Hapo ndio tatizo linapoanzia.Mimi ninavyo fahamu mbadala wa FAO la kujitoa ni unemployment benefit, sasa hii bima ya afya inakujaje tena? Naomba ufafanuzi no kama sielewi hivi!
Hii kitu alionywa lakin hakusikia.. akajitapa hii nchi ni tajir so misaada haitaji.Ni Kweli kaka, Katika Nchi hii mitaji ya biashara ni ngumu kupata na mikopo hakuna
Mkombozi wa Mtanzania Mnyonge ilikuwa FAO LA KUJITOA
Nchi kunyimwa misaada ni kiburi cha watawala....
Unajua nimeshangaa sana... nani ni think tank wao? Anawapa mawazo ya kijinga kama haya.Wanatulazimishia magonjwa? Bima ya afya itamsaidiaje MTU kujikwamua kiuchumi baada ya ajira kukoma ?wasipougua je ?tuache uhuni.kwani walikuwa na mkataba wa fedha yao kugeuzwa bima ya afya ?
Jipe moyo tu, CCM mnaweza kuing'oa kwa Tume ya akina Jecha na Katiba hii?Hakuna shida, miaka minne ijayo tuna wa replace hawa baffoons na viongozi wangine. Fao letu litarudishwa tu
Dodoma. Serikali imesema fao la kujitoa halipo,badala yake imekuja na fao la bima ya afya.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bungena Vijana), Jenista Mhagama alisema hayo bungeni
jana kuwa suala la fao la kujitoa haliwezekani kwa sasa na badala yake imeanzisha mchakato wa fao la
bima ya afya ambalo itakuwa ni mbadala wa fao la kujitoa.
“Katiba ya Tanzania katika kifungu cha 11
kinaeleza namna ambavyo mifuko hiyo
(akimaanisha ya hifadhi ya jamii) inapaswa kuwa,
lakini hata juzi Mheshimiwa Rais aliagiza
utengenezwe utaratibu katika bima ya mfuko na
itakuwa ni mbadala wa watu wasiokuwa na ajira,”
alisema Mhagama.
Mapema bungeni jana, swali kuhusu malipo ya mafao kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii liliwaibua wabunge wengi waliotaka kuuliza maswali ya nyongeza licha ya mawaziri kutoa majibu.
Akijibu swali la wafanyakazi waliopatikana na vyeti feki kama wanaweza kulipwa mafao yao Waziri wa Utumishi Angella Kairuki ali hatuwezi
kutoa taarifa kwa sasa kwani bado
wanashughulikia jambo hilo ili kuona namna bora ya kufanya na wakifikia hatua nzuri watatoa majibu ya kuaminika na kuomba wapewe muda kwa sasa
Mapema mbunge wa Viti Maalumu,
Amina Mollel alitaka kujua kwa nini wafanyakazi waliopatikana na vyeti feki wasilipwe mafao yao.
Naibu wa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu(Sera, Uratibu na Bunge), Anthony Mavunde alisema kuanzishwa kwa mifuko ya jamii kumefikia hatua mbalimbali ikiwamo kukamilika kwa tathimini ya mifuko ya hifadhi ya jamii
(actuarial evaluation) ambayo imetoa mapendekezo kuhusu namna bora na mambo ya kuzingatia katika kuunganisha mifuko ya hifadhi ya jamii.
“Mpaka sasa Serikali haijafanya uamuzi rasmi wa idadi ya mifuko itakayobaki baada ya kulinganisha mifuko iliyopo hivi sasa,” alisema Mavunde.
Chanzo..Mwananchi

Naomba ujumbee huu uwafikie wahusika wenye mamlaka, labda wanaweza kulitazama upya hili sualaKuhusu fao la kujitoa wafanyakazi hatujui haki zetu,inakuwaje mtu contract yako iishe wakwambie usubiri miaka 55? Kama ni hivyo tunataka kwanza waje nasheria ambayo inasema unaajiliwa in terms of parmanent basis,Halafu viongozi wetu vichwa nazi hawajui athari za watu kutokuwa na ajira?
We ukinipa hela yangu nitaanzisha biashara au kilimo nitalipa kodi sasa nyie vichwa nazi nani amewaambia mninyime jasho langu?
Nyie vichwa Nazi mnaosema Tanzania ni yetu sote kama mimi ni sehemu ya Tanzania mbona mnataka kupola jasho langu ambalo limenivuja huku mkiomba niteketee na familia yangu? Mbona mmekuwa kama wakoloni.
Nyie vichwa nazi mnaoomba Tanzania yenye amani wakati mnataka kupola fao langu na familia yangu huku nyie baada ya miaka mitano au kumi mnalipatana mamilioni tena kwa kodi yangu ya PAYE na mnataka kupola fedha yangu kidogo.
Mheshimiwa Rais mimi si mwanasiasa kwa hili angalia nyuma, Wengine hatuna sehemu ya kusemea,Wengi ambao tunalia kuhusu hili fao la kujitoa ni wale watoto wa wakulima,usitegemee watoto wa akina Mbowe,Lowassa,Pinda,Membe,Maghembe,Mengi, Jenista Mhagama,Kabudi,Tundu Lissu,Ndugai na etc watakuja kulialia kama sisi,hawajui shida,Watoto wao hawajawahi kwenda shule bila viatu,hawajawahi kunywa uji wenye chunvi,hawajawahi kula ugali wenye wadudu kule bording,hawajawahi kusomea vibatari,hawajawhi kung'atwa na kunguni na kwenye ajira ni mwendo wa memo tu,
Hao watoto contract zao zikiisha tu kesho tu kalamba dume,Sisi watoto wa masikini kupata kazi nyingine inachukua muda na inawezekana usipate kabisa,Mheshimiwa Rais hizi ni sauti za wafanyakazi iliayo toka nyikani tafadhali hili usidharau, hao uliowapa madaraka hawana uchungu na sisi watoto wa masikini akina kayehura anisamehe kama nimekosea jina lake,Erio hawakukuchagua hawana cha kupoteza.
Baba mbona wamachinga uliwasikiliza sisi wa Sector binafsi unataka kutunyima fao letu? Angalia migodi inafungwa kwamba wanaingia hasara uzalishaji unapungua,Tanzanite one watu waliachishwa kazi wapo mtaani, Fastjet,Tigo kwa wahindi ndiyo maelfu,The Gurdian,TBL nakadhalika.
Serikali,Wabunge, Mahakama,Waajiri,Wafanyakazi na Wananchi hili suala linagusa masilahi ya mtu ambaye ni mfanyakazi,Wabunge ambao mnatuona wafanyakazi si lolote,Kwa sababu mnakopa kwenye mifuko yetu,mmegeuka wanyonyaji wa watanzania badala ya kuwasaidia eeh mungu tusaidie tuepshie mbali na hawa waliojaa shibe.
Mwisho mheshimwa Rais hata hao viongozi wetu ni walewale ambao wanapatikana kiujanjaujanja tu,hawapo kwa ajili yetu kwa ajili ya matumbo yao chaguzi zetu hazina tofauti na zile za vyama vya Siasa Rushwa tupu.
Hili fao la kujitoa linagusa vijana wengi ambao ndiyo nguvu kazi ya Taifa,Wazee haliwahusu kwa sababu wanauhakika baada ya miaka miwili mitatu wanachukua chao hata ukiangalia hao viongozi wetu ungewauliza nani ameajiliwa kwa mkataba hayupo hata mmoja ndiyo hawawezi kutusemea.
Njaa huleta wivu,husda,hasira na chuki katika Jamii,ehhee mungu tuokoe na dhulumama kwenye nchi yangu.
Nchi ya viwanda![]()
![]()
![]()
mkuu hilo sahau ukaguzi wa vyeti tu wemejitoaaaa,kama vile wao ni watumishi wa wakoloni ijekua mambo ya hela?.
Ndiyo kinacho waokoa.Wanajuwa, kwani walipomkatalowassa walishinda kwasasa hawana wasiwasi, ikishindikana sana jecha yupo.