Fahamu upande wa pili wa Dangote

Fahamu upande wa pili wa Dangote

Tapeli wa kuja kuweka almost 1 billion $
Ktk ya poli la mtwara,basi huyoo tapeli ana tufaa mnoo,na ku created almost 10000 jobs opportunities coming brother wacha hizo bana,muogope hata mungu bas kidogo,umeukimbia ukweli completely,why?
 
Uko very ungrateful wewe wacha hizo,let's base to da facts usilete uvyama. Ktk kila jambo
 
Dangote i know ni kind of Taperi fulani na kila afanyacho ni kwa faida yake tu... Jamaa anaweza hata akajenga kiwanda lakini akawa hajatumia hata senti moja yake kwa jinsi alivyo kiboko.... hata Bima anakatia kila kitu lakini halipi.... pwaaa
 
Nadhani kuna kitu wanacho wahindi sisi ngozi nyeusi hatuna. Kama na Nigeria anawatumia zaidi wahindi kuliko weusi nadhani ni wajibu wetu kuangalia kwa nini wamiliki wengi wa makampuni wanawatumia zaidi wahindi.
Ni rahisi kukwepa kodi na mambo mengine kama umeajiri wageni.

Wazawa wakiona kosa dogo lazima walilete hapa JF halafu magazeti wanalichukuwa.
 
Dangote i know ni kind of Taperi fulani na kila afanyacho ni kwa faida yake tu... Jamaa anaweza hata akajenga kiwanda lakini akawa hajatumia hata senti moja yake kwa jinsi alivyo kiboko.... hata Bima anakatia kila kitu lakini halipi.... pwaaa

Kumbe sio kila mzungu ni padri. Pia sio kila mwarabu ni shehe. Jamaa ni tapeli flani anayejua kutumia vizuri udhaifu wa mamlaka za kiafrika. Kwa jumla si mshindani mzuri wa kibiashara. Serikali inatakiwa iwe angalifu sana. Isije kuwa inamjenga mtu mmoja na kumfanya awe na nguvu huku wengine wakipata taabu sana katika uendeshaji wa biashara zao. Hebu ona anavyowanyorosha wenzetu wa Zambia na kwao Nijeria.
Dangote Selling Stolen Cement Below Value to Dodge Taxes – Source
Dangote Cement denies competitors’ allegations | Companies -
Transport staff ask Buhari to probe Dangote, say he is underpaying for labour - Vanguard News
 
nilipomuuliza sababu ya wao wazee kugawa ardhi bure kwa Dangote aliniambia kwamba wao waliamini Dangote si mfanyabiashara ni Alhaji kwa hiyo walitoa ardhi kwa Alhaji ili ajenge kiwanda kiwasaidie watu..

Nilishangaa sana, lakini kilichonifurahisha ni kwamba wanajuta maana zaidi ya laki tano na ziara ya Mecca hawajafaidika tena kwa namna walivyotarajia.

Mimi naomba nichangie angle moja ya taarifa yako muhimu sana.

La Dangote kupewa ardhi bure. Hili nalikubali kwa tarumbeta na mayowe kwa saabu sitaki foreigner anunue ardhi miaka 99! It is that simple.

Wazee wa vijiji waliompa Dangote ardhi bure walifanya jambo la heri hata kama walihongwa safari za Mecca, kama unavyosema, kwa sababu ardhi imebaki ya kwetu na tukitaka tunamtimua Dangote na wahindi wake on any given Sunday.

Magufuli akipandwa na maruhani usiku asubuhi tunamwambia Dangote jikate! Cement tulikuwa nayo, 13,000 sasa hivi 11,000 ya Dangote, big freaking deal, sio poa lakini sio hatari, jikate na wahindi wako, sepa!

Subsidies alizopewa Dangote kwa nini wasipewe Twiga au cement ya Wazo Hill ambavyo ni viwanda vya kibongo ( or used to be)? Viwanda vya nje vikishakomba fedha vinapeleka nje. Listen, the reason Mafuru amefukuzwa kazi Hazina leo ni kwa sababu amesema akiwa Clouds TV kwamba miradi mikubwa mingi ambayo nchi inapeleka hela sasa hivi tunafanya na foreign investors, pesa haibaki hapa kwenye mzunguko, Magufuli hakupenda kusikia huo ukweli. To hell with these Foreign Direct Investments multinationals.
 
Mimi naomba nichangie angle moja ya taarifa yako muhimu sana.

La Dangote kupewa ardhi bure. Hili nalikubali kwa tarumbeta na mayowe kwa saabu sitaki foreigner anunue ardhi miaka 99! It is that simple.

Wazee wa vijiji waliompa Dangote ardhi bure walifanya jambo la heri hata kama walihongwa safari za Mecca, kama unavyosema, kwa sababu ardhi imebaki ya kwetu na tukitaka tunamtimua Dangote na wahindi wake on any given Sunday.

Nashangaa unaposema kwa vile ardhi alipewa bure basi inabaki ni yetu. Akipewa mtu ardhi ainakuwa yake, tofauti na kununua ni kwamba hatoi fedha, basi. Baada ya kupewa ardhi bure, bila shaka alipewa kibali rasmi cha kuonyesha hiyo ardhi ni yake (siyo yetu).

Nimewahi kuishi Nigeria kwa miezi tisa. Naona Mondoros amejua namna wenavyofanya biashara huko. Ni fraud at at every point.

Nirudie kwamba watu kama Dr Kafumu wanaotaka kutuaminisha kwamba tuliingia mkataba mzuri na Dangote hawana sifa za kusema hivyo. Ni wao waliotuingiza mkenge wa kuwekeana mikataba mibaya na ya siri ya uchimbaji wa dhahabu.

Those who have been around for a while will recall the following: " Tumenyonywa vya kutosha, tumenyanyaswa vya kutosha. Ni unyonge wetu ndio ulitufanya tunyonywe, tunyanayaswe na kudharauliwa. Sasa tunataka kufanya mapinduzi".
 
Nashangaa unaposema kwa vile ardhi alipewa bure basi inabaki ni yetu. Akipewa mtu ardhi ainakuwa yake, tofauti na kununua ni kwamba hatoi fedha, basi. Baada ya kupewa ardhi bure, bila shaka alipewa kibali rasmi cha kuonyesha hiyo ardhi ni yake (siyo yetu).

alipewa eneo ajenge kiwanda, hakununua.

ardhi bado ya kwetu, siku akitaka kusepa ang'oe kiwanda chake, ardhi aiche, hakuna aliyekula hela ake kupewa ardhi.
 
Sina muda wa kubishana na watu tu lakini mengi uliyoongea mtoa mada ni uongo mtupu! Mfano mdogo tu ni kwamba, suala la Dangote kupewa ardhi halina uhusiano na upendeleo bali ni serikali yenyewe wakati wanaweka incentives kwa strategic investors; ikawekwa hilo suala la ardhi kama moja ya incentives. Na hiyo ni sheria ambayo hata JK ameikuta kwa sababu ilitungwa mwaka 2002; kipindi cha Mzee Mkapa!!

Kuhusu wanakijiji na ardhi yao; hebu fanya utafiti kidogo utaona tatizo lilikuwa wapi!!

But all in all, kusema "Dangote labda abadilike ndio tutaweza kufaidi uwepo wake hapa Tanzania...." ni ujinga uliopitiliza! Hivi kabisa kwa ufahamu wako unaamini kuna mwekezaji atakayekufanya wewe ufaidi?
 
Umesahau kuwa yeye ndio the Richest Man in Africa! Angekuwa hivyo unavyomuelezea asingeweza kufikia mafanikio haya, ukiambiwa uthibitishe maneno yako utabaki kutoa macho tu kwenye screen yako, acha ujinga!
 
alipewa eneo ajenge kiwanda, hakununua.

ardhi bado ya kwetu, siku akitaka kusepa ang'oe kiwanda chake, ardhi aiche, hakuna aliyekula hela ake kupewa ardhi.

Yaani hana "title deed" ya ardhi aliyojenga kiwanda? Kuna benki itatoa fedha za kujenga kiwanda kwenye ardhi ambayo haina title deed?
 
Ukiona propaganda za "sizitaki mbichi hizi", zimezidi hivi ktk social media ujue hili saga limemwelemea Mjomba Magu na tujue tayari jamaa anajiandaa kung'oa mitambo ya kiwanda chake kukipeleka Kenya!!

Sasa mwoneni naye huyu, jamaa insha ndeefu na kila mstari umebebwa na na maneno..... jamaa ni tapeli .....tapeli.....tapeli, lakini cha ajabu hata hasemi alimtapeli nani, nini na wapi!!

Possibly, ukweli wa haya waweza kuwa ni the opposite.

Kwamba, inawezekana CCM ndiyo walikuwa wanataka kumtapeli jamaa na kwa kuwa kawashtukia na kama ilivyo asili yao kutapeli sasa wanajaribu kuigeuza picha up side down ili tushindwe kuisoma vyema!!
fact[emoji106]
 
Dangote kumlaumu ni ujinga ni sawa na kuilaumu IPTL. Hakuna mtu anafanya biashara ili asipate faida! Hao vichwa maji waliokubali kuingia hiyo mikataba na Dangote ndio wakulaumiwa. Na Mkuu kama kweli ukweli ndio huu mbona Serikali hii isiweke kila kitu hadharani? Ukiwaambia mikataba mikubwa ipitie bungeni Serikali hiyo hiyo inakataa. Kama serikali inajua jamaa anawalipa wafanyakazi hela kidogo je? kwan kima cha chini ni shiling ngapi? Tatizo hii Serikali ya CCM inafanya mambo gizan then yakiharibika ndio wanakuja hadharani tena kulalamika
 
Yaani hana "title deed" ya ardhi aliyojenga kiwanda? Kuna benki itatoa fedha za kujenga kiwanda kwenye ardhi ambayo haina title deed?


kwanza, umejuaje Dangote kakopa hela benki kujenga kiwanda?

second, hata Lukuvi katangaza juzi tena jamani, nashangaa hulijui hili, M-Nigeria au mjuba yeyote wa kuja nchi hii haruhusiwi kumiliki title deed ya ardhi Tanzania!

tuliseme mara ngapi hili?

title deeds za diaspora waliozaliwa hapa na baadae kuomba uraia nje title deeds zao zinapelekwa Ikulu kufutwa, sembuse m-Nigeria kaja hapa 2014?

ardhi ya Tanzania ni kwa Watanzania natural born citizens, au kama we ni documented alien umeomba kuandikishwa uraia hapa ukapewa ardhi, tukishtuka hujakana wa kwenu ulikotoka hapa tunakufuta na title deed tunai shred.

niliposikia kwamba Dangote ardhi yenyewe kawekwa bure bure si yake ya kununua nikasema Alhamdullilah Allakuli Haal, Hadha Min Fadhil Rabbi, hizi ndio fadhila za Munyanzi Mngu, siku yeyote tukitaka tunamwambia Dangote huna chako hapa, sepa!
 
Walioingia naye mikataba ni ccm ....

Wanaovunja mkataba ni Ccm.....

Waliompokea ni Ccm......

Wanaotaka aondoke ni Ccm.....

Tafakari chukua hatua.........

Ccm ya JPM imeongoka. Imetubu na kuacha ufisadi kwa hiyo tusiilaumu sana.
 
Mbona hamkuyasema haya kabla

Mbona nyie ni wababaishaji sana.Mnapenda ujanja ujanja tu na uongo uongo kwenye uongozi wenu
 
Back
Top Bottom