Fao la kujitoa lafutwa rasmi

Fao la kujitoa lafutwa rasmi

Hv hawa watu wanaakili timamu kabisa?hawaoni rate za retrenchement makazini hasa private sector wanataka watu wakaishije?mnasema wajiajiri watajiajiri vp wkt pesa zao walizozihangaikia mwezi mzima mmezifungia.
Magu akija anasema safi zifungieni tu watu walikua wanatumia hovyo hovyo dohhhhh tumepatikana jmn
 
Sasa sie wafanyakazi inatubidi tutii heshima kwa waajiri wetu,yaani tuwanyenyekee
 
wabunge wawatetee wananchi. Unemployment benefit kama ndio wanamaanisha iwe replaced na bima ya afya sio sawa...
 
Namba namba namba, aliyetutungia huu wimbo yeye alishasoma namba, akatangulia mbele za haki! r.i.p
 
Wabunge wote ni vilaza. Yaani hakuna hata aliyekemea hiyo hatua? Shame on us
 
nawasihi wabunge kama mnapitia humu, hii ni issue ya dharura. nafikiri hapiti mitaani kwa wananchi wanaofanya kazi za mikataba ya muda mfupi jinsi wanavyoishi..!! laiti mngejua wala bungeni msingekaa. watu wanahangaika kwenda kutafuta mikopo ya riba kubwa kwa mtaji mdogo usioeleweka, watu wanatelekeza familia zao. wake wanaacha familia zao kwenda kufanya uzinzi kupata kipato cha kuhudumia watoto, baba hayupo anahangaikia ajira. kwa nini wasipewe hela yao wakahangaikia biashara ndogo ndogo ? wakati mzazi mwingine anahangaika kutafuta ajira ?
nawasihi wabunge mliangalie hili kwa mapana.
 
Hawa jamaa wanatugeuza geuza tu kama samaki, hawajapanga cha kuwafanyia wenye vyeti feki wakati umewaondoa watu kwenye mshahara, sasa wataishije na nguvu zao zilitumika kujenga Taifa na maisha yao!? Wawarudishe kwanza hatua zikikamilika ndipo wawaondoe otherwise huu ni ukandamizaji wa maisha ya watu
 
1😛esa za rambi rambi Kagera
2😛esaza rambi rambi Arusha
3: Pesa wa wafanyakazi fao lake aliloweka kumlinda
4: Utitiri na kodi za kupitiliza
5:Faini na makusanyo ya Trafiki
6: Kodi ya reli


Eh Mungu tuokoe na hizi dhuluma!
 
Eeeeh mungu kama upo tuokoe mbona nchi yetu tunanyanyasika hivi. Kama Vipi tufanye unavyotaka tufutike sote
 
Mimi ninavyo fahamu mbadala wa FAO la kujitoa ni unemployment benefit, sasa hii bima ya afya inakujaje tena? Naomba ufafanuzi no kama sielewi hivi!
 
Dodoma. Serikali imesema fao la kujitoa halipo,badala yake imekuja na fao la bima ya afya.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bungena Vijana), Jenista Mhagama alisema hayo bungeni
jana kuwa suala la fao la kujitoa haliwezekani kwa sasa na badala yake imeanzisha mchakato wa fao la
bima ya afya ambalo itakuwa ni mbadala wa fao la kujitoa.

“Katiba ya Tanzania katika kifungu cha 11
kinaeleza namna ambavyo mifuko hiyo
(akimaanisha ya hifadhi ya jamii) inapaswa kuwa,
lakini hata juzi Mheshimiwa Rais aliagiza
utengenezwe utaratibu katika bima ya mfuko na
itakuwa ni mbadala wa watu wasiokuwa na ajira,”
alisema Mhagama.
Mapema bungeni jana, swali kuhusu malipo ya mafao kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii liliwaibua wabunge wengi waliotaka kuuliza maswali ya nyongeza licha ya mawaziri kutoa majibu.

Akijibu swali la wafanyakazi waliopatikana na vyeti feki kama wanaweza kulipwa mafao yao Waziri wa Utumishi Angella Kairuki ali hatuwezi
kutoa taarifa kwa sasa kwani bado
wanashughulikia jambo hilo ili kuona namna bora ya kufanya na wakifikia hatua nzuri watatoa majibu ya kuaminika na kuomba wapewe muda kwa sasa
Mapema mbunge wa Viti Maalumu,
Amina Mollel alitaka kujua kwa nini wafanyakazi waliopatikana na vyeti feki wasilipwe mafao yao.

Naibu wa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu(Sera, Uratibu na Bunge), Anthony Mavunde alisema kuanzishwa kwa mifuko ya jamii kumefikia hatua mbalimbali ikiwamo kukamilika kwa tathimini ya mifuko ya hifadhi ya jamii
(actuarial evaluation) ambayo imetoa mapendekezo kuhusu namna bora na mambo ya kuzingatia katika kuunganisha mifuko ya hifadhi ya jamii.

“Mpaka sasa Serikali haijafanya uamuzi rasmi wa idadi ya mifuko itakayobaki baada ya kulinganisha mifuko iliyopo hivi sasa,” alisema Mavunde.


Chanzo..Mwananchi
Ni ppf tu au na nssf?
 
Wanatulazimishia magonjwa? Bima ya afya itamsaidiaje MTU kujikwamua kiuchumi baada ya ajira kukoma ?wasipougua je ?tuache uhuni.kwani walikuwa na mkataba wa fedha yao kugeuzwa bima ya afya ?
 
Back
Top Bottom