Wengi wetu hatujui maana ya majina yetu ila tumeyakalili

brevars

Member
Apr 15, 2023
49
71
Sijajua ni kutokujua umuhimu au ni ile hali ya kuchukulia poa tu. Wengi wetu tumekua na kujikuta tunaitwa majina utasikia hili ni jina la babu mzaa mama au jina la kaka yake na mjomba bila kujua maana ya jina hilo au asili yake.

Unakuta pia mtu unampa jina la rafiki yako au la mtu maarufu huenda mcheza mpira, mwanamuziki. Kwahiyo wengi wetu tumeyakalili majina yetu ila hatuyajui majina yetu.

Majina yamebeba Roho ndio maana watumishi kadhaa walipewa majina yaliyoendana na huduma zao.

Tujenge utalatibu wakujua maana ya jina kabla ya kumuita mtoto hii inaweza saidia.
 
Hamna lolote jina ni jina tu....

Jina langu ni jina la mtu mkubwa sana kwenye bibilia, alinipa bibi yangu aliniambia alioteshwa nitakuja kua mtumishi mkubwa sana, bibi alikua mlokole damu damu

Saivi hata siamini kwenye uwepo wa huyo Mungu.

Jina ni kama pambo tu.
 
Jina langu ni jina la mtu mkubwa sana kwenye bibilia, alinipa bibi yangu
Alikupa jina tu Ila hakukuendeleza ili uwe km huyo mtu mkubwa hapo ndipo alipofweli Bibi yako angepambana kukujenga uwe km huyo mtu mkubwa Sasa hivi ungekua mtu mkubwa km Bibi yako alivyotaka, mtu hujengwa kua kwenye nafasi fulani au kua mtu fulani tatizo watu huishia kutoa majina na kutamani mtu awe km huyo mtu bila kumjenga jinsi gani yule mtu alikua
 
Back
Top Bottom