Fahamu upande wa pili wa Dangote

Fahamu upande wa pili wa Dangote

Walioingia naye mikataba ni ccm ....

Wanaovunja mkataba ni Ccm.....

Waliompokea ni Ccm......

Wanaotaka aondoke ni Ccm.....

Tafakari chukua hatua.........
ccm ni wajanja kuliko unavyodhani ndio maana wamekuleteeni magufuli. so far hakujaharibika kitu. baada ya kuingizwa kuwekeza akitegemea bwerere amakutana na kisiki cha jpm. hawezi kukimbia baada ya kuwekeza ila ku fall in line na matakwa ya sheria na maslahi ya nchi sio kutugeuza shamba la bibi. Maslahi halali ya mwekezeja bila shaka yamehifadhiwa.
 
Walioingia naye mikataba ni ccm ....

Wanaovunja mkataba ni Ccm.....

Waliompokea ni Ccm......

Wanaotaka aondoke ni Ccm.....

Tafakari chukua hatua.........

Ndio siasa yetu hiyo Mkuu.
...Waliomsema Lowasa ni FISADI number One ni CHADEMA
Waliompa kiti agombee URAIS wetu ni CHADEMA
Waliosema wanaomshabikia FISADI Lowasa wakapimwe akili ni CHADEMA
Leo wanaosema mwenye ushahidi wa UFISADI wa Lowasa aende mahakamani ni CHADEMA
Yaani ni CONFUSION tupu!!!
 
Huyu jamaa kaja na povu la wahindi. Usha jiuliza kwanini aliwapa wahindi wasimamie wakati wa erection na commissioning?. Ni watanzania wangapi wenye uwezo wa kusimamia project kubwa ya cement na wasiibe. Kuna thread humu ya dangote akilalamika wizi mkubwa unao fanywa na wazawa wenzutu huko mtwara. Mbali na hiyo hao wahindi hawahusiki ata kidogo kwenye kuensesha kiwanda. Kiwanda kinaendeshwa na wachina " sinoma" ambao wako kwenye guarantee period na baada ya miaka miwili watafanya hand over kwa wazawa. Na hao wahindi unao wasema walio kwenye mgt ni mageneral managers walio kuwa wanasimamia project. Na na soon baada ya project kuisha na ku hand over wanasepa zao. Swala la coal; akati Dangote inaingia kwenye operation bara bara ya mtwara- mbinga ilikuwa bado inashida kubwa hivo transport cost per ton of material ilikuwa kubwa ukilinganisha na ku import. Hali hii ilisababisha kiasi cha makaa ya mawe kuagizwa toka nje ya nchi ambapo soon bara bara itakapo isha inasemekana kuna lory 600 zinakuja kwa ajili ya kubeba raw material pamoja na cement.


Swala la kuua viwanda pengine hauja elewa kinacho fanyika. Kwanza dangote anajenga viwanda kwa gharama ndoko akiwatumia wachina ambao wako kama cheap labor hivo kufanya return on investment kuwa kubwa na kufanya payback period kuwa ndogo huku akiwa na most competitive technology. Swala ambalo viwanda vingi vya Tanzania havina. Inasemkena kila kitu ni automated kiasi kwamba hata idadi ya man power I apungua hivo wachache wenye uelewa mkubwa ndio wanao patiwa nafasi . Hayo ndio minayo yajua kihusu dangote hayo mengine ndo nimesikia kwako ngojea niyafanyie utafiti
Samahani kwa kukoti
Ila kwenye hili swala la Dangote
Position ziko managed na wahindi na finance ni mageria
Hr ndo yuko mbongo ambae kazi zote naye anatumwa na wahindi tu
Kuhusu operation chief kweli kiwanda kimejengwa na Sinoma ambao kazi yao ujenzi na kuinstall kiwanda but head of production, contraction, hadi head of security ni muhindi na hata mifuko ile ya bag cement mifuko inatengenezwa buguruni kiwanda cha kihindi
Watu wengi wanalalamika operation za kihindi kwa Dangote
Mfano wamestop uzalishaji lakini kuna wafanyabiashara walilipia pesa zao so hata kutoa information kwa Wateja ni shida
Kwa MTU amabae yuko enged na Dangote hatakuwa na perception ya watu wa nje ambao wanayasikia tu na kuamini huyu Dangote tunae. Msimulia
In short Dangote ni msanii sana
Sema inaonekana aliingizwa chaka na swala la. Gesi ndo hilo ambalo mpaka sasa nikilio kikubwa kwa Dangote juu ya selikali out of that kiukweli ni shida ila hata price aliokuja nayo si ambayo tunaiamini maana viwanda vyote vya cement tofauti ambayo Dangote alikuja nayo ni elfu 1000 mpak 2000 but after that wakawa sawa sema. Transportation cost ndo kinachofanya watu wa mtwara waone bei imepungua
 
Ukiona propaganda za "sizitaki mbichi hizi", zimezidi hivi ktk social media ujue hili saga limemwelemea Mjomba Magu na tujue tayari jamaa anajiandaa kung'oa mitambo ya kiwanda chake kukipeleka Kenya!!

Sasa mwoneni naye huyu, jamaa insha ndeefu na kila mstari umebebwa na na maneno..... jamaa ni tapeli .....tapeli.....tapeli, lakini cha ajabu hata hasemi alimtapeli nani, nini na wapi!!

Possibly, ukweli wa haya waweza kuwa ni the opposite.

Kwamba, inawezekana CCM ndiyo walikuwa wanataka kumtapeli jamaa na kwa kuwa kawashtukia na kama ilivyo asili yao kutapeli sasa wanajaribu kuigeuza picha up side down ili tushindwe kuisoma vyema!!
Eti anaajiri wahindi, kwanini asijiulize sababu za Dagonte kuajiri wahindi maana hata huko kwao Nigeria ameajiri wahindi kwenye menejimenti! Ukisoma katikati ya mistari ni rahisi kuona kuwa huyu jamaa katumwa!
 
Watanzania tulishangilia sana bei ya Cement ya Dangote na hapo ndipo tulipoonekana Mazuzu mbele ya wenye akili. Hiyo inaitwa penetration strategy in marketing. Unashusha bei ya bidhaa ili kuwaua wapinzani wako wakongwe waliopo katika soko, wakishakufa ukabaki mwenyewe sasa unarudisha bei mara mbili zaidi kufidia maana huna mpinzani katika soko. Mfano mzuri ni kampuni ya ndege ya fast jet. walipoingia walianza na nauli sh 32,500 Dar Mwanza, tukashangilia sana baada ya kuona amebaki mwenyewe kwenye soko na Precision wapo hoi bei ilipanda mara 10 zaidi. Sasa hii ya kumpendelea Dangote peke yake ilihali wengine tukiwaacha wapambane katika mazingira Magumu sio fair kabisa maana katika soko wote wanapambana pamoja. Serikali kueni makini sana na hawa Wahindi pamoja na wachina
 
wabongo kwa majungu na kuongea tumejaaliwa hivi kwa akili ya kawaida unadhani kati ya serikali na dangote nani anamuhitaji sana mwenzake??
hivi kuna nchi gani ambayo itakataa investment kama ya dangote?
marekani trump hadi anaweka vikwazo na gharama kubwa ili viwanda visiondoke marekani na kushusha kodi by 20% yote kubembeleza uwejezaji leo wewe huku tanzania unasema eti hatumhitaji dangote aondoke tu.
 
Mtu amewekeza half a billion dollars unamwita mbabaishaji!?
Dunia ya wale nchi zinzshindani kuwa na sera nzuri na vivutio mbalimbali kuvutia foregn investors, Misri baada uchumi wake kuyumba waliamua kushusha bei ya nishati ili kushawishi investor kujenga viwanda na iliwasaidia kwa kiwango fulani maana kuna siku nilikuwa naangalia news kupitia ktn tv ya kenya ambapo baadhi ya wachumi walikuwa wakishauri serikali ya kenya kuangalia upya gharama za nishati kwani walipoteza wawekezaji ambao waliamua kwenda Misri na south Africa. So suala la kuvutia ili kushawishi investor ni muhimu la kuzingatia ni serikali na idara zake kuwa na mikakati inayotekelezeka na yenye manufaa pande zote.
 
Ukiona propaganda za "sizitaki mbichi hizi", zimezidi hivi ktk social media ujue hili saga limemwelemea Mjomba Magu na tujue tayari jamaa anajiandaa kung'oa mitambo ya kiwanda chake kukipeleka Kenya!!

Sasa mwoneni naye huyu, jamaa insha ndeefu na kila mstari umebebwa na na maneno..... jamaa ni tapeli .....tapeli.....tapeli, lakini cha ajabu hata hasemi alimtapeli nani, nini na wapi!!

Possibly, ukweli wa haya waweza kuwa ni the opposite.

Kwamba, inawezekana CCM ndiyo walikuwa wanataka kumtapeli jamaa na kwa kuwa kawashtukia na kama ilivyo asili yao kutapeli sasa wanajaribu kuigeuza picha up side down ili tushindwe kuisoma vyema!!
Mwenzio kaeleza kwa fact na wewe tupe fact how ccm walitaka kumtapeli?
 
wabongo kwa majungu na kuongea tumejaaliwa hivi kwa akili ya kawaida unadhani kati ya serikali na dangote nani anamuhitaji sana mwenzake??
hivi kuna nchi gani ambayo itakataa investment kama ya dangote?
marekani trump hadi anaweka vikwazo na gharama kubwa ili viwanda visiondoke marekani na kushusha kodi by 20% yote kubembeleza uwejezaji leo wewe huku tanzania unasema eti hatumhitaji dangote aondoke tu.
Ha ha ha
 
Dangote labda abadilike ndio tutaweza kufaidi uwepo wake hapa Tanzania, ila kwa jinsi alivyo na ninavyomfahamu..kwa sasa kuondoka kwake ni nafuu kwa Watanzania na Taifa.

Yule bwana hawezi kufanya biashara bila utapeli hata mfanyakazi wake wa chini kabisa anajua. Jamaa anaingia mahali kwa lugha tamu sana na ahadi kibao, lakini si mtu yule.

Wapo wanaosema kuhusu ajira za watanzania walioko pale, ni hivi wafanyakazi wataalamu walioko pale ni wale waliokuwa kwenye viwanda vingine vya cement vilivyokuwa vinawalipa vizuri ila baada ya kusikia tishio la ujio wa likiwanda kubwa ambalo lingepewa gas, exemption ya kodi n.k likapunguza bei ya cement viwanda hivyo vingekufa kwa kushindwa kujiendesha,

Hatua mojawapo zilizochukuliwa na viwanda bora kama vile Twiga na vingine ni kupunguza wafanyakazi kwa kiasi kikubwa ambao wengi walienda Dangote kulipwa ujira mdogo sana maana yeye Dangote anatumia management ya Wahindi.

Kule Nigeria alianza biashara zake kwa style ya kuwahonga viongozi wakuu na wakampa excemption ya kodi, matumizi ya barabara hovyo na vitu vingine akashusha bei ya Cement, viwanda vingine vikafa akabaki yeye mwenyewe akishikilia kama 90% ya soko la cement na Lafarge kama chini ya 10% vingine vilikufa baada ya kuhakikisha kwamba ameviua akapandisha bei ikarudi kama zamani.

Hivyo ndivyo alitaka kufanya Tanzania, JK alimpa maeneo makubwa sana, mpaka na eneo la kujenga bandari yake binafsi, jambo ambalo kwa maoni yangu naona ilikuwa hatari hata kwa usalama wa nchi.

Eneo lililojengwa kiwanda na mining lilikuwa la vijiji vitano, ni eneo kubwa ambalo lilikuwa mali ya wananchi, Dangote kwa kushirikiana na viongozi wa serikali ya awamu ya nne waliwatapeli wale wazee kwa kuwapa vitu vidogo vidogo na ziara ya kwenda kuhiji kwa wazee wachache pamoja na laki tano tano na ahadi kibao wakabariki kuiacha ile ardhi na wale wazee wakatumika kuwashawishi wengine wakaingia kingi.

Mara kadhaa nilikuwa nikiwaona hawa wazee wanaojiita wenyeviti wa vijiji vile wakiambaa ambaa pale nje ya kiwanda cha Dangote wakitapeli watu kwa ahadi ya kuwaunganishia vibarua kiwandani wakati hata wao hawana ruhusa ya kuingia ndani ya kiwanda, wazee wamepigika wanajuta tu kimoyo moyo.

Niliwahi kujaribu kuongea na mmoja wao ambaye alikuwa mwenyekiti wa wenyeviti wakati huo nikiwa kiongozi wa chama cha wafanyakazi hapo Kiwandani, nilipomuuliza sababu ya wao wazee kugawa ardhi bure kwa Dangote aliniambia kwamba wao waliamini Dangote si mfanyabiashara ni Alhaji kwa hiyo walitoa ardhi kwa Alhaji ili ajenge kiwanda kiwasaidie watu..

Nilishangaa sana, lakini kilichonifurahisha ni kwamba wanajuta maana zaidi ya laki tano na ziara ya Mecca hawajafaidika tena kwa namna walivyotarajia.
Mtindo wa ufanyaji kazi wa Dangote ni wa kitapeli tapeli tu, anatapeliwa kuanzia mfanyakazi wake wa chini mpaka Rais na mawaziri wakiingia kingi wanatapeliwa.

Kule Nigeria, ana kiwanda kikubwa Four kiln lines kwenye state ya Obajana na kingine Ibese, wafanyakazi zaidi ya 60% ni wahindi, wanaishi vizuri kila kitu wanachotumia ni tofauti na weusi, magari, nyumba za kuishi n.k ni tofauti kabisa.

Wahindi wanaletwa wakiwa hawajui kitu kabisa wanafundishwa na weusi (wanigeria) halafu wakishajua wanawasimamia weusi, wanawanyanyasa sana waafrika, pale ndipo nilipojua kwamba Tanzania ni nchi nzuri sana na siku zote nawambia ukitaka kujua uzuri wa nchi yetu Tanzania nenda Nigeria. Hususanu kufanye kazi kwa Dangote.

Wakati Dangote anafungua kiwanda Tanzania, alikuwa anaahidi kuajiri watanzania lakini ukweli ni kwamba alikuwa ameandaa makontena ya wahindi kuja Tanzania kama ilivyo Nigeria, thanks to God Magufuli akaingia Madarakani.

Wale wahindi wachache waliokuwepo walichukia sana wakaanza hata kukuza mambo au kutunga uongo wakiilaumu Serikali ati kwa kuweka vikwazo vingi, wakati mwingine wanamdanganya Dangote kuhusu Serikali yetu na Watanzania ili wao wapate faida. Ninao ushahidi wa mambo baadhi ambayo kwa makusudi kabisa management ya kihindi ilikuwa ikimdanganya Dangote kwa faida yao.

Mojawapo ilikuwa ni ubora wa makaa ya Mawe ya Tanzania, tulikuwa na vijana wetu maabara pale, hata mimi niliposikia kwamba makaa yetu ya mawe yana quality ya chini niliumia sana niliwauliza wahandisi wetu waliokuwa maabara wakasema ni uongo.

Hiyo ilikuwa mbinu ya wahindi kufanya biashara na makampuni ya South Afrika kwa faida yao huku wakichafua bidhaa zetu.

Lingekuwa jambo la ajabu sana kama serikali ingekubali uhuni huo, nawapongeza sana Mawaziri hawa wa awamu ya tano kwa kutumia elimu yao vizuri kuchunguza hilo kwa sababu hata enzi zile tulikuwa tuwaeleza serikali kila tunapopata nafasi lakini enzi ya awamu ya nne ilikuwa enzi ya aina yake. tulionekana wapuuzi au maskini wanoko.

Watanzania tunapopinga au kutetea ni vema tukatafuta ukweli kwanza, Dangote industries ukiisikia kwenye vyombo vya habari utaona ni mkombozi kwa watanzania, lakini kwa namna ilivyo na inavyotaka ifanyiwe ni hatari sana kwa taifa.

Tumshukuru sana Rais na serikali kwa msimamo wake. Dangote hana tofauti na akina Carl peters wa zamani labda abadilike.........

Itaendelea wiki ijayo

Tanzania ya viwanda.
 
Karuka tena karuka, matunda hakufikia,
Mwisho wake akachoka, kachoka hata mkia,
Sizitaki mbichi hizi, sungura akagumia,
Naona nafanya kazi bila faida kujua.


.
 
Dangote is running 500 trucks kila siku up and down,liters ngapi za diesel anaunguza hapo?
na madereva 500 wako ktk pay rolling yake eeh?
ananatumia 4millions $ kwa diesel tu za ku run factory yake,wafanyakazi almost 10000 wame ajiliwa,you can imagine mshahara kiasi gani kila mwezi wanalipwa,Tazama matairi mangapi hapo ktk hizo truck 500 yanatumika? na yote yamelipiwa ushuru hayo matairi,Tazama oil liters ngapi zinahitajika ktk hizoo trucks eeh? na vyote hivyo vimelipiwa ushuru,hii ni mifano.midogo tuu nimekupa ya kiasi gani jamii ina nufaika nae alafuu wewe unamuita Tapeli Sio???
katafute issues ya kuandika humu ndani,ila sio concerning Dangote,Kwanza humjuw hata kidogo unataka kuupotosha uma wa watanzani tu hapa aaahh
Wewe akili zako vipi. .....nani kakwambia kuwa tapeli hatumii gharama. akili zako zipo local sana.
 
Wewe akili zako vipi. .....nani kakwambia kuwa tapeli hatumii gharama. akili zako zipo local sana.
Wacha hizo tafuta kingine bana wee vp kusoma hujuw bac hata picha,jiongeze japo kidogo bac aaah
 
Eti anaajiri wahindi, kwanini asijiulize sababu za Dagonte kuajiri wahindi maana hata huko kwao Nigeria ameajiri wahindi kwenye menejimenti! Ukisoma katikati ya mistari ni rahisi kuona kuwa huyu jamaa katumwa!
Straight up
 
Eti anaajiri wahindi, kwanini asijiulize sababu za Dagonte kuajiri wahindi maana hata huko kwao Nigeria ameajiri wahindi kwenye menejimenti! Ukisoma katikati ya mistari ni rahisi kuona kuwa huyu jamaa katumwa!
Ila humu atachemsha tuu maanake hata mtoto wa darasa la 7 anajuwa sababu kubwa za figisu figisu anazofanyiwa dangote,zero brain huyu alioleta utumbo huu
 
Back
Top Bottom