Ufafanuz murua mkuu.HABARI,
"Revolution,
Kweli mbole ya samadi sehemu nyingi ni adimu hata za viwandani zinafaa kutumika hizo husaidia kukuza haraka ila ki uhalisia hata ukipanda bila mbolea hii miti inaota na utavuna kama kawaida ila tofauti ya Kutumia mbolea husaidia kukua kwa haraka.
LUMUMBA
Nashukuru sana mkuu Lumumba, nimepitia Uzi wote nauliza swali ambalo halijaulizwa, Je unaweza kumwagilia mikorosho labda kwa kutumia Sprinkler kila siku jioni kwaajili ya kuifanya ikue haraka haraka? Au unaweza shauri umwagiliaji kwa ratiba ipi? Case study ya shamba ambalo Lipo Lindi.
Ufafanuz murua mkuu.
Mimi Nina maswali kadhaa. Ushirika hukusanya korosho za wakulima,je.kuna malipo yoyote ya awali ambayo wakulima hulipwa? Au malipo pekee mpka mnada ufanyike ndo walipwe.. Pia gharama za usafirishaj wa korosho ghafi kutoka kwa mkulima mpka sehemu za kuhifadhi hugharamiwa na mkulima?
Naomba ufafanuz wako mkuu
Asante sana mkubwa kwa jitihada zako za kutuelimisha na kuhamasisha ukulima huu wa korosho,
Samahani nina swali ambalo lipo nje kidogo na mada yako ya leo,ni hivi kuna taarifa kuwa sababu ya korosho yetu kuwa na soko ni kwa kuwa inatoka msimu ambao duniani kote hawavuni...
Je ni habari za ukweli?ikiwa ni kweli vipi mikoa mingine ambayo ndo kwanza wanahamasishwa kulima?nao itatoka msimu mmoja na korosho za kusini?
Sawa.. Hiyo namna ya "kubebesha" inaweza kutumika kwa mimea mingine pia, au ni kwa mikorosho pekee?
Samahan mkuu. Ni zao gani jingine la biashara tofaut na korosho. Ambalo lina soko zuri kimataifaHABARI,
"BILGERT,
Unapokuwa kwenye ushirika huwa mara nyingi mpaka mnada ufanyike ndio mkulima analipwa ila mkulima ndio unatumia gharama zako kupeleka mazao yako kwenye ushirika,Ila kuna baadhi ya ushirika huwa wanakuwa na mkataba na mtu kusafirisha zao la washirika mnada ukifanyika mkulima anakatwa pesa ya usafiri kwa kilo au tani kutokana na ukubwa wa mavuno ya mkulima
LUMUMBA
Kwahiyo hii njia inasaidia kupunguza muda wa kusubiri mavuno bila shaka, kama ni hivo inamaana unaweza kuanza kupata korosho ndani ya mwaka mmoja?
HABARI,
Kwanza niwapongeze wadau wote mnaofatilia Kilimo cha korosho.
"Thesis, kimpupu, "Mshuza2,, SUKAH, Gu Jike , ankai, Shark , Mndengereko One ,Na wengine
Nime Post video 4 zinazoonyesha jinsi ya kubebesha miche ya mikorosho (grafting).Ukiangalia kwa vitendo inatosha,Kama una swali niulize.
LUMUMBA
Okey, hapo nimekuelewa. Sasa hivi wanahamasisha kilimo vha korosho huku Iringa ndo maana nataka nielewe vizuri ili nichangamkie fursa.HABARI,
"mnyikungu,
Ndio hii njia inapunguza muda wa kuanza kuvuna Ndani ya mwaka mmoja korosho zinatoka kwani unakwa ukpandikiza kikonyo kilichokuwa mwisho wa mti mama ambacho ni cha kutoa matunda ila sasa unashauriwa yale mau ya mwaka wa kwanza na wa pili uyatoe yasibebe matunda kwani mti unakuwa hauna nguvu bado na pia yanakuwa ni machache kwani mti unakuwa hauna matawi mengi ila unaweza kuanza kuvuna korosho chache kuanzia mwaka wa 3 ila muda unavyozidi kwenda ndio matawi yanaongezeka na mavuno yanaongezeka pia Tegemea kuanza mavuno baada ya miaka 3 ni muda mzuri.
Pia kuna mbegu za miaka 3 zipo pale Naliendele ila kwa hizi za kubebesha unakuwa na uhakia kwani mche utakuwa na tabia za ule mti mama uliotoa.
LUMUMBA
Shukrani sana Nimenunua ekari tano kwa kuanzia na sasa shamba Lipo kwenye kusafishwa maana nilinunua pori nimehamasika baada ya kutangazwa kuuzwa Elfu hamsini naishi Dar es salaam, sina utaalamu sana kuhusu msimu sahihi wa kupanda zao la korosho japo, pia nimefikiria kutumia miche iliyobebbeshwa ambayo naambiwa inapatikana Naliendele kwa bei ya sh 1000, Je kwa mwezi wa tatu ni msimu wa Kawaida kupanda zao Hilo? Na Je kuja eneo Karibu Hapo lindi mjini naweza kupata mbegu zilizobebeshwa? Na pia Je naweza pata wapi shamba Darasa nikajifunze zaidi kwa maeneo Karibu na Dar au hata huko lindi? Na pia niepuke makosa gani kabla sijaanza utekelezaji wa mradi huu? Shukrani sana kwa utayari wako mkuu PatriceLumumba
Samahan mkuu. Ni zao gani jingine la biashara tofaut na korosho. Ambalo lina soko zuri kimataifa
Shukrani mkuu.HABARI,
"BILGERT,
Safi kwa swali zuri mazao yenye soko zuri kimataifa ni mengi sana, Muhogo, Parachichi, Tangawizi nitatuma list yake kesho pamoja na masoko yake. Tatizo tulilokuwa nalo ni kwamba wengi wanaosafirisha kwenda nje sio wazawa wengi ni wahindi sasa wanakuwa na uchaguzi sana kwenye mazao yenye faidi kubwa kama korosho. Ila kwa sasa soko la parachichi nalo limeanza kuwa kubwa hasa kwa nchi za Ulaya Ujerumani, Spain, Uingereza, Uholanzi .nk.ndio maana kilimo chake kimeanza kuwa kikubwa sana Iringa.
Kwa muhogo unga wake unahitajika sana China kwa wingi sana ila bado watu hawajaweka mkazo huko na shida bado hawana mtu wa kuwahakikishia soko nikimaanisha kununua.
Tangawizi India na china pia wanahitai sana.
LUMUMBA
Okey, hapo nimekuelewa. Sasa hivi wanahamasisha kilimo vha korosho huku Iringa ndo maana nataka nielewe vizuri ili nichangamkie fulsa