Fahamu mambo mbalimbali kuhusu Kilimo cha Korosho

Nimevutiwa sana na kilimo cha korosho je mashamba ya kukodisha yanapatikana na gharama za kukodisha ziko vipi.
 
HABARI,
"Faza1980,

Unajua ule msemo unaosema kwenye miti hakuna wajenzi unaendana na haya mambo kwa kuwa tunaaridhi basi tunabweteka kuichezea kuna jamaa alisema hapa eti mita 12 kwa kila mti na mti nikashangaa sana wakati kwa heka ya mita 70 kwa 70 huwezi kupanda chini ya mikorosho 100 india wanapanda mpaka mikorosho 150-200 kwa heka na wanavuna wewe hujachelewa hakuna kuchelewa Duniani mpaka umeingia kaburini chukua maamuzi sasa tena maamuzi sahihi.

LUMUMBA
Asante sana.
 
Swali langu. Jee? Kwa Heka moja inatakiwa kitaalamu upande miche mingap? Na je, ukishapanda mikorosho ni ikawa mikubwa unaweza ukapanda mahindi yakakubali au mboga mboga. Au unaweza ukaotesha nyasi za mifugo ikakubali

HABARI,
"Come27,
Safi kwa swali zuri kwa kitaalamu idadi ya miti ya korosho kwa heka hakuna idadi kamili inategemea na mpango wako wa matumizi ya aridhi kama unataka kuchanganya mazao kama swali lako unaweza kupanda miti 50-80 kwa heka kama ni mpang wa korosho pekeyake mpaka miti 100-120 unaweza kama ukitumia mbegu za kisasa na unapopanda miti 120 baada ya miaka 10-15 unaweza kuanza kupunguza miti ikianza kubanana ila unakuwa tayari umesha anza kuvuna kwa muda.

Pia unaweza kabisa kupanda mahindi,mogamboga na nyasi za mifugo pia hakuna shida,KARIBU


LUMUMBA
 
Nimependa hapo uliposema

Duniani hakuna kuchelewa hadi unaingia kaburini..nami naongezea "utakachokifanya hapa duniani siyo lazima ukifaidi wanaweza kufaidi Hata wanao"


HABARI,
"Marire,
Asante hata wewe umeongea vema leo hii nchi nyingi zilizoendelea kama marekani wanatumia matunda ya waliotangulia ndio maana hata wao wanapambana kuweka sawa maisha ya wamarekani wa miaka 200 ijayo.

LUMUMBA
 
Hongera sana mkuu kwa kumpa taarifa sahihi na anwani sahihi, pia namshauri kabla hajaanza kulima afike ofisi ya kilimo katika halmashauri ambako shamba lake linapatikana ili iwe rahisi kupata huduma za kitaalamu wakishirikiana na hicho kitu cha utafiti. Nakumbuka mwaka jana zimetolewa miche kwa wakulima wa mikorosho bure, naamini akienda na wazo lake atapokelewa na kupata huduma yenye tija maana kaingia wakati mwafaka.


HABARI,
"daudthefarmer,
Kweli kabisa asante sana nashukuru,

LUMUMBA
 
Dodoma napo zinakubali saana hasa kongwa sehemu moja inatwa mkoka mashamba yapo kibao bei chee na yana rutuba balaa, wakenya ndio wanamwagika kuja kujichukulia mashamba kwa migongo ya wenyeji wakat sisi tumelala jaman. Mfano hizi picha hapa chini ni korosho za Dodoma ila sisi Watanzania jamani tuna shida saana.

IMG_20171118_151916#1.jpg
 

Attachments

  • IMG_20171118_145306#1.jpg
    IMG_20171118_145306#1.jpg
    199.4 KB · Views: 101
hata hiyo ya kisasa huja kukua huwa kama ya kizamani, njoo shambani kwangu uione, usione inazaa ikiwa na tawi moja ukadhani inaishia hapo.
Unalima sehemu gani mkuu? Nataka Mimi nije wakati wa musimu kwa ajili ya manunuz na kwa wakulima wengine VP nitaweza kununua sh ngp per kg?
 
Unalima sehemu gani mkuu? Nataka Mimi nije wakati wa musimu kwa ajili ya manunuz na kwa wakulima wengine VP nitaweza kununua sh ngp per kg?
Njoo Liwale pia. Korosho zinapatikana kwa wingi sana.
 
Mkuu Lumumba,

Nashukuru kwa uhamasishaji wako mzuri. Nania ya kuwekeza kwenye korosho kuanzia eka 30 mpaka 100 kwa lengo la kupanda kila mwaka sio chini ya eka 20 kama Mungu akinipa nguvu.

Naomba kujua mambo yafuatayo mkuu;

1. Wapi panafaa kwa uwekezaji huu kati ya Lindi na Mtwara (hapa tukiangalia upatikanaji wa ardhi ya kutosha kuweza kupanuka kwa urahisi, bei ya ardhi kwa eka ya mkoa husika, miundombinu n,k).
2. Gharama za kupanda zikoje mathalani kwa eka moja hii itanisaidia kutengeneza bajeti.
3. Changamoto kubwa ya zao hili ni zipi?
4. wastani wa mavuno kwa mti mmoja ni kilo ngapi?

Natanguliza shukrani zangu za dhati. Naamini majibu yako yatasaidia na wengine pia na hatimaye kuhamasika kuwekeza kwenye zao hili ambalo lina fursa lukuki.

Asante
 
Kaka lumumba samahani mikorosho 17 waweza pata gunia ngp

HABARI,
"rommy shabby,
Karibu sana mdau bila samahani,Kipimo kizuri cha mavuno ya korosho ni kilo si gunia kwani bei yake huanzia kilo tofauti na mahindi kwa gunia. Mikorosho 17 kwa ule wenye umri wa miaka 5-10 unaweza kupata kilo 10-20 au zaidi inategemea na matunzo na kwa kilo ya sasa 3000-4000.

LUMUMBA
 
Back
Top Bottom