Faini ya Tsh.1 kesi ya Mengi Vs Manji, je, ni dharau na kupoteza muda wa mahakama?

Status
Not open for further replies.

M-pesa

JF-Expert Member
Sep 4, 2011
602
150
Nimekuwa nikitafakari sana hii kesi ya bw. Reginald Mengi Vs Yusuph Manji.
Kwa mtazamo wangu naona ni dharau pamoja na kipotezea mahakama muda. Kuna kesi ngapi zilizorundikana mahakamani huku watu wakiteseka kusubiri haki itendeke? Lakini hawa mabwana kutokana na kiburi cha pesa wameamua kunyima haki wananchi wengine kwa kuendeleza kesi ya kipumbavu. Wenye kujua sheria mnasemaje?
 
Lokissa

JF-Expert Member
Nov 20, 2010
7,442
2,466
sio dharau lengo la kila mmoja ni kulinda haki na muonekano wake ktk jamii
(to maintain status quo) Sii kweli kuwa kesi hiyo inachelewesha kesi zingine
kwani sheria ya mwenendo madai inawaruhusu kufanya hivo.
 
M-pesa

JF-Expert Member
Sep 4, 2011
602
150
Mods naomba munisaidie ku edit title, ianze na neno Fidia ya Tsh.1 Kesi ya Mengi Vs Manji, je, si dharau pamoja na kupoteza muda wa mahakama?

Asanteni.
 
Mzee

JF-Expert Member
Feb 2, 2011
13,536
5,642
Hiyo ni dharau kubwa sana.
Mahakimu wanatumia muda na maliasili za taifa kutatua kesi ya Tsh1????.
 
M-pesa

JF-Expert Member
Sep 4, 2011
602
150
Ok, kumbe uzito wa kesi hauendani na kiasi cha fidia upande mmoja unachoomba!

sio dharau lengo la kila mmoja ni kulinda haki na muonekano wake ktk jamii
(to maintain status quo) Sii kweli kuwa kesi hiyo inachelewesha kesi zingine
kwani sheria ya mwenendo madai inawaruhusu kufanya hivo.
 
M-pesa

JF-Expert Member
Sep 4, 2011
602
150
Mkuu hata mimi naichukulia hii kesi kwamba ni ya dharau! Hapa sheria ndo huwa inaacha maswali mengi.

Hiyo ni dharau kubwa sana.
Mahakimu wanatumia muda na maliasili za taifa kutatua kesi ya Tsh1????.
 
remta

New Member
Oct 9, 2011
1
0
kwa mtazamo wangu sio dharau wala kupotezeana muda ni technicali za kisheria ndio maana mzee mengi anahudhuria sana mahakamani kila kesi inapotajwa. anafahamu akishindwa na manji. ataamriwa kulipa gharama za kesi kwa manji. na kwa uelewa wangu zitakuwa fedha nyingi sana .na hata mzee Mengi akishinda manji naye ataamriwa alipe gharama za kesi ambazo nazo zitakuwa nyingi. hivyo shilingi 1 ni ujanja tu kuna zaidi ya hicho kiasi.
 
M-pesa

JF-Expert Member
Sep 4, 2011
602
150
Mkuu asante kwa kunifungua macho. Naomba nieleweshe jambo lingine zaidi, Je, mbali na hiyo Tsh1. Unadhani ni kiasi gani upande mmoja waweza shurutishwa ulipe endapo utashindwa?

kwa mtazamo wangu sio dharau wala kupotezeana muda ni technicali za kisheria ndio maana mzee mengi anahudhuria sana mahakamani kila kesi inapotajwa. anafahamu akishindwa na manji. ataamriwa kulipa gharama za kesi kwa manji. na kwa uelewa wangu zitakuwa fedha nyingi sana .na hata mzee Mengi akishinda manji naye ataamriwa alipe gharama za kesi ambazo nazo zitakuwa nyingi. hivyo shilingi 1 ni ujanja tu kuna zaidi ya hicho kiasi.
 
Taso

JF-Expert Member
Jun 12, 2010
2,341
2,011
Majaji wa mahakama za common law, kama hapa kwetu, wanaruhusiwa na sheria za bunge kujitungia kanuni za kuratibu mchakato mzima wa kuanzisha na kuendesha kesi, rules of civil procedure. Wangeweza kujiwekea taratibu za kuzuia kesi hizi za shilingi moja moja.

Katika nchi nyingine kuna "jurisdictional amount" ambayo ni kiwango cha chini kabisa ambacho ni lazima ukidai kabla mahakama haijajisumbua kukusikilizeni.
 
Noti mpya tz

JF-Expert Member
Mar 23, 2011
974
243
Mahakama ni sehem ambayo kila mtu anao uhuru wa kupeleka malalamiko yako kama anaona kuna sehem hajatendewa haki na anao uhuru wa kufungua kesi kutokana na anavyojisikia so kwa haya mabwana hasa Manji ambae ni mshitaki anao uhuru wa kudai hiyo TSH 1 na alikuwa hata sahihi kudai Mengi akiri kusema maneno ya kumkashifu bila fidia yyte.
 
M-pesa

JF-Expert Member
Sep 4, 2011
602
150
Nakubaliana nawe mkuu, kulitakiwa kuwe na minimum amount ambayo ni reasonable. Lakini Tsh1 inaleta tafsiri ya kwamba Manji anamuambia Mengi " Mimi sina shida na Pesa yako....ninataka tu kusafishwa"

Majaji wa mahakama za common law, kama hapa kwetu, wanaruhusiwa na sheria za bunge kujitungia kanuni za kuratibu mchakato mzima wa kuanzisha na kuendesha kesi, rules of civil procedure. Wangeweza kujiwekea taratibu za kuzuia kesi hizi za shilingi moja moja.

Katika nchi nyingine kuna "jurisdictional amount" ambayo ni kiwango cha chini kabisa ambacho ni lazima ukidai kabla mahakama haijajisumbua kukusikilizeni.
 
M-pesa

JF-Expert Member
Sep 4, 2011
602
150
Lakini mkuu inakuwaje kesi za uchaguzi ...mamilioni ya pesa yanatakiwa kutangulizwa mahakamani, afu kesi inakuwa inakwenda kwa mwendo wa konokono?

Mahakama ni sehem ambayo kila mtu anao uhuru wa kupeleka malalamiko yako kama anaona kuna sehem hajatendewa haki na anao uhuru wa kufungua kesi kutokana na anavyojisikia so kwa haya mabwana hasa Manji ambae ni mshitaki anao uhuru wa kudai hiyo TSH 1 na alikuwa hata sahihi kudai Mengi akiri kusema maneno ya kumkashifu bila fidia yyte.
 
Pota

JF-Expert Member
Apr 8, 2011
2,018
705
Nimekuwa nikitafakari sana hii kesi ya bw. Reginald Mengi Vs Yusuph Manji.
Kwa mtazamo wangu naona ni dharau pamoja na kipotezea mahakama muda. Kuna kesi ngapi zilizorundikana mahakamani huku watu wakiteseka kusubiri haki itendeke? Lakini hawa mabwana kutokana na kiburi cha pesa wameamua kunyima haki wananchi wengine kwa kuendeleza kesi ya kipumbavu. Wenye kujua sheria mnasemaje?
M-pesa mi nakuunga mkono, pia wewe kutuletea hii thread humu ni kuidharau jf na kutupotezea muda
 
Status
Not open for further replies.

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

0 Reactions
Reply
Top Bottom