Familia zingine kama zimelaaniwa jamani

Familia zingine kama zimelaaniwa jamani

Ukizaliwa katika familia ambayo unasema 'kwa bab tuko wanne sijui,na kwa mama tuko watatu'
ujue kazi kubwa ipo hapo

Majority ya familia hizo huwa na maugomvi na migogoro isiyokwisha

Ni bahati mno ukijikuta mmezaliwa watoto wote baba mmoja na mma mmoja

yanayokukuta wewe ni madogo kuna watu yamewakuta makubwa kuliko yako
kuna kushikana uchawi na watoto wa baba mmoja au mmama moja kutozungumza
wala kusalimiana
Hiyo pia naona kawaida maana kuna familia nyingine mmezaliwa gumbo moja lakini kulogana na kuchukiana ni kitu chakawaida sasa bora Muwe mama mbalimbali hata utasema ndio sababu, familia nyingi hazijaka vizuri, kama ukikuta familia yenu uko smart mshukuru Mungu
 
Jipe moyo muombe Mungu huku ukifanya juhudi za kutafuta utayashinda majaribu.Ni wengi tumepitia ktk mitandao yenye magumu pengine makubwa kuliko hata haya ila mungu akatutoa salama.Pole mdogo wangu yana mwisho haya.
 
Ongea na hao walimu wako chuo wakupe nafasi umalize mitihani then wakishikilie cheti chako hadi uweze kumaliza deni ndo upewe hiko cheti.
Haina maana kusoma miaka mitatu vizuri halafu ushindwe sehemu ya mwisho kabisa,.
 
Haya mambo huwa mara nyingi yanasababishwa na wazazi wa kike, kwa sababu baba huwa anapata taarifa za watoto kutoka kwa mama yao na kutekeleza kupitia mama yao, sasa mama unaanza kujinadi kwa watoto eti wewe ndo unawahangaikia baba yenu hana msaada wowote. Basi mzee akija kungundua huwa anakauka kimya wala hazungumzi lolote hapo ndo watoto huwa yanawafika shingoni.
 
Mitihani: Omba uje ufanye special exams kama watakukatalia kufanya. Hii itakupatia enough time ya kutafta ada.
 
Ndugu...kuna life struggles ziaid yako, usione watu wanatembea barabarani lakini wamebeba mengi kwenye vifua vyao. Wewe shukuru shule umeiona na mpaka uko chuoni. Huyo baba hakuwa responsible toka mwanzo kwanini sasa utegemee kuwa atakusaidia.

Fanya hivi, assume he's dead, utaishi maisha ya stressless. Usifanye juhudi ya mamako ya kukufikisha hapo ilipo ipoteee, haya ni mapito tu ya kidunia.

cc kanana23
 
Last edited by a moderator:
Me nilidhani huna wazazi,kumbe wapo?kwanza we ni me au ke na uko chuo gani?
 
Pole, na amini wakiume, hebu komaa ufikie katika level ya uwanaume...
 
ushaur wako, unajua ni ngum sana kujua anapitia nini hasa kama umepata malezi ya wazazi wote wawili. ko lets have a little compassion for mkuu apo juu

Ndio maana nikauliza anataka nn exactly ?? Cz thread yake design ilikua haijakaa vizuri. Amei update

Mitihani tumeumbiwa binadam, hasa mtoto wa kiume. Alipofikia hata hapo chuo kikuu amshukuru sana Mungu.

Huo ujinga anaotaka kufanya sijui kulipiza kisasi kwa mzee wake ndio atajizolea nuksi tu na kupoteza baraka zote. Amuombe Mungu kisha apigane kiume tu. Lazma mtu uelewe wakati mwingine u gotta pursue ur path to ur dream on ur own.
 
Komaa ww mtoto wa kiume yaani umetoka huko kooooote uje kushindwa hapo mwishoni.... Huyo mdingi wee mpotezee atakuja kula jeuri yake we cha msingi umiza kichwa ushakua ujue angalia wapi utavuta mkwanja uclear deni uendelee na life..!

Watu wana miaka na miaka pesa ya mdingi hawajawahi hata kuiona sembuse wewe jikaze!
 
Habari Jf,

Naandika hapa mpaka nasikia kufa.

Nimezaliwa katika familia ya watoto watatu kwa mama yangu ingawa baba ana familia nyingine so my mom ni kama mke mdogo.

Toka nakua familia yangu haikua katika maelewano mazuri ( matatizo ya mitara).

Baba yangu alikua mtu anayejiweza (ameshastaafu).

Alikua Muhandisi wa mkoa enzi hizo kwa hiyo tulikua tunaishi kawaida mama yangu pia ni mtumishi wa Serikali.

Lakini katika makuzi yetu baba yetu hakua responsible kabisa kuhusu sisi.

Mama yetu yeye ndo alijua kula yeti,vaa yetu,na elimu pia alijitahid kadri ya uwezo wake tusome mpaka tukafika chuo.

Dada yetu mkubwa kamaliza chuo mimi ndo namalizia mwaka wa tatu.

Baba yangu toka nianze kusoma hajawai kunilipia even a single sent japo uwezo alikua nao na anao.

Kwasababu amepata mafao yake (story ni ndefu nikiandika maisha na vimbwanga vya familia yetu ni kitabu kabisa).

To cut the story hivi mimi nipo mwaka wa mwisho chuoni najiandaa na University exams.

Jumatatu sasa katika kuclear nikajikuta nadaiwa basi nikampigia mama yangu simu kumuelezea hali halisi kasema hana pesa.

Basi katika kuhangaika ikabidi nimpigie baba yangu yani kanikatalia katakata.

Nimejikuta nalia sijui cha kufanya mpaka najiuliza kama tulizaliwa kimakosa au vip.

Eeeh mungu nisaidie uniondolee roho ya kisasi dhidi ya mzee wangu.

NB: Nashindwa cha kufanya kuhusu huyu mzazi wangu.

Kwani baba yako ni mwanachama wa chama gani cha siasa ila itakuwa ni #ccm ndozao kuwatelekeza watoto
 
Mama yenu zliwajengea chuki dhidi ya baba yenu

Mtakura jeuri yenu kenge nyie!
 
Ndugu Pole sana nakuomba usikate tamaa kwani hayo nimajaribu na pia jioni upokwenye mafunzo ya maisha.Baada ya dhiki huja faraja.
 
Pole kanana23,hayo ni majaribu
sijui kama unamwamini Mungu au la!
lakini nataka nikutie moyo kwamba Mungu aliyekuwezesha
kufika hapo hatakuacha,ukiangalia viunzi ulivyovuka mpaka hapo
ni vingi hhivyo hicho nacho kihesabu ni kimojawapo,kisikukatishe tamaa.

Hakuna alnayezaliwa kwa bahati mbaya,japo mambo ya mitara
yana matatizo yake,lakini watoto hakuna anayechagua azaliwe wapi
wanajikuta wamezaliwa,iwe ni ndoa ya mkeka,mitara n.k
cha msingi ni kumwomba Mungu akusaidie uvuke.
na ukiishavuka hutakubali kamwe kuingilia ndoa ya mwenzio
kwani utakuwa umeona ubaya wa mitara.
Jipe moyo utashinda
 
Last edited by a moderator:
Tatizo hapo naliona ni huyo mama yenu, kawalea na kuwafundisha kumchukia baba yenu. Kawakaririsha kuwa baba yenu ni mbaya na ndio maana hata story yako yote inaonyesha kumchukia baba sana. Aidha inaonyesha wazi kuwa haukuwa na muda na baba yako hadi ulipoona umepata tatizo ambalo kila uliyemtegemea kashindwa. Ukipoona umekwama ndio baba akawa option ya mwisho tena unamtafuta kwa kumpigia simu!!!!. Siku zote humtafuti leo unampigia simu!!! tena kumuelezea matatizo na jinsi ulivyokwama kulipa deni/ada. Hili ni tatizo kubwa pale akina mama wanapokosana na kuachana na waume zao, huwalea watoto kwa kuwafundisha kuwa baba yao alikuwa mbaya sana na hakuchangia malezi yao. Unajua ulivyozaliwa na kukua hadi wanaachana chanzo kilikuwa nn? Acheni kuingilia ugomvi wa wazazi, wao ndio wanajua chanzo cha ugomvi na kuachana kwao. Watoto hamuhusiki na hilo. Mtafuteni baba yenu (siyo kwa simu), mkae na kujenga urafiki nae. Laana inaweza kuwaangukia kama mtaendelea kufuata maneno ya mama na kumchukia baba yenu kwa sababu ambazo hamzijui.
 
Pole sana, na hapo ukifanikiwa mzee atakavojisogeza sasa mmh
 
Back
Top Bottom