SoC01 Fahari ya majina yetu ya asili Tanzania imekwenda wapi?

Stories of Change - 2021 Competition
Jul 15, 2021
15
45
Hivi sasa watanzania tulio wengi majina yetu hayana asili yoyote ya Tanzania, sana sana tumebakisha majina ya mwisho kuwa ya asili na yale ya mwanzo kuwa ya Kizungu ama Kiarabu. Mfano mzuri ni mimi hebu tizama jina langu hapo juu.

Natambua fika kuwa majina haya tulio wengi tumepewa na wazazi wetu kwa misukumo mbali mbali aidha kwa ajili ya utanda-wizi, masharti ya dini au kwa kufuata mikumbo. Na ni kweli kwamba mpaka leo na sisi tumekuwa wazazi na bado tunaendelea kufanya vivyo hivyo.

Swali la kujiuliza sasa je, majina yetu ya asili yamepoteza mvuto ama tunajisikia wa kale pale ambapo tunatumia majina hayo?

Turejee kidogo historia ili tuweze kuona fahari ya majina yetu ya asili ilipotelea wapi. Wakati wa ukoloni mawakala wa kikoloni walitangulia katika nchi za Afrika ili kuja kujionea hali halisi na kuanza kuwa sehemu ya waafrika. Mawakala hawa wa kikoloni walikuwa ni wamisionari, wafanyabiashara na wapelelezi ambao kazi yao kubwa ilikuwa ni kubadili fikra zetu ili tuweze kufikiri vile wao wanavyofikiri na kutoa taarifa kwa mabwana wakubwa juu ya hali ilivyo kwa nchi za Kiafrika.

Kati ya mawakala hawa wa kikoloni wamisionari ndo waliojikita zaidi kubadili fikra zetu ili tuweze kuyaona mambo yetu kuwa sio ya kistaarabu na yakichawi. Tukashurutishwa kuacha ibada zetu za kuabudu miti, mito, milima na mengineyo tukalazimishwa kupokea aina mpya ya ibada zilizostaarabika.

Katika mapokeo haya ya dini tulijifunza kusoma vitabu vya dini, kuhudhuria ibada, kupata ubatizo na mambo mengine kadha wa kadha. Sasa hapa ndipo changamoto zilipoanzia, kwani ili kuweza kuonyesha tumepokea dini vile ipasavyo ilitubidi kubatizwa na kupokea jina jipya kama vile ambavyo watakatifu wa dini walikuwa nayo. Hivyo ilitupasa kusahau majina yetu ya asili na kuchagua majina hayo mapya ambayo hata maana yake hatukuyajua.

Utaratibu huu uliendela hata baada ya nchi zote za Afrika na Tanzania kwa ujumla kuwa huru. Leo hii tunashuhudia vile ambayo asilimia kubwa ya watanzania ukikutana nao wanajina la Kizungu ama Kiarabu.

Leo hii ukipata mtoto na ukienda kumwandikisha hospitalini ama kwenye dini zetu husika kwa jina lenye asili ya kabila lako, kila mtu atakushangaa na kuanza kukuliza “kinachokufanya umpe mtoto jina baya hivyo ni nini”? hapo ukute umempa mtoto wako jina la Bhoke lenye maana ya ‘asali’ kwa mujibu wa Kabila la Kikuria. Tukumbuke ya kuwa majina mengi ya asili yalitolewa kulingana na matukio ambapo mtoto husika alizaliwa. Ila leo hii wengi wetu tunaona kufanya hivi ni uzandiki na ukale.

Hali hii inadhihirisha fika kabisa kuwa bado hatujapata uhuru wa fikra na kuweza kuamua mambo yetu binafsi kama watanzania huru. Kwanini mpaka leo kwenye jambo rahisi kama hili linalomhusu mtu binafsi tunaamuliwa na mifumo mingine?

Mwanamziki mkongwe marehemu Bob Marley aliimba kwenye wimbo wake wa Ukombozi na kusema: “Tujikomboe kutoka kwenye utumwa wa fikra, na sio mtu mwingine bali sisi wenyewe tunaweza kukomboa fikra zetu” (Emancipate yourselves from mental slavery; none but ourselves can free our minds).

Ni imani yangu kabisa, majina yenye asili ya makabila mbalimbali ya Tanzania yanamaana nzuri kabisa na tunayoweza kulinganisha na mazingira yetu. Lakini cha ajabu wengi wetu hatuoni tena ufahari wa kutumia majina yetu ya asili badala yake tunazidi kukumbatia majina kutoka nchi za Magharibi na kuyaona ndio yenye tija kwetu.

Kama alivyosema mwanamziki Boby Marley ni jukumu letu kukomboa fikra zetu kutoka utumwani na tuweze kufanya maamuzi yenye tija kwetu. Hivi ulishawahi kujiuliza kwanini nchi za Magharibi mpaka leo kila taifa lina majina yake ya asili ambayo yanatofautiana kutoka taifa moja kwenda jingine?

Sasa kwanini sisi watanzania tunashindwa kujikomboa katika utumwa huu wa fikra ambapo mpaka leo tunadhani kuwa na jila la Kizungu ama Kiarabu ni usasa na kuwa na jina la asili ni ukale?

Nimejaribu kuzungumza na watu wengi na kuwauliza inakuwaje wanawapatia watoto wao majina yasio na asili ya makabila yao. Wengi wao walijibu ni kwasababu ya matakwa ya dini zao. Sasa swali la msingi linakuja je, ukimpa mtoto jina lenye asili ya kabila lako litamfanya asiweze kumwabudu Mungu wake? Kwani imani na jina vinamahusiano gani?

Nimeamua kujadili mada hii leo ili tuweze kujitathimini katika swala dogo kama hili la majina na kuangalia ni kwa kiasi gani tuko huru na tumeuacha utumwa kando.

Ni dhahiri wengine wanaweza kudhani majina ni swala dogo sana na halina madhara yoyote kwenye maisha yetu. Hebu jiulize sasa, utambulisho wako uko wapi kama hata jina lako lenyewe unashindwa kujivunia nalo?

Kama tutashindwa kujikomboa katika jambo dogo kama hili la majina je, tunadhani tunaweza kujikomboa na unyonyaji mkubwa unaondelezwa na nchi za kibepari kwa ubabe mkubwa?

Leo hii inatia simanzi kubwa kuona mtu akiwa na mtoto badala ya kujua taratibu za kabila lake kwenye kutoa majina utakuta watu wanakwenda kwenye mitandao na kuanza kutafuta majina kutoka kwa watu maarufu kwenye nchi za mabeberu. Hali hii inadhihirisha kabisa tunaendelea kuwatukuza mabwana wakubwa hawa kwa kila kitu hata kiwe kidogo kiasi gani tunadhani wao ndio bora zaidi kuliko sisi.

Ni muhimu kufahamu kabisa mabepari hawa hufarijika zaidi wanapoona tunausalimisha utu wetu wote kwao kwani inakuwa rahisi zaidi kuendelea kututawala kuanzia kwenye fikra zetu mpaka kwenye rasilimali zetu.

Tukumbuke ya kuwa mabadiliko ya kweli hayaanzi na mtu mwingine zaidi yako wewe mwenyewe. Ili tuweze kukata minyororo hii ya utumwa katika fikra zetu hebu tuanzae kuenzi na kupenda asili yetu kwani bila kufanya hivyo baada ya muda mfupi tutashtuka hatuna cha kujivunia tena zaidi ya kuendelea kukumbatia kila kitu kutoka kwa mabepari.

Kwa kuhitimisha, hebu sasa tuanzishe mijadala kila mahali tulipo na kuona ni kwa namna gani tunaweza kuleta mabadiliko katika nchi yetu. Tanzania ni yetu sote na tuanze kuipenda na kuipigania kwa dhati ili kuweza kunusuru utaifa wetu, maana tusipokuwa makini hata hiki Kiswahili tunachoringa nacho punde kitakuwa cha watu wengine.
 
Kwenye majina ya asili mimi huwa nawakubali sana wa afrika kusini.

Ijapokuwa walitawaliwa na wazungu kuliko sisi, ukifuatilia majina ya vijana wao wengi maarufu utakuta ni ya asili, majina kama lasizwe, khanya, nombuso, leti, zozibini yani ni ya asili kabisa
 
Ila nadhani labda ni effects za mafanikio ya mbinu za kuua makabila na kutengeneza identity moja ya mtanzania
Manake binti wa kikurya na binti wa kinyakyusa utakuta wote wanaitwa irene badala ya kuitwa bhoke na anyubatile
 
South Africa wako vizuri sana na Botswana kidogo,japo sijaona umuhimu wa hayo majina kama uchumi wa nchi hauko stable na maisha mabovu ya watu,vita ,njaa , political instability n.k.kwangu mi naona ni issue Minor sana na inategemea vijana walijengwa vipi na mila na desturi za taifa au kabila flani
 
South Africa wako vizuri sana na Botswana kidogo,japo sijaona umuhimu wa hayo majina kama uchumi wa nchi hauko stable na maisha mabovu ya watu.kwangu mi naona ni issue Minor sana
Hakika. Watu wanataka tuwe makini na vitu vidogo vidogo. Ni kama Kiswahili kinavyopigiwa upatu. Wanaokipigia watoto wao wako Feza schools wakisubiria kwenda chuo Ulaya na Amerika. Mtu akijua Kiingereza safi anakuwa "compatible' sehemu nyingi duniani.

Itamfaa nini mtu aitwe kina la asili akiwa kwenye umasikini wa kutupwa?
 
Tukashurutishwa kuacha ibada zetu za kuabudu miti, mito, milima na mengineyo tukalazimishwa kupokea aina mpya ya ibada zilizostaarabika.
Kwahiyo we unaona hapo kwenye hivo ulitaja pana ibada kweli?
Kuhusu jina ni uamuzi wako hakuna mtu atakulazimisha lile jna unataka na hata sheria inakuruhusu kulibadili hata leo ukipenda ila ufate taratibu tu,
Kidogo kidogo tunaweza badilika
 
Haya mambo ya majina ya kiasili inategemeana na Koo, niliwahi kushuhudia kijijini mtoto kapewa jina la babu yake Ile kupewa usiku dogo hakulala, zaidi ya wiki dogo analia tu.

Wamezunguka hospital dogo Ugonjwa hana ikabidi waende Kwa waganga wakaambiwa mwenye jina Kuna vitu anataka, Kuna mibangili alikuwa anavaa na huyo anatakiwa avalishwe na pia matambiko flani yanatakiwa yafanyike.

Dogo akavalishwe bangili na hirizi na tambiko likafanyika akatulia. Sasa hayo mambo nani anayataka
 
Hivi sasa watanzania tulio wengi majina yetu hayana asili yoyote ya Tanzania, sana sana tumebakisha majina ya mwisho kuwa ya asili na yale ya mwanzo kuwa ya Kizungu ama Kiarabu. Mfano mzuri ni mimi hebu tizama jina langu hapo juu.

Natambua fika kuwa majina haya tulio wengi tumepewa na wazazi wetu kwa misukumo mbali mbali aidha kwa ajili ya utanda-wizi, masharti ya dini au kwa kufuata mikumbo. Na ni kweli kwamba mpaka leo na sisi tumekuwa wazazi na bado tunaendelea kufanya vivyo hivyo.

Swali la kujiuliza sasa je, majina yetu ya asili yamepoteza mvuto ama tunajisikia wa kale pale ambapo tunatumia majina hayo?

Turejee kidogo historia ili tuweze kuona fahari ya majina yetu ya asili ilipotelea wapi. Wakati wa ukoloni mawakala wa kikoloni walitangulia katika nchi za Afrika ili kuja kujionea hali halisi na kuanza kuwa sehemu ya waafrika. Mawakala hawa wa kikoloni walikuwa ni wamisionari, wafanyabiashara na wapelelezi ambao kazi yao kubwa ilikuwa ni kubadili fikra zetu ili tuweze kufikiri vile wao wanavyofikiri na kutoa taarifa kwa mabwana wakubwa juu ya hali ilivyo kwa nchi za Kiafrika.

Kati ya mawakala hawa wa kikoloni wamisionari ndo waliojikita zaidi kubadili fikra zetu ili tuweze kuyaona mambo yetu kuwa sio ya kistaarabu na yakichawi. Tukashurutishwa kuacha ibada zetu za kuabudu miti, mito, milima na mengineyo tukalazimishwa kupokea aina mpya ya ibada zilizostaarabika.

Katika mapokeo haya ya dini tulijifunza kusoma vitabu vya dini, kuhudhuria ibada, kupata ubatizo na mambo mengine kadha wa kadha. Sasa hapa ndipo changamoto zilipoanzia, kwani ili kuweza kuonyesha tumepokea dini vile ipasavyo ilitubidi kubatizwa na kupokea jina jipya kama vile ambavyo watakatifu wa dini walikuwa nayo. Hivyo ilitupasa kusahau majina yetu ya asili na kuchagua majina hayo mapya ambayo hata maana yake hatukuyajua.

Utaratibu huu uliendela hata baada ya nchi zote za Afrika na Tanzania kwa ujumla kuwa huru. Leo hii tunashuhudia vile ambayo asilimia kubwa ya watanzania ukikutana nao wanajina la Kizungu ama Kiarabu.

Leo hii ukipata mtoto na ukienda kumwandikisha hospitalini ama kwenye dini zetu husika kwa jina lenye asili ya kabila lako, kila mtu atakushangaa na kuanza kukuliza “kinachokufanya umpe mtoto jina baya hivyo ni nini”? hapo ukute umempa mtoto wako jina la Bhoke lenye maana ya ‘asali’ kwa mujibu wa Kabila la Kikuria. Tukumbuke ya kuwa majina mengi ya asili yalitolewa kulingana na matukio ambapo mtoto husika alizaliwa. Ila leo hii wengi wetu tunaona kufanya hivi ni uzandiki na ukale.

Hali hii inadhihirisha fika kabisa kuwa bado hatujapata uhuru wa fikra na kuweza kuamua mambo yetu binafsi kama watanzania huru. Kwanini mpaka leo kwenye jambo rahisi kama hili linalomhusu mtu binafsi tunaamuliwa na mifumo mingine?

Mwanamziki mkongwe marehemu Bob Marley aliimba kwenye wimbo wake wa Ukombozi na kusema: “Tujikomboe kutoka kwenye utumwa wa fikra, na sio mtu mwingine bali sisi wenyewe tunaweza kukomboa fikra zetu” (Emancipate yourselves from mental slavery; none but ourselves can free our minds).

Ni imani yangu kabisa, majina yenye asili ya makabila mbalimbali ya Tanzania yanamaana nzuri kabisa na tunayoweza kulinganisha na mazingira yetu. Lakini cha ajabu wengi wetu hatuoni tena ufahari wa kutumia majina yetu ya asili badala yake tunazidi kukumbatia majina kutoka nchi za Magharibi na kuyaona ndio yenye tija kwetu.

Kama alivyosema mwanamziki Boby Marley ni jukumu letu kukomboa fikra zetu kutoka utumwani na tuweze kufanya maamuzi yenye tija kwetu. Hivi ulishawahi kujiuliza kwanini nchi za Magharibi mpaka leo kila taifa lina majina yake ya asili ambayo yanatofautiana kutoka taifa moja kwenda jingine?

Sasa kwanini sisi watanzania tunashindwa kujikomboa katika utumwa huu wa fikra ambapo mpaka leo tunadhani kuwa na jila la Kizungu ama Kiarabu ni usasa na kuwa na jina la asili ni ukale?

Nimejaribu kuzungumza na watu wengi na kuwauliza inakuwaje wanawapatia watoto wao majina yasio na asili ya makabila yao. Wengi wao walijibu ni kwasababu ya matakwa ya dini zao. Sasa swali la msingi linakuja je, ukimpa mtoto jina lenye asili ya kabila lako litamfanya asiweze kumwabudu Mungu wake? Kwani imani na jina vinamahusiano gani?

Nimeamua kujadili mada hii leo ili tuweze kujitathimini katika swala dogo kama hili la majina na kuangalia ni kwa kiasi gani tuko huru na tumeuacha utumwa kando.

Ni dhahiri wengine wanaweza kudhani majina ni swala dogo sana na halina madhara yoyote kwenye maisha yetu. Hebu jiulize sasa, utambulisho wako uko wapi kama hata jina lako lenyewe unashindwa kujivunia nalo?

Kama tutashindwa kujikomboa katika jambo dogo kama hili la majina je, tunadhani tunaweza kujikomboa na unyonyaji mkubwa unaondelezwa na nchi za kibepari kwa ubabe mkubwa?

Leo hii inatia simanzi kubwa kuona mtu akiwa na mtoto badala ya kujua taratibu za kabila lake kwenye kutoa majina utakuta watu wanakwenda kwenye mitandao na kuanza kutafuta majina kutoka kwa watu maarufu kwenye nchi za mabeberu. Hali hii inadhihirisha kabisa tunaendelea kuwatukuza mabwana wakubwa hawa kwa kila kitu hata kiwe kidogo kiasi gani tunadhani wao ndio bora zaidi kuliko sisi.

Ni muhimu kufahamu kabisa mabepari hawa hufarijika zaidi wanapoona tunausalimisha utu wetu wote kwao kwani inakuwa rahisi zaidi kuendelea kututawala kuanzia kwenye fikra zetu mpaka kwenye rasilimali zetu.

Tukumbuke ya kuwa mabadiliko ya kweli hayaanzi na mtu mwingine zaidi yako wewe mwenyewe. Ili tuweze kukata minyororo hii ya utumwa katika fikra zetu hebu tuanzae kuenzi na kupenda asili yetu kwani bila kufanya hivyo baada ya muda mfupi tutashtuka hatuna cha kujivunia tena zaidi ya kuendelea kukumbatia kila kitu kutoka kwa mabepari.

Kwa kuhitimisha, hebu sasa tuanzishe mijadala kila mahali tulipo na kuona ni kwa namna gani tunaweza kuleta mabadiliko katika nchi yetu. Tanzania ni yetu sote na tuanze kuipenda na kuipigania kwa dhati ili kuweza kunusuru utaifa wetu, maana tusipokuwa makini hata hiki Kiswahili tunachoringa nacho punde kitakuwa cha watu wengine.
Nchi yetu ni yapekee Afrika ambayo haitambui makabila yake; maana yake lugha zake za asili. Ndio maana vijana wetu na wote waliopita shule wanashindwa kuwapa watoto majina yenye maana nzuri yanayotokana na lugha zetu. Ni kweli tumelogwa na dini zetu ambao wanatuweka kuona kwamba kila jina linalotokana na asili ya lugha zetu baya. Si kweli kabaisa, nakubali kuna majina yenye maana isiyofaa, lakini kwa elimu yetu tunayoipata ni rahisi sana kupata jina la luga zetu za asili lenye maana nzuri.
Ncjhi zote wanatunza lugha zao za asili; serkali ifikirie kwa undani. Serikali iangaze upya sala la lugha. Hebu tuache kutumia majina ya Kiyahudi (Kibiblia) na Kiarabu ( Quran). Narudia kusema hakuna majina ya kidini. Kwa sababu yote hayo yalikuwepo hata kabla ya Yesu au Mohamed kuzaliwa yalikuwepo. Mohame kabla hajaanzisha Uislamu aliitwa hivyo hata baba yake Abdalla alikufa bila kujua Uislamu, ila sasa hivi tuliita ni jina la Kiislamu. Hivyo hivyo kwa Wakristo, Yakobo au Yohana yallikuwepo kabla.
 
Back
Top Bottom