Fao la kujitoa lafutwa rasmi

Fao la kujitoa lafutwa rasmi

Jenista aache unaa atakuwa bomba sana
Unaa sio mzur
Kairuk ..awe realistic....anadeal na maslahi za familia na zikilala njaa laana kwake

Tarehe 15/ 5 uhakiki ukiisha wenye vyeti vyao walipwe mishahara ya watu ....laa sivyo wajue wataadhibu watoto.
 
Huu ni upuuz sana sasa unataka mfanyakaz wa migodini asubiri had miaka 55 ndiyo achukue mafao yake huu ni wizi na ni dalili ya serikal kutaka kuibeba hii mifuko baada ya wao serikal kuponda pesa zote za kwenye mifuko ya jamii . kwa mtindo huu kuna haja gan ya kureplace fao la kujitoa kwa kuweka bima afya nazan FAO ambalo lingekuwa sahihi kwa hali hii ni kuweka tu FAO la Unemployment benefit ili mtu akiwa hana kaz basi alipwe pesa had akija kupata kaz


Kwa huu mtindo wa viongoz kujifanya manyapala nawaambia hii nchi tutakuja kutafuta ubaya . kipind hiki bila unafik wamechochea sana chuki kutoka kwa wananchi , hebu angalia huku Mara watumishi hewa(kuna waliosimamishwa wakat sio watumishi hewa) huku wanafunzi hewa , Mara wenye kukosa vigezo vya kujiunga chuo n, huku ukija kuna manyanyaso kibao wafanyabiashara na wafanyakaz wanaishi kama watumwa kwenye nchi yao , hakuna tena Uhuru wa kutoa maoni au kukosoa pale wanapokosea viongoz wa serikal, utata kwenye maamuz ya pesa zetu Leo hii mkuu wa familia anapanga mwenyewe matumiz ya pesa kwenye miradi bila kusubiri idhini ya bunge , vyama vya upinzan hawana haki ya kufanya kaz zao, michango ya misiba inaliwa , michango ya tetemeko hatujui ilipo, kutumbuliwa kwa kuoneana, haya hili la vyeti feki bila huruma watu wanatimuliwa ovyo kuna watu kwa pressure walikaribia kustaafu wanafukuzwa , matokeo yake wengine wana kufa, lakin vyeti feki hivyo mkuu kuna mkuu wake wa mkoa had Leo anamlinda

Yapo mengi sana ya kusikitisha hawa wanaofanyiwa huu ubaya taarifa zao zinasambazaa had vijijin maana huko wapo familia zao wakiona matatizo na kuambiwa ukwel juu ya huu uonezi wa serikal dhidi ya haki yao hakika ule unafuu wa kusema vijijin ni mafala unazid kuondoka , maana na wao wanakosa misaada kutoka kwa hawa waliokuwa wanawategemea


Kuna watoto wa wakulima wsmesoma ualimu had Leo ajira hawapewi na hakuna majibu ya maana juu ya hili

Kuna kukosekana kwa ajira na mbaya zaid naona maisha ni magumu kila muda


Hii na mengine watz watachoka mwisho wa siku hasira zao tutashindwa kuja kuzuia kisa ujinga wa viongoz wetu


Mungu ibarik Tanzania
Kaka waulize TAMICO msimamo wao ni huoi kuhusu hili? Utashangaa wao pia wanasapoti hili fao kufutwa
 
Kwa hiyo wale wanaofanya kazi sekta binafsi kwa mikataba nao watasubiri miaka 50? Hii nchi ni zaidi ya maajabu..
 
Vyama vya wafanyakazi havipo kwa ajili ya maslahi ya wafanyakazi.. hovyo kabisa..
 
Hii mbona ilianzia kwa JK na mtetezi mkubwa wa hili fao kufutwa ni Zito Kabwe, Tundu Lisu, TUCTA, wafanyakazi wa mashirika ya Uma, wabunge walionyesha kupinga hili fao kufutwa ni Mnyika na Jaffo peke yao.
Ukihudhulia mikutano ya SSRA utajua jinsi vyama vya wafanyakazi wanavyosapoti hili fao lifutwe sema wakitoka nje wanapiga siasa, it has nothing to do na Magufuli maana sheria ilipitishwa bunge la JK na wafanyakazi hasa Mining walipokuja juu wabunge wakashtuka lakini NSSF wakisaidiwa na Zito Kabwe bungeni akashawishi kamati ya uongozi ya bunge ikutane kujadili ndo wakaamua sheria isibadilishwe lakini wafanyakazi wapewe mda wakati inaangaliwa jinsi ya kuhandle wale watakao wanafukuzwa kazi.
Muulize Sungusia au hata Mnyika jinsi wabunge wa upinzani karibia wote hasa wakiongozwa na Zitto walivyokuwa wanasapoti hili fao kufutwa.Ilifikiwa hatua ikabidi tumpigie simu Dk.Slaa akiwa bado katibu mkuu wa CDM tukishangaa mbona hata wabunge wa CDM wanasapoti hili fao kufutwa nakumbuka Slaa alitujibu tatizo nyie wafanyakazi wakati tunadai haki huwa mnakaa mbali ila yakiwafika ndo mnaomba support yetu,akatuambia anajua kuna wabunge wake wanasapoti hilo fao kufutwa lakini watakaa waone jinsi watakavyotusaidia. Ikabidi tufanye harakati nyingine ya kwenda kuonana na dada Irene Saka na Jenister Mhagama wakati huo akiwa mwenyekiti kamati ya bunge inayojishughulisha na maswala ya jamii.
Hawa wabunge wote rangi zao sawa wala wasikudanganye chochote kwa kupiga kelele majukwaani
Kweli inaonekana sheria ilishasainiwa imebaki utekelezaji. Walitoa muda uchaguzi upite na ile pita pita ya Jaffo ilikuwa adaha.
Sasa ni utekelezaji, wafanyakzi wasiposimamia masilahi yao wategemee maumivu.
 
Hahahaha eti Lowassa na Mbowe wataisoma number!!! Ukiwa mjinga utakuwa chakula cha wanasiasa uchwara kila siku, acha Watanzania tuisome number ili kufikia 2020 akili ziwe zimerudi katika mahali pake
 
Kwa hiyo wale wanaofanya kazi sekta binafsi kwa mikataba nao watasubiri miaka 50? Hii nchi ni zaidi ya maajabu..

Mkuu na Mimi nasubiri jibu, maana naona wanatuchanganya sana sasa.
 
Kweli inaonekana sheria ilishasainiwa imebaki utekelezaji. Walitoa muda uchaguzi upite na ile pita pita ya Jaffo ilikuwa adaha.
Sasa ni utekelezaji, wafanyakzi wasiposimamia masilahi yao wategemee maumivu.
No Jaffo alikuwa anatetea kweli sema sasa hivi unajua ni Naibu Waziri hawezi kuja front tena
 
Wafanyakazi Kote nchini, amkeni sasa..Fanyeni kitu

Wafanyakazi anzisheni Group la WhatsApp ili kuunganisha nguvu nchi nzima

Admin wa group wawe wengi..akiwa mmoja watamteka kama Ulimboka au Ben Saa Nane

Mange Kimambi please, saidia hii movement

[HASHTAG]#mangekimambi[/HASHTAG]
Mkuu hilo group la WhatsApp lenye kuchukua watu 250?!!!!!!
 
No Jaffo alikuwa anatetea kweli sema sasa hivi unajua ni Naibu Waziri hawezi kuja front tena
Walicheza mchezo hili ajeda isibebwe na upizani ingawa lao moja na serikali. Vikao vya chama vilishakaa na ndio maana alipata huo unaibu waziri kwa malipo hayo.
Siasa ni mchezo mtamu sana kwa unaemnufaisha ila mchungu sana kwa unaeumia.
Tunachokiona au kusikia huku juu ni just a tip of iceberg.
 
Kwa hiyo wale wanaofanya kazi sekta binafsi kwa mikataba nao watasubiri miaka 50? Hii nchi ni zaidi ya maajabu..
Mkuu unajua tabia za fisi akitazaama unavyopiga mkono abahisi utadondoka...usiwe hivyo...unafanana na kubadget hela ya deni
 
Bima ya Afya ya nini? Kwani kuna mfanyakazi ambaye anachangia mifuko hana bima ya afya? NSSF wanao fao la bima ya afya na bado wanatoa fedha baada ya ajira kwisha.Mbadala wa fao la kujitoa ni Fao la kutokuwa na ajira tu.
 
NDIO maana sitaki ajira ya serekali ya ccm. Pesa sio zao wanashindwa kufanya Yao . Watu wanashindwa jadili kuleta maendeleo , wanaangaika na kutunga sheria za kubana watu wasilipwe ela zao pindi wanapoitaji. Kiufupi ninapofanya kazi nishakubaliana na menejimenti awanikati mafao wanakupa ela zote mkononi na wao wananipa nusu ya ile a mbayo wangenilipia. Sihitaji mifuko hii kabisa!.unafanya kazi bongo kama Dubai. Unalipwa chako chote. akuna Makato. Mtu mzima unalazimishwa kutunziwa pesa! Unadhani Huna akili ya kujiongoza. Mimi ningependekeza ifutwe hii sheria. Mtu alipwe Chake chote na ajijue na future yake. Watu akatwe bima ya afya pekee tu.
 
Miaka 60 mingi sana mpaka kuja kupokea hayo mafao unaweza kurest in pisi bila kuonja mafao yako
 
Kwa nini wanasiasa wao walipwe kila baada ya miaka mitano? si na wao wasubiri mpaka wafikishe hiyo miaka 55.
Yaaani na mi nasema wale hawawezi kutetea chochote maana haijagusa maslah yao... mxiuuuuu nimekwazika sana
 
Haki nimeishia kuwaombea dua mbaya... naomba Mungu aikubali..manyanyaso gani haya... naomba yawakute japo watoto zao labda wataelewa
 
Back
Top Bottom