Fahamu namna ya kuperuzi JamiiForums BURE

Fahamu namna ya kuperuzi JamiiForums BURE

Kwa wale ambao hawajawahi kuisikia internet.org, ilitambulishwa na Facebook mwaka jana kama njia ya kuwaunganisha theluthi mbili ya idadi ya watu duniani ambao hawana mtandao wa intaneti. Kupitia internet.org, Facebook imeweza kuwafikia watu bila gharama yoyote zaidi ya kifaa anachokitumia.

Nchini Tanzania, wateja wanaotumia mtandao wa tiGO wataweza kuperuzi JamiiForums.com BURE kupitia kiunganishi (app) cha internet.org (kwa watumiaji wa android tu)

Kurasa nyingine ambazo zitaweza kutembelewa zinajumuisha:
AccuWeather, BBC News, BBC Swahili, BabyCenter & MAMA, BrighterMonday, Daily Nation, Facebook, Facts for Life, Girl Effect, Facebook Messenger, ZoomTanzania, UNICEF Ebola Information, Wattpad na Wikipedia

Mpango huo ulitangazwa na Facebook Julai 2014 na umezinduliwa kwa ushirikiano na kampuni ya simu ya Airtel ambayo pia ilikuwa kampuni ya kwanza kupeleka huduma hiyo nchini Zambia.

Huduma kama hii ilizinduliwa Tanzania miezi michache iliyopita kupitia kampuni ya simu za mkononi ya tiGO.

Gharama za kutumia mtandao wa Intaneti imekuwa kikwazo kikubwa kwa watumiaji wa nchi zinazoendelea wanaotaka kutembelea tovuti mbalimbali hivyo huduma hii itawarahisishia wengi ambao hawawezi kumudu gharama kuweza kutembelea mitandao husika bila gharama.

Download App ya Internet.org hapa


tanzania1.jpg

hakuna kitu hapo iyo adi ukiwa na bundle ndo uta enjoy kweli cha bure ni bure speed ndogo yani nili install na kuifutilia mbali iko bored aina speed
 
Masoud kisonzela mkuu hiyo airtel ya wiki kwa buku iloje kiongoz naomba muongozo mkuu.
 
embu niambie hiyo airtel ya buku inakuwa vp mkuu.


piga *148*88# chagua bundle then internet ya wiki then chagua package uipendayo.

1000 unapata 800 MB per week.

Karibu.
 
Nasikitika kwamba hiyo bure sio bure.
Nimerudi zangu eatel najilia vyangu kwa buku per week.
Hiyo tigo eti mpaka uwe na kifurushi ndio utumie JF bure. Salsa Luna maana gain ya bure? *148*88# bado in baba lao.
 
Nasikitika kwamba hiyo bure sio bure.
Nimerudi zangu eatel najilia vyangu kwa buku per week.
Hiyo tigo eti mpaka uwe na kifurushi ndio utumie JF bure. Salsa Luna maana gain ya bure? *148*88# bado in baba lao.

Mimi wala sijahangaika nayo.Airtel wiki buku nahangaika nini?
Mzima lakini Profesa Mkiu?
 
Last edited by a moderator:
Jamii forums na nyie acheni kudanganya watu hiyo apps inafunguka mpaka uwe na salio kama huna salio haifunguki sasa uwo UBURE uko wapi?
TUACHE KUDANGANYA WATU
 
Mimi mzima nifah! wewe je!
Mimi ni Profesa Mkiu hawa jamaa wameunganisha ID zangu so prof mkiu haipo tena kwenye uso wa jf.

Duh!Mbona juzi kati tu hapo nilikuona? Haya bwana mie mzima pia.
Mimi pia nilikua na kifekero id ikaunganishwa na hii ya nifah.Ajabu nimemuona mtu anaitumia ile id humu!
 
Last edited by a moderator:
Duh!Mbona juzi kati tu hapo nilikuona? Haya bwana mie mzima pia.
Mimi pia nilikua na kifekero id ikaunganishwa na hii ya nifah.Ajabu nimemuona mtu anaitumia ile id humu!


Hawa jamaa siku hizi wamevurugwa.
Mimi nilimtaja kwa jina la utani mwanasiasa mmoja hivi, kwa hasira ndio wakaunganisha majembe yangu.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom