Fahamu namna ya kuperuzi JamiiForums BURE

Fahamu namna ya kuperuzi JamiiForums BURE

JamiiForums

JF Official Account
Joined
Nov 9, 2006
Posts
6,249
Reaction score
5,743
Kwa wale ambao hawajawahi kuisikia internet.org, ilitambulishwa na Facebook mwaka jana kama njia ya kuwaunganisha theluthi mbili ya idadi ya watu duniani ambao hawana mtandao wa intaneti. Kupitia internet.org, Facebook imeweza kuwafikia watu bila gharama yoyote zaidi ya kifaa anachokitumia.

Nchini Tanzania, wateja wanaotumia mtandao wa tiGO wataweza kuperuzi JamiiForums.com BURE kupitia kitumizi (app) cha internet.org (kwa watumiaji wa android tu)

Kurasa nyingine ambazo zitaweza kutembelewa zinajumuisha:
AccuWeather, BBC News, BBC Swahili, BabyCenter & MAMA, BrighterMonday, Daily Nation, Facebook, Facts for Life, Girl Effect, Facebook Messenger, ZoomTanzania, UNICEF Ebola Information, Wattpad na Wikipedia

Mpango huo ulitangazwa na Facebook Julai 2014 na umezinduliwa kwa ushirikiano na kampuni ya simu ya Airtel ambayo pia ilikuwa kampuni ya kwanza kupeleka huduma hiyo nchini Zambia.

Huduma kama hii ilizinduliwa Tanzania miezi michache iliyopita kupitia kampuni ya simu za mkononi ya tiGO.

Gharama za kutumia mtandao wa Intaneti imekuwa kikwazo kikubwa kwa watumiaji wa nchi zinazoendelea wanaotaka kutembelea tovuti mbalimbali hivyo huduma hii itawarahisishia wengi ambao hawawezi kumudu gharama kuweza kutembelea mitandao husika bila gharama.

Download App ya Internet.org hapa


tanzania1.jpg
 
Habari nzuri kwa watumiaji wa mtandao wa TiGo nna'browse Jamii Forums kwa free data.

JamiiForums inapatikana BURE kwa wateja wa tiGO Tanzania kupitia 0.internet.org

- Ni miezi michache baada ya huduma kama hii kuanza kutolewa kwa wateja wa Airtel nchini Kenya


attachment.php


attachment.php
 

Attachments

  • 1235007_845643198833009_6297717435861988827_n.jpg
    1235007_845643198833009_6297717435861988827_n.jpg
    27.3 KB · Views: 54,304
aisee kwa hili nmewakubali tigo...wamejitahidi Sana..sasa jf bureeh
 
0713?
poa ila mi natumia Vodacom na airtel
 
Big up to tigo,Big up to JF
Hapo JF itazidi kuenea,idadi ya visitors itaongezeka hence business opportunity kwa JF as a Mtandao.
Once again,Big up to tigo & JF

nxon , Invisible ,jaribun ku lobby as well na Vodacom na Airtel kuukuza huu mtandao.

Pia hii advert isiishie tu hapa JF,tunataka kuiona ikirushwa live Runingani na akina Joti,kama vile Joti anavyoinadi Facebook ya bure kwa kiswahili through tigo advertisement.

Free JF surfing through tigo Internet advert should be quickly Composed na ipewe airtime ya kutosha.

Tuko tayar kuchangia.

Go JF, go JF.

Objective iwe ni kila mtumiaji smartphone bongo awe na access na JF, full time, Kiganjani kwake kabla ya October 2015.
 
Bramo nijuavyo JF imejizuia kujinadi kwa mtindo unaotumiwa na mitandao mingine (ingawa siku hizi wamebadilika kidogo) ili tu kulinda uhuru wao katika kuhabarisha umma na mijadala uhuru... Kama wangelenga biashara kama lengo kuu tusingekuwa na JF huru kama hii ndio maana wanasisitiza michango zaidi kutoka kwa sisi wanachama wenyewe ili tulinde uhuru wetu wenyewe.....

JF huru italetwa na sisi members tu...
 
Internet ya kulipia ni shida . sasa hii ya bure ?????. Hii sasa sifa
 
Back
Top Bottom