mtu wa MUNGU akifa nguvu ya upendo humvuta kila mtu kwa kifo chake. Sikuwahi kuzungumza na wewe lakini kifo chako kimenigusa sana.

Namwomba MUNGU ainue akina Regia wengine wengi kwa faida ya Taifa Letu.

Pia huu ni wito kwa wale wanaotumia majina yasioeleweka waanze kutumia majina yao sahihi kaka kamanda Regia Mtemanyenje.

RIP Regia Mtemanyenje.
 
Sina jipya ila simanzi tupu tumekuwa na the late regia tangu sekondari,chuo kikuu na hatimaye tumekutana chadema na sasa mauti yamemchukua mapema mno.ila tuamini kwamba kazi ya mungu haina makosa.
 
Ulazwe pema mpendwa! Tutaendelea kuyapigania yale uliyoyaamini
 
R.I.P Dada....umeacha mengi huku duniani.
Tuliobaki tuombe tujaaliwe kuendeleza yale uliyoyaacha.
 
Bwana ametoa Bwana ametwaa jina lake libarikiwe. Hakika nyota imezimika. Mungu awape faraja ndugu zake na wale wote wanaoguswa. Wote tuchukue tahadhari kubwa wakati tunaendesha gari au kuwa ndani ya gari hasa pale tunapotaka kuovertake gari lililosimama au linalotembea. Ajali nyingi zinatokea hasa kwenye mazingira kama haya. Nakumbuka ajali ya wanakwaya wa Ambassodor Rwanda iliyopoteza watu watatu pia ilikuwa kwenye scenario ya kuovertake gari lililosimama kisha kukutana na gari lingine. Wale wanaoendesha viongozi wetu au viongozi wetu wanaoendesha magari ni vizuri wangehudhuria kikamilifu mafunzo ya udereva wa kujihami (Defennsive Driving Course) zinazotolewa na vyuo vinavyokubalika kuepusha hasara kama hizi kwa watu muhimu kwa taifa. Kama hakuna chuo kuna makampuni makubwa ya kimataifa hasa ya mafuta yanatoa mafunzo haya (DDC) wanaweza kuwapata wakufunzi waliobobea wakawasaidia.
 
Hakika tutakukumbuka sana Regia. Nakumbuka mapambano yako katika uchaguzi mkuu 2010, michango yako bungeni hasa changamoto uliyowapa wasomi kutumia usomi wao kulikomboa taifa nk. Tutakukosa forever hapa duniani, lakini iko siku tutaonana sehemu tofauti.

Mungu ailaze mahali pema peponi roho yake - Amina
 
Hii ni kwa ajili ya tributes za Regia; kama unalo zuri la kusema kumhusu yeye au kumbukumbu yako njema tushirikishe.



Nyota Imezimika




Ni pigo limetufika
Nashindwa la kutamka
Ilikuwa inawaka
Sasa nyota yazimika
Nabaki natetemeka
Machozi yanadondoka!
Namlilia Regia, ni nyota imezimika!

Mwanga ametuachia
Mbele ametangulia
Kaitwa kaitikia
Japo tulitamania
Aishi kitambo pia
Tuijenge Tanzania
Namlilia Regia, ni nyota imezimika!

Ee Mola nakuabudia
Utukufu nakurudishia
Kwa maisha ya Regia
Jinsi ulimtumia
Tupe na nguvu Jalia
Mfanowe kufuatia
Namlilia Regia, ni nyota imezimika!

Nashindwa kuendelea
Majonzi yamelemea
Pema ninamuombea
Rafiki nilimzoea
Mwanga utaendelea
Mapambano yanaendelea
Namlilia Regia, ni nyota imezimika!​


Nimepokea kwa masikitiko makubwa, kutokuamini na mshtuko taarifa za msiba wa Mhe. Regia Mtema. Kifo chake kimekuja wakati ambapo moto wa mabadiliko nchini umekuwa ukipamba kwa kasi zaidi na nyota yake ikizidi kuangaza kila kukicha. Regia alikuwa ni mmoja wa vijana ambao wametupa matumaini kuwa kuna vitu vinawezekana nchini na vinaweza kufanywa na vijana.

Msimamo wake, uthabiti wake na kujiamini vilikuwa ni tunu ambazo zilimsimamisha bila woga kutetea kila alichoamini. Kwa baadhi yetu ambao tumepata nafasi ya kuzungumza naye nje ya mitandao hii na wale ambao tumemjua kwa muda mrefu kabla ya kuibuka na kuwa mwanasiasa tunaweza kusema kuwa Regia alikuwa ni mwanasiasa aliyesukumwa sana na moto wa mabadiliko. Moto ambao alitamani kuwa sehemu yake katika kuona cheche zake zinawafikia wengi zaidi.

Alitamani kuiona Tanzania ikiwa bora zaidi na ambayo watu wake wanafurahia matunda ya nchi yao kwa haki, usawa na umoja. Tunaposema alikuwa ni mwanaharakati hatutii chumvi. Wengi tumeshuhudia jinsi ambavyo amekuwa ni miongoni mwa wanasiasa ambao wamekomazwa kwenye mitandao hii. Amekuwa jasiri kuliko wanasiasa wengi wakongwe kuja na kupitishwa kwenye tanuru la maoni ya JF na kila wakati ambapo ulifikiria kuwa labda amekwazika na hatorudi tena Regia alirudi na alirudi akiwa mpya kabisa. Aliweza kusimama katika moto bila kuungua na kama aliungua haikuwa rahisi kujua!

Kwa upande wangu, Regia alikuwa ni mshiriki mkubwa wa mambo mengi ambayo nimeyafanya na yeye ameyafanya. Aliponiomba wakati wa kampeni ya 2010 kumsaidia kupitia Ilani yake kwa Wana Kilombero niliona ni heshima ya pekee. Mapema mwaka huu tulikuwa tumeanza kuzungumzia baadhi ya mambo ambayo tungeweza kuyafanyia kazi kwa kushirikiana na wengine katika Bunge lijalo. Bahati mbaya mbingu imebadili mipango hiyo. Ninaamini hata hivyo huko aliko anatutie shime ya kuendelea kutekeleza mipango mbalimbali.

Regia alikuwa mchangamfu, mcheshi, mwenye kupenda utani, na kwa hakika kabisa alikuwa makini. Kitu kimoja ni kuwa hakuogopa kusema alichokuwa anafikiria au kilichomgusa moyoni. Alisema hisia zake na na mawazo yake pasi ya kutaka kuonesha kumwogopa mtu au kumpendelea mtu. Aliamini katika kutetea msimamo wake na akishawishiwa kuona mapungufu hakuchelewa kujirudi. Kwa kweli haikuwa rahisi kuzungumza naye bila kujikuta unatabasamu. Alikuwa amejaliwa kipaji cha kujenga urafiki na watu wengi na hata kuwa kwake Mbunge hakukuwa kwake kiuzizi cha kuwa karibu na marafiki zake. Hakujiona ni “kigogo” wa aina fulani aliyependa kutukuzwa au kuogopwa. Alijiona yeye ni mwanasiasa na kweli alikuwa hivyo. Lakini alikuwa ni zaidi ya mwanasiasa - alikuwa ni binti wa Kitanzania aliyejaliwa vipaji vingi na mwenye njozi nyingi kwa nchi yake!

Rambirambi zangu nyingi - na labda nawasemea wengine vile vile - ziwaendee familia yake ya Mzee Estelatus Mtema pamoja na tena kwa namna ya pekee kwa pacha wake Remija Mtema. Remija kuliko mtu mwingine yeyote duniani amepoteza sehemu yake na mzigo huu ni mkubwa kupita kiasi. Wakati kwa wengi wetu tumepoteza rafiki, mwanaharakati, mwanasiasa na mshirika wa mabadiliko kwa ndugu zetu hawa wamepoteza binti, dada, shangazi na ndugu yao wa karibu. Ni msiba mkubwa kwao. Nawaombea faraja wote hawa na wale wote ambao wameguswa na msiba huu mkubwa.

Mungu ailaze roho ya Marehemu Regia pema peponi na atujalie sisi wengine dhamira na kiu ya kuendeleza na kusimamia kile ambacho dada yetu alikisimamia na kukipigania. Namna sahihi ya kuenzi maisha ya Regia ni kuendelea kuipigania Tanzania na Watanzania bila kujali jambo jingine lolote linalowatofautisha kama mtu mmoja mmoja.

Hata kama nyota imezimika, mwanga tulioushuhudia unatupa matumaini kuwa zipo siku njema mbeleni!

Mpaka Tuonane tena Paradiso!

MMM


Ciao Regia !!!! Grazie di Tutto
 
Last edited by a moderator:
RIP RM !
ALWAYS U WILL REMAIN A SHINING STAR :
>ALL OVER KILOMBERO & ULANGA.
>ALL OVER TANZANIA.
And
>FOREVER HERE IN
JF !
 
Ni nyota iliyozimika ghafla sana wakati ndio kwanza iliianza kumulika. niliwahi kupita ifakara nikakuta mkutano uliokusanya umati mkubwa sana hali iliyoonyesha kukubalika kwake mbele ya wananchi, na ilikuwa ni ishara tosha kuwa angefika mbali kisiasa. Tunasema kazi ya Mungu haina makosa, pamoja na huzuni nyingi tulizonazo lakini tuzidi kumuombea marehemu na hasa familia yake iliyopigwa na butwaa kuhusu msiba huu mkubwa. RIP commando!
 
Japo hatutaiona sura yako,
Japo hatutaisikia sauti yako
Japo hatutaona macho yako
DAIMA TUTAENDELEA KUWA PAMOJA.

Kwetu Regia u mzima, unaishi ndani yetu na tuko pamoja DAIMA.
 
Baadhi yetu wana JF tuliokutana msibani leo katika Ibada pale Kanisa katoliki Segerea, tumeamua kwamba tutapanga siku maalumu hivi karibuni na tutakutana British Council na kujadili yale yote aliyosimamia Regia na nini cha kufanya ikiwa ni namna ya JF kumuenzi marehemu. Yote tutayajulisha maana tutashirikiana na uongozi wa JF.

Mimi si mwandikaji sana, lakini leo wacha niandike machache.Machache haya ninayoweza kusema ni kuwa, Mwaka 2010 tulipoendesha shindano la "JF Woman of the Year 2010" Regia alichaguliwa na Wana JF na akashinda. Hii ni uthibitisho tosha kuwa Regia alikuwa anapendwa, anathaminiwa na anakubalika katika hoja zake. Ni Regia huyu huyu aliyethubutu kuweka pembeni ID yake ya JF ya "Gender Sensitive" na kutumia jina lake halisi Regia Mtema! Ni wachache sana wanaweza na wanaojiamini kwa hilo.

Lakini kikubwa na ambacho wengi hamjui ni kuwa, katika Mwaka wa uchaguzi 2010 JF ilijizolea umaarufu sana toka ndani na nje ya Nchi katika kutoa habari za uchaguzi mkuu. Binafsi niliendesha threads kuu kama za Uzinduzi wa Kampeni wa Chadema jangwani, Uzinduzi wa Kampeni wa CCM ambayo yote ilifanyikia jangwani. Reporting ile ilikuwa ni LIVE nikiaangalia TV, kusikiliza na hatimaye kuandika kadiri nilvyoona katika Luninga na huku napost JF. Hii ilifanya baadhi wakaniita "Mzee wa Matukio"

Wakati wa Uzinduzi wa Kampeni wa CHADEMA wote mnajua kuwa Matangazo yalikatishwa na TBC. Ni katika kipindi hiki nilianza kuhaha ni vipi sasa nitawaletea wadau matangazo live. Unajua kipindi kile kulikuwa na watu wengi sana online. Na wengi walisononeka. Niliwasiliana na Maxence (Founder wa JF) na kumuuliza kama kuna mtu yeyote anaweza akanisaidia kupost live ambaye yuko jangwani.

Maxence alinipata namba ya simu ya Regia, akaniambia yuko Jangwani na atakupa updates zote. Huo ndiyo ukawa Mwanzo wa Mimi na Regia kufahamiana. Mwanzoni nilimjua tu kama Gender Sensitive na Baadaye Regia Mtema.

Naam . . . Nilipompigia Regia akaniambia kuwa haina tabu, yeye atanipa updates kwa simu, naam, hatukukata simu, Yeye akieleza matukio na hotuba nami pia nikisikiliza kwa mbali na wakati huo huo nikipost JF. Huyo ndiye Regia ninayemfahamu ambaye alikuwa tayari wakati wowote kufanya kile anachokiamini na kukusimamia. Ulemavu wake wa mguu kweke yeye haukuwa na nafasi ya kumnyima fursa yoyote au kufanya jambo lolote alilitaka. Wakati mwingi aliwazidi hata wasio na ulemavu wowote.

Niliposikia msiba huu, niliumia. Na leo sikuwa na jinsi, ilibidi nisitishe kila kitu na kwenda kumwaga Mwanamapinduzi huyu, naamu, Kumwanga Regia.

Kwa heri Kamanda Regia, kalale pema peponi Kamanda, umefanya sehemu yako. Inatupasa na sisi tufanye sehemu yetu na kuiga na kuendeleza mazuri yote aliyoyafanya.

Regia, wewe ni kama Mshumaa uliokuwa unaleta Mwanga wa matumaini katika kiza kinene sana na sasa Mshumaa huo umepulizwa na upepo na kuzima.

Regia, yo are a Tanzanian Rose & Gold, you are like Candle in the wind.

We will miss you Regia. You were the JF icon.

Kalale pema peponi Kamanda

Amen.
 
Mungu hutukumbusha jinsi ya kumtumikia kwa haki kwa kuwaita kwake,wapendwa wetu!
 
Tuwe na jicho la imani na tumwombee,Tujifunze kutoka kwake.Kwa heri Regia umetuachia pengo upumzike kwa amani
 
Back
Top Bottom