Faida na hasara ya vitanda vya chuma

Faida na hasara ya vitanda vya chuma

kitanda kama icho cha 5kwa6 napata kwa shingap?
...
Screenshot_20200805-035520~2.jpg
 
Wadau naandika hapa kutaka kujua changamoto ya vitanda vya chuma (faida au hasara zake) maana hiki kitanda changu cha mbao kina changamoto sana kila mara kinabonyea katikati.

Nabadili chaga baada ya muda kinarudi hivyo hivyo kiasi kwamba imekua kero kubwa na imenisababishia maumivu ya mgongo sasa nataka nibadili style ya kitanda je kuna mwenye uzoefu navyo anijuze tafadhari?
...
Screenshot_20200805-034842~2.jpg
 
Mkuu sitakushauri chochote mpaka utupie kapicha ka wewe na huyo shemej mkiwa mmekaa hata pembeni ya hicho kitanda
 
Faida
*Havishambuliwi na wadudu waaribifu mf: mchwa
*kinapangika vizuri ktk gari wakati wa kuhama
*kinakupa chaguzi ya rangi upendayo
*hii ni moja ya sex tool makini kikifungwa kiumakini
*KUNGUNI hatagi ktk chuma. kunguni hawapendelei vitanda hivi na kama watakuwepo ni simple kuwateketeza kwani watakaa ktk godoro tu.
*hudumu kwa muda mrefu ukilinganisha na mbao kwa gharama ya kitanda husika

HASARA
*Ku conduct umeme kama kitakuwa na waya ziko uchi na kugusa sehemu ya kitanda
* kushika kutu. Hii ni kwa wale wanaokaa nyumba zinazovuja. Au waliotegesha vitanda dirishani hasa msimu wa mvua,
*kinadumu sana , hakiharibiki.



Wadau ongezeeni.
Faida nyingine ya kitanda cha chuma, ni kwamba kinaepusha matumizi ya mbao ambayo kimsingi ni miti ambapo hupelekea utunzaji wa mazingira na kuepukana na janga la jangwa. Ni muda mrefu sasa vitanda vyangu mimi ni vya chuma na ninavifurahia kwa kweli.
 
Cha chuma faida hakiliwi na mchwa,kwichi kwichi haipo, kina space nzuri kudeki unadeki hadi mvunguni,hakuna sehemu ya kijificha kunguni kiviilee. Na ikatokea nyumba umewaka moto wewe unapaka rangi tuu na chaga nyingine kitand kipo.
Hasara;
Cha chuma ni kizito wakati wa kudeki ukisogeza vibaya kinakwangua tylies yako kiko juu juu mtoto akiteleza anavunjika shingo.hasara nyingine wakati wa kugegeda hakina sehemu ya kupachika vidole ili uweke lock ya miguu ili uipige vizuri.
Ni hayo tuu kwa leo.
Hahahahahah
kuweka "lock" ya vidole
 
Nimekuwa muumini wa vitanda vya mbao sana. Vya chuma nilikuwa sivipendi kabisa. Siku moja nililala lodge moja huko Arusha nikakutana na kitanda cha Chuma nikaipenda sana. Nukapiga picha.
Baada ya hapo nikaja kutengeneza kitanda kama hicho. Ajabu siku hizi nikiamka napata matatizo ya mgongo sana na nikiamka nakuwa na uchovu wa hali ya juu sana.
Jana nikaenda kwa fundi wa kitanda cha mbao ili nichonge kingine kwakuwa kile cha awali sasa wanalalia wengine. Bila kutoa hoja yangu fundi akaniuliza unatumia kitanda gani nikamwambia cha chuma. Akaniambia kitanda cha chuma siyo kizuri kwakuwa kinasababisha uamke asubuhi ukiwa umechoka sana na hii tumewahi kuambiwa inatokana na madini yake. Akaniambia yeye pale alipo aliisha badilishia wateja wake kutoka kitanda cha chuma kwenda mbao zaidi ya wateja 10.
Sasa huenda nami ndio kinachonitesa.
 
Sijuu hasara wala faida, ila sijawahi kuipenda chuma na hasa hayo ma square pipe furnitures. Mbao ni nambari uno.
Kitanda Cha chuma kizuri sio hayo ma square pipe ya madirisha wanayotumia.
Kitanda kizuri ni chuma round nenda maduka ya ujenzi kanunue mwenyewe na chuma za pembeni ni pana Kama vile vitanda vya zamani vya Jeshi,vinafungwa kwa nati.
Nilibahatika aisee sijawahi kulaumu
 
Weka ubao ila nao uwekwe miguu.

Una kilo ngapi? Mkeo jee?
Godoro lako nchi ngapi?
Huyu atakuwa anatumia zile godoro feki ambazo baada ya mwezi zinabonyea kati na kutengeneza shapa ya mtumbwi. Sasa akilala yeye na wife, wote wanakutana kati, hivyo uzito unaelemea sehem moja.
 
Wadau naandika hapa kutaka kujua changamoto ya vitanda vya chuma (faida au hasara zake) maana hiki kitanda changu cha mbao kina changamoto sana kila mara kinabonyea katikati.

Nabadili chaga baada ya muda kinarudi hivyo hivyo kiasi kwamba imekua kero kubwa na imenisababishia maumivu ya mgongo sasa nataka nibadili style ya kitanda je kuna mwenye uzoefu navyo anijuze tafadhari?
Kubonyea katikati nafikiri inasababishwa na magodoro feki
 
Vitanda vya chuma ukiwa shabiki wa rough kama mimi lazima uvichukie. Vinataka uende missionary tu. Sivitaki kabisa
😷 😷 😷 😷 😷 🤣 🤣 🤣 🤣 weka square pipe nene kidogo, Achana na hizo za inchi moja
 
Back
Top Bottom