Faidika na darasa la FaizaFoxy; Uliza chochote utajibiwa

Kwa nn una chuki na watu wenye majina yanayofungamanishwa na dini ya kikristo?
Hata wafanye jema vipi,huwatambui

Si kweli. Sina sababu ya kumchukia mtu kwa jina lake au dini yake au kabila yake au kwa chochote kile.

Mimi ni Muislam na Uislam unanifundisha:

Qur'an 49:13.
Enyi watu! Hakika Sisi tumekuumbeni kutokana na mwanamume na mwanamke. Na tumekujaalieni kuwa ni mataifa na makabila ili mjuane. Hakika aliye mtukufu zaidi kati yenu kwa Mwenyezi Mungu ni huyo aliye mchamngu zaidi katika nyinyi. Hakika Mwenyezi Mungu niMwenye kujua, Mwenye khabari.
 
Kwanini una chuki na Joyce Ndalichako?

Sina chuki na Joyce Ndalichako bali nnauhakika si kiongozi mzuri, alivurunda kama mkuu wa NECTA mpaka baadhi ya Waislam wa Tanzania wakaandamana kumkataa. Jikumbushe:

DSC08684.jpg
 
Haya madai kwamba Mwislamu akifa katika kuupigania Uislamu (mf. Kwa kujitoa mhanga maisha yake) anakwenda akhera na anakabidhiwa mabikra 72 wasiomaliza ubikra na kuwafaidi milele na milele ni ya kweli na yana misingi yo yote katika Uislamu au ni porojo tu za makundi haya ya kigaidi yanayotumia Uislamu kama mwamvuli wake? Madai haya yamo katika Quran tukufu au katika hadithi za Mtume?
 
Back
Top Bottom