Fao la kujitoa lafutwa rasmi

LICHADI

JF-Expert Member
Feb 4, 2015
4,431
12,292
Dodoma. Serikali imesema fao la kujitoa halipo,badala yake imekuja na fao la bima ya afya.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bungena Vijana), Jenista Mhagama alisema hayo bungeni
jana kuwa suala la fao la kujitoa haliwezekani kwa sasa na badala yake imeanzisha mchakato wa fao la
bima ya afya ambalo itakuwa ni mbadala wa fao la kujitoa.

“Katiba ya Tanzania katika kifungu cha 11
kinaeleza namna ambavyo mifuko hiyo
(akimaanisha ya hifadhi ya jamii) inapaswa kuwa,
lakini hata juzi Mheshimiwa Rais aliagiza
utengenezwe utaratibu katika bima ya mfuko na
itakuwa ni mbadala wa watu wasiokuwa na ajira,”
alisema Mhagama.
Mapema bungeni jana, swali kuhusu malipo ya mafao kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii liliwaibua wabunge wengi waliotaka kuuliza maswali ya nyongeza licha ya mawaziri kutoa majibu.

Akijibu swali la wafanyakazi waliopatikana na vyeti feki kama wanaweza kulipwa mafao yao Waziri wa Utumishi Angella Kairuki ali hatuwezi
kutoa taarifa kwa sasa kwani bado
wanashughulikia jambo hilo ili kuona namna bora ya kufanya na wakifikia hatua nzuri watatoa majibu ya kuaminika na kuomba wapewe muda kwa sasa
Mapema mbunge wa Viti Maalumu,
Amina Mollel alitaka kujua kwa nini wafanyakazi waliopatikana na vyeti feki wasilipwe mafao yao.

Naibu wa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu(Sera, Uratibu na Bunge), Anthony Mavunde alisema kuanzishwa kwa mifuko ya jamii kumefikia hatua mbalimbali ikiwamo kukamilika kwa tathimini ya mifuko ya hifadhi ya jamii
(actuarial evaluation) ambayo imetoa mapendekezo kuhusu namna bora na mambo ya kuzingatia katika kuunganisha mifuko ya hifadhi ya jamii.

“Mpaka sasa Serikali haijafanya uamuzi rasmi wa idadi ya mifuko itakayobaki baada ya kulinganisha mifuko iliyopo hivi sasa,” alisema Mavunde.


Chanzo..Mwananchi
 
Dodoma. Serikali imesema fao la kujitoa halipo, badala yake imekuja na fao la bima ya afya.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Vijana), Jenista Mhagama alisema hayo bungeni jana kuwa suala la fao la kujitoa haliwezekani kwa sasa na badala yake imeanzisha mchakato wa fao la bima ya afya ambalo itakuwa ni mbadala wa fao la kujitoa.

“Katiba ya Tanzania katika kifungu cha 11 kinaeleza namna ambavyo mifuko hiyo (akimaanisha ya hifadhi ya jamii) inapaswa kuwa, lakini hata juzi Mheshimiwa Rais aliagiza utengenezwe utaratibu katika bima ya mfuko na itakuwa ni mbadala wa watu wasiokuwa na ajira,” alisema Mhagama.

Mapema bungeni jana, swali kuhusu malipo ya mafao kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii liliwaibua wabunge wengi waliotaka kuuliza maswali ya nyongeza licha ya mawaziri kutoa majibu.

Akijibu swali la wafanyakazi waliopatikana na vyeti feki kama wanaweza kulipwa mafao yao, Waziri wa Utumishi Angella Kairuki ali hatuwezi kutoa taarifa kwa sasa kwani bado wanashughulikia jambo hilo ili kuona namna bora ya kufanya na wakifikia hatua nzuri watatoa majibu ya kuaminika na kuomba wapewe muda kwa sasa

Mapema mbunge wa Viti Maalumu, Amina Mollel alitaka kujua kwa nini wafanyakazi waliopatikana na vyeti feki wasilipwe mafao yao.

Naibu wa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), Anthony Mavunde alisema kuanzishwa kwa mifuko ya jamii kumefikia hatua mbalimbali ikiwamo kukamilika kwa tathimini ya mifuko ya hifadhi ya jamii (actuarial evaluation) ambayo imetoa mapendekezo kuhusu namna bora na mambo ya kuzingatia katika kuunganisha mifuko ya hifadhi ya jamii.

“Mpaka sasa Serikali haijafanya uamuzi rasmi wa idadi ya mifuko itakayobaki baada ya kulinganisha mifuko iliyopo hivi sasa,” alisema Mavunde.

Chanzo: Gazeti la Mwananchi.
 
Back
Top Bottom