Faidika na darasa la FaizaFoxy; Uliza chochote utajibiwa

Taaluma yako ni ipi?


Kasome post namba 43.

Licha ya hiyo, kuna kozi nyingi sana na seminars nyingi sana za taaluma mbali mbali nimepitia sehemu nyingi duniani. Lakini katika yote hayo hakuna taaluma niliyoipata zaidi na iliyonifunguwa ubongo na macho kama Qur'an, kusafiri na kujisomea mwenyewe kila nnapopata nafasi.
 
General Knowledge.

Naam, kama kichwa cha habari kinavyojieleza.

Natumia fursa hii ya mtandao adhyim wa JF kuwapa fursa wanamtandao wote wapate fursa ya kuuliza kuhusu mada au jambo lolote ambalo unataka upatiwe majibu.

Si majibu yote yatatoka kwangu binafsi, bali nitajitahidi iwezekenavyo kukupatia majibu murwa na yanayolingana na swali lako na ambapo sina jibu itakuwa fursa kwa wengine kutoa majibu.

Hapa ni kwa ajili ya kuelimishana na kujuzana bila kikomo, iwe swali lolote liwalo.

Tanabahi: Ukiuliza utumbo ntakujibu utumbo.
Aslam aleikum muislam mwenzangu na ndugu yangu kiimani.Ni na maswali kama matatu hivi la kwanza wewe ni mfuasi wa ccm chama tawala moja ya ahadi zenu nikupiga vita rushwa swali zile milioni kumi zilitoka wapi na wabunge walipewa kwa kwakazi gani? Swali la pili muheshimu anatumia nguvu nyingi sana kukandamiza Uhuru wa kukosoa kwa maana ya kutoa maoni,kupiga marufuku mikutano ya hathara ambayo inatusaidia sisi wanachi wakawaida kujua mapungufu ya serikali pamoja na kutoonyesha bunge live swali ni ya mh kufanya yote hayo kwa nguvu kubwa paka kutoa milioni kumi kwa wabunge ni IPI? Tatu mlituaidu ajira mh kasema uwakiki ulikuwa miezi miwili imesha imepita mda lakini paka Leo ajira hamna mikopo ya wanavyuo kizungu mkuti nini tatizo linalokwamisha?
 
Je Trump ndio kiboko chenu nyie magaidi wa kiislam?


Kuuhusisha Uislam na ugaidi ni kutoutendea haki, nimesoma katika tovuti moja ya tafiti na imeandika kuwa zaidi ya 90% ya ugaidi uliofanywa America haukufanywa na Waislam, jisomee:

Non-Muslims Carried Out More than 90% of All Terrorist Attacks in America

Terrorism Is a Real Threat … But the Threat to the U.S. from Muslim Terrorists Has Been Exaggerated

An FBI report shows that only a small percentage of terrorist attacks carried out on U.S. soil between 1980 and 2005 were perpetrated by Muslims.

Princeton University’s Loon Watch compiled the following chart from the FBI’s data:



piechart2.jpg
Terrorist Attacks on U.S. Soil by Group, From 1980 to 2005, According to FBI Database



According to this data, there were more Jewish acts of terrorism within the United States than Islamic (7% vs 6%). These radical Jews committed acts of terrorism in the name of their religion. These were not terrorists who happened to be Jews; rather, they were extremist Jews who committed acts of terrorism based on their religious passions, just like Al-Qaeda and company.


Soma zaidi: http://www.globalresearch.ca/non-mu...0-of-all-terrorist-attacks-in-america/5333619






Sasa jibu, ni nani gaidi kwa hayo?
 
A,aleukoum,nauliza mama,nilioa,baadae mke akadai talaka,nikamwambia afuate utaratibu,yaani aikomboe talak,nikampa,sasa anadai turudiane,alishawishiwa tu,kidini inawezekana kurudiana?
 
Je? kweli wewe ni wa jinsi ya Ke?
Una kiwango gani cha Elimu?
Kuna nyakati huwa unaaongelea mambo ya zamani miaka ya 50 -60 ulkuwepo? Au ni simuliz??
NB Unafkir nini kifanyike kuboresha Elimu? Zote za kisekula na kidini


  • Ni kweli.
  • kasome post namba 43.
  • Nilikuwepo.

Ningependelea sana kuona elimu inafundishwa ili watu waelewe, wenye uelewa wa haraka wasonge mbele na wasio na uelewa wa haraka wasiachwe bali waeleweshwe mpaka waelewe.

Mwalimu awe na darasa lake kama la historia, hesabati na mengineyo na wanafunzi waende kusoma kwa wakati wao kwa uelewa wao, badala ya sasa mwalimu anawafata wanafunzi mpaka 150 katika darasa moja wenye viwango tofauti vya uelewa.
 
ABUBAKAR NI NANI KATIKA UISLAM?

Abubakar wapo wengi, lakini kama unamaanisha Abubakar Abdallah Bin Quhafah As-Siddiq, huyu alikuwa ni swahaba na baba mkwe wa Mtume Muhammad Salla Allahu Alayhi Wasalaam kwa Bi Aisha na pia alikuwa Muislam wa kwanza kutangaza wazi Uislam wake wakati wa Mtume nje ya familia ya Mtume.

Licha ya hayo, pia alikuwa ni mshauri muaminifu wa Mtume Muhammad Salla Allahu Alayhi Wasalaam na kaja kuwa kiongozi mkuu (khalifa) wa Waislam wa kwanza baada ya Mtume.
 
Back
Top Bottom