Membe Vs Musiba: Huwezi Kuomba Msamaha Baada ya Hukumu, Msamaha unaomba Wakati wa kesi au Kabla ya Kesi

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
21,340
51,891
Kwema Wakuu!

Membe Vs Musiba; Huwezi Kuomba Msamaha Baada ya Hukumu, Msamaha unaomba Wakati wa kesi au Kabla ya Kesi.

Kuna Watu bhana wanafurahisha Sana. Hivi uliona wapi mtu akapewa Msamaha pasipo ya yeye kuomba Msamaha? Wapi? Na lini? Uliona wapi mtu anasamehewa ikiwa alipewa muda wa kutosha, nafasi za kutosha za kuomba Msamaha lakini Kwa Ujeuri, ukaidi, dharau na Kiburi akakataa? Uliona au kusikia wapi?

Kusamehe ni Jambo zuri la hiyari, hakuna sheria yoyote duniani, Kuzimu na akhera inayomlazimisha MTU kusamehe. Kwa sababu kikawaida Msamaha ni Neema, na neema ni kinyume na HAKI. Kuomba Msamaha unapokosea ni Jambo Zuri, na unaomba Msamaha sio ili usipewe adhabu Bali kuonyesha kujuta, na unataka kufanya Amani na MTU.

Msamaha pia unahusisha kulipia Gharama Fulani kama sehemu ya fidia ili kuweka Mambo Sawa na uliyemkosea.

Msamaha ni kitu cha thamani Kwa Watu wanaotafuta Amani na Furaha. Msamaha hautolewi na kupewa Watu wapumbavu ambao huweza kuutumia vibaya. Msamaha unatolewa Kwa Watu waliojifunza kuwa ni kweli wamefanya Makosa na wanajutia Makosa Yao.

Huwezi omba Msamaha siku ya Hukumu, na kamwe haitowezekana kusamehewa siku ya Hukumu. Ni mtu mwenye Jeuri, kiburi, dharau, na muovu anayeweza kuomba Msamaha siku ya Hukumu yaani Baada ya kuhukumiwa ilhali alipewa nafasi za kutosha ili kuweka Mambo Sawa.

Ni Watu wanafiki pekee wanaoweza kuomba Msamaha Kwa namna hiyo. Halikadhalika ni Watu wanafiki pekee wanaoweza kuwa upande wa Watu wa namna hiyo. Msamaha hauwafai Watu wanafiki, kwani Wanafiki wanatabia ya Kisasi na usaliti. Kwao Msamaha huitumia kama mbinu ya kishetani kujisalimisha(Jambo ambalo wanaona aibu na hawataki litokee).

Vipo visa na reference nyingi zinazoeleza kile nikisemacho, mtu ukishafanya madhara Fulani kuna hatua za kuchukua, huwezi fanya kitu Makusudi alafu Kwa kiburi na Jeuri uliyemkosea anakusihi uachane na tabia yako Mbaya tena umuombe Msamaha lakini unakuwa mkaidi, yakikupata ndio unaona ndio Wakati Sahihi Kwa vile umeshindwa. Wewe ni Shetani na watakaokutetea pia ni vibaraka wa Shetani.

Ni vizuri kama Watu waungwana tukikosea tuombe Msamaha Kwa Wakati, na jukumu la kusamehewa litabaki Kwa tuliowakosea, na sio Haki yetu kusamehewa, itategemeana na uliyemkosea.

Narudia hakuna sheria popote duniani, Mbinguni, na akhera inayoamrisha Watu au kiumbe kitoa Msamaha. Isipokuwa Msamaha ni hiyari ya MTU. Kitu kikiwa hiyari sio amri wala sheria. Labda sheria za Kinafiki.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
 
Musiba alikuwa na kiburi sana. Kumsamehe Musiba itakuwa ni kuutukuza ujinga na uzandiki. Membe baba shikilia hapo hapo!
na zaidi...alionywa akashupaza shingo. Hao waliokuwa wanamtia kiburi wamsaidie kulipa
 
Hicho ndicho wanatakiwa kukifanya hao viongozi wa Dini.
Tatizo theolojia ya msamaha watu wengi hawaijui, huwa wanaiabuse sana. Ingekuwa ni ajali msiba alimgonga membe sawa. Wanasahau kuwa hata kabla ya kwenda mahakamani, Msiba aliambiwa aombe msamaha na afute kauli zake, lakini badala yake akaongeza kumtusi mzee membe, makamba, kinana na wengine wengi
 
Tatizo theolojia ya msamaha watu wengi hawaijui, huwa wanaiabuse sana. Ingekuwa ni ajali msiba alimgonga membe sawa. Wanasahau kuwa hata kabla ya kwenda mahakamani, msiba aliambiwa aombe msamaha na afute kauli zake, lakini badala yake akaongeza matusi

Ndio maana wengi Wanawaona viongozi wa dini kama Wanafiki. Ni kama hawajui concept ya Msamaha
 
Aliwatusi au aliwaambia kile walichukuwa wamepanga kukifanya? Sasa ilitakiwa nani ampeleke mwenzake mahakamani? Mboja dunia iko kinyumenyume na watu wanajifanya wamelewa
 
Mungu mwenyewe mwingi wa rehema, mwenye kusamehe, asiyezikumbuka dhambi zetu tena baada ya kusamehe hajawahi kusamehe hadi aombwe msamaha! Sembuse mwanadamu mwenye dhambi? Nakubaliana na wewe!
 
Wakati MEMBE akienda mahakama I hao viongozi wa dini walikuwa wapi? Au walijua hatoshinda kesi?? Alipotukanwa hawakujali,alipohatarishiwa usalama kwakutuhumiwa kwenda Zimbabwe na Kongo kutafuta wasaidizi walikaa kimya,alipotuhumiwa kuficha mapesa ndani kwake angevamiwa na majambazi walikaa kimya, Aalivyopoteza muda na fedha mahakamani walikaa kimya Leo wanakosa hekima ndiyo wanaingilia kumuombea mtu mjinga eti asamehewe kisa naye atapoteza PESA!!! Saa nyingine viongozi wa makanisa wanatupush tutamke maneno mabaya sana kwao sijui KWANI wanataka shetani achekelee???? Kimya nayo ni hekima hatakama huna unapoongea....
Membe please Wacha shetani aanguke na haki itimilikekiukamilifu hili jambo siyo lako pekee tuko wengi ambapo tumewahi kutusiwa isivyo haki!!!
Hizo mali atazolipa utawajengea hata WAZEE kule Tabora na kwinginepo wanaokosa hata vyoo kwenye Kambi za wazee...
 
Back
Top Bottom