Fao la kujitoa lafutwa rasmi

Fao la kujitoa lafutwa rasmi

Haya mafao kwa watu wa sector za madini ndio uwasaidia kufanya maendeleo anapotoka kampuni moja kwenda nyengine anavuta mpunga anajenga nyumba , baada ya miaka 5 anatafuta chaka jengine anavuta mpunga anahama na mfuko ananunua gari au anapata capital ya kuanzisha biashara. Kuzuia fao la kujitoa ni pigo kubwa sana kwa miners na wafanyakazi wengine wanaofanya kwa mikataba ya muda au kwenye project za muda mfupi.
Serikari itazame in 3 dimensions maamuzi yake inazipangiaje bajeti pesa ambazo sio zao ? Huu ni unyanyasaji wa hali ya juu na ukandamizaji...Bongo sio ulaya.
 
Watu walitegemea fao la kujitoa waimarishe maisha yao afu wengine waanze biashara baada ya kumaliza mikataba sasa acha tuisome namba

Ni Kweli kaka, Katika Nchi hii mitaji ya biashara ni ngumu kupata na mikopo hakuna

Mkombozi wa Mtanzania Mnyonge ilikuwa FAO LA KUJITOA

Nchi kunyimwa misaada ni kiburi cha watawala....
 
Wafanyakazi Kote nchini, amkeni sasa..Fanyeni kitu

Wafanyakazi anzisheni Group la WhatsApp ili kuunganisha nguvu nchi nzima

Admin wa group wawe wengi..akiwa mmoja watamteka kama Ulimboka au Ben Saa Nane

Mange Kimambi please, saidia hii movement

[HASHTAG]#mangekimambi[/HASHTAG]
 
Leo wana meno makali wanashindwa kufanya maamuzi ya kuwaangalia walalahoi, kesho wakiwa hawana uongozi wanaanza kulalamika kuwa wanahujumiwa na serikali,...Hovyo kabisa hawa, refer Nape na Kitwanga
 
Wabunge wamelala wanaitikia ndio! 2020 wanapewa kanga na wali wananchi wanasahau! Wanafanyakazi wananyanyasika kwa pesa yao!! Sababu maamuzi kipumbavu ya wanasiasa wamechezea pes zetu inauma sanaaa
 
Wafanyakazi Kote nchini, amkeni sasa..Fanyeni kitu

Wafanyakazi anzisheni Group la WhatsApp ili kuunganisha nguvu nchi nzima

Admin wa group wawe wengi..akiwa mmoja watamteka kama Ulimboka au Ben Saa Nane

Mange Kimambi please, saidia hii movement

[HASHTAG]#mangekimambi[/HASHTAG]
Mkuu acha basi drama, magroup ya whatsapp?
 
Leo wana meno makali wanashindwa kufanya maamuzi ya kuwaangalia walalahoi, kesho wakiwa hawana uongozi wanaanza kulalamika kuwa wanahujumiwa na serikali,...Hovyo kabisa hawa, refer Nape na Kitwanga
Ujnga wetu wenyewe..haimaanishi kuichukia ccm siwexi ichukia kwa kuwa nalala kwangu wala silali gest house.....

Watu na wanaccm wasitupotezee wakati kwamba kuiathibu ccm ni kuichukia na kutotaka iendelee kuongoza.

Huu ujibuji na ubabaishaji ndio shida. Mathalani kuna haja gani kutolipa vzr waliona clean sheet ya vyeti vyao.

Mnababaika nini na mifuko ya jamii isiyo na tija. Mnasubiri nini kudeal na vyama vya wafanyakazi kukata tuu makato ktk salary..mnasubiri nin kuchukulia hatua magari mabovu na yanayojaza abiria barabarani...mbona hampendi kumxaidia raisi
 
Huu ni upuuz sana sasa unataka mfanyakaz wa migodini asubiri had miaka 55 ndiyo achukue mafao yake huu ni wizi na ni dalili ya serikal kutaka kuibeba hii mifuko baada ya wao serikal kuponda pesa zote za kwenye mifuko ya jamii . kwa mtindo huu kuna haja gan ya kureplace fao la kujitoa kwa kuweka bima afya nazan FAO ambalo lingekuwa sahihi kwa hali hii ni kuweka tu FAO la Unemployment benefit ili mtu akiwa hana kaz basi alipwe pesa had akija kupata kaz


Kwa huu mtindo wa viongoz kujifanya manyapala nawaambia hii nchi tutakuja kutafuta ubaya . kipind hiki bila unafik wamechochea sana chuki kutoka kwa wananchi , hebu angalia huku Mara watumishi hewa(kuna waliosimamishwa wakat sio watumishi hewa) huku wanafunzi hewa , Mara wenye kukosa vigezo vya kujiunga chuo n, huku ukija kuna manyanyaso kibao wafanyabiashara na wafanyakaz wanaishi kama watumwa kwenye nchi yao , hakuna tena Uhuru wa kutoa maoni au kukosoa pale wanapokosea viongoz wa serikal, utata kwenye maamuz ya pesa zetu Leo hii mkuu wa familia anapanga mwenyewe matumiz ya pesa kwenye miradi bila kusubiri idhini ya bunge , vyama vya upinzan hawana haki ya kufanya kaz zao, michango ya misiba inaliwa , michango ya tetemeko hatujui ilipo, kutumbuliwa kwa kuoneana, haya hili la vyeti feki bila huruma watu wanatimuliwa ovyo kuna watu kwa pressure walikaribia kustaafu wanafukuzwa , matokeo yake wengine wana kufa, lakin vyeti feki hivyo mkuu kuna mkuu wake wa mkoa had Leo anamlinda

Yapo mengi sana ya kusikitisha hawa wanaofanyiwa huu ubaya taarifa zao zinasambazaa had vijijin maana huko wapo familia zao wakiona matatizo na kuambiwa ukwel juu ya huu uonezi wa serikal dhidi ya haki yao hakika ule unafuu wa kusema vijijin ni mafala unazid kuondoka , maana na wao wanakosa misaada kutoka kwa hawa waliokuwa wanawategemea


Kuna watoto wa wakulima wsmesoma ualimu had Leo ajira hawapewi na hakuna majibu ya maana juu ya hili

Kuna kukosekana kwa ajira na mbaya zaid naona maisha ni magumu kila muda


Hii na mengine watz watachoka mwisho wa siku hasira zao tutashindwa kuja kuzuia kisa ujinga wa viongoz wetu


Mungu ibarik Tanzania
 
Mimi haya mambo sielewi.

Ina maana hata wale wanaofanya kazi kwenye miradi pindi miradi inapofikia ukomo zile pesa zao kule NSSF hawazipati au vipi?

Dodoma. Serikali imesema fao la kujitoa halipo,badala yake imekuja na fao la bima ya afya.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bungena Vijana), Jenista Mhagama alisema hayo bungeni
jana kuwa suala la fao la kujitoa haliwezekani kwa sasa na badala yake imeanzisha mchakato wa fao la
bima ya afya ambalo itakuwa ni mbadala wa fao la kujitoa.

“Katiba ya Tanzania katika kifungu cha 11
kinaeleza namna ambavyo mifuko hiyo
(akimaanisha ya hifadhi ya jamii) inapaswa kuwa,
lakini hata juzi Mheshimiwa Rais aliagiza
utengenezwe utaratibu katika bima ya mfuko na
itakuwa ni mbadala wa watu wasiokuwa na ajira,”
alisema Mhagama.
Mapema bungeni jana, swali kuhusu malipo ya mafao kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii liliwaibua wabunge wengi waliotaka kuuliza maswali ya nyongeza licha ya mawaziri kutoa majibu.

Akijibu swali la wafanyakazi waliopatikana na vyeti feki kama wanaweza kulipwa mafao yao Waziri wa Utumishi Angella Kairuki ali hatuwezi
kutoa taarifa kwa sasa kwani bado
wanashughulikia jambo hilo ili kuona namna bora ya kufanya na wakifikia hatua nzuri watatoa majibu ya kuaminika na kuomba wapewe muda kwa sasa
Mapema mbunge wa Viti Maalumu,
Amina Mollel alitaka kujua kwa nini wafanyakazi waliopatikana na vyeti feki wasilipwe mafao yao.

Naibu wa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu(Sera, Uratibu na Bunge), Anthony Mavunde alisema kuanzishwa kwa mifuko ya jamii kumefikia hatua mbalimbali ikiwamo kukamilika kwa tathimini ya mifuko ya hifadhi ya jamii
(actuarial evaluation) ambayo imetoa mapendekezo kuhusu namna bora na mambo ya kuzingatia katika kuunganisha mifuko ya hifadhi ya jamii.

“Mpaka sasa Serikali haijafanya uamuzi rasmi wa idadi ya mifuko itakayobaki baada ya kulinganisha mifuko iliyopo hivi sasa,” alisema Mavunde.


Chanzo..Mwananchi
 
Twafaaaaaaaaa Nisamehe Jay key
Hii mbona ilianzia kwa JK na mtetezi mkubwa wa hili fao kufutwa ni Zito Kabwe, Tundu Lisu, TUCTA, wafanyakazi wa mashirika ya Uma, wabunge walionyesha kupinga hili fao kufutwa ni Mnyika na Jaffo peke yao.
Ukihudhulia mikutano ya SSRA utajua jinsi vyama vya wafanyakazi wanavyosapoti hili fao lifutwe sema wakitoka nje wanapiga siasa, it has nothing to do na Magufuli maana sheria ilipitishwa bunge la JK na wafanyakazi hasa Mining walipokuja juu wabunge wakashtuka lakini NSSF wakisaidiwa na Zito Kabwe bungeni akashawishi kamati ya uongozi ya bunge ikutane kujadili ndo wakaamua sheria isibadilishwe lakini wafanyakazi wapewe mda wakati inaangaliwa jinsi ya kuhandle wale watakao wanafukuzwa kazi.
Muulize Sungusia au hata Mnyika jinsi wabunge wa upinzani karibia wote hasa wakiongozwa na Zitto walivyokuwa wanasapoti hili fao kufutwa.Ilifikiwa hatua ikabidi tumpigie simu Dk.Slaa akiwa bado katibu mkuu wa CDM tukishangaa mbona hata wabunge wa CDM wanasapoti hili fao kufutwa nakumbuka Slaa alitujibu tatizo nyie wafanyakazi wakati tunadai haki huwa mnakaa mbali ila yakiwafika ndo mnaomba support yetu,akatuambia anajua kuna wabunge wake wanasapoti hilo fao kufutwa lakini watakaa waone jinsi watakavyotusaidia. Ikabidi tufanye harakati nyingine ya kwenda kuonana na dada Irene Saka na Jenister Mhagama wakati huo akiwa mwenyekiti kamati ya bunge inayojishughulisha na maswala ya jamii.
Hawa wabunge wote rangi zao sawa wala wasikudanganye chochote kwa kupiga kelele majukwaani
 
Back
Top Bottom