Fahamu mambo mbalimbali kuhusu Kilimo cha Korosho

Umbali kati ya Shimo na Shimo ni 12M .Eka moja wastani miti 30

HABARI,

"mahavanga,

Hujakosea kwa kipimo chako hicho nakubaliana na wewe kabisa hata ukitaka miti 20 kwa heka inawezekana ,Kama umefatilia post zangu zote nilieleza vema, Kama mkulima anafanya kilimo cha mchanganyiko na mazao mengine kama mahindi,mtama,ufuta alizeti n.k ni sawa ila kama ni zao la korosho tu ni matumizi mabaya sana ya aridhi sana mita 12 duh.

Ndugu mikorosho ya kubebeshwa na ya kisasa huwa haitanuki sana nitatuna picha moja kutoka mahali mkorosho wa miaka 10 haujazidi mita 3 upana kwa kila upande na kila mwaka wanavuna zaidi ya kilo 20 kwa mti mmoja hapo ndani ya mita 12 zako umeacha mikorosho miwili inayoweza kupandwa.

Hapo kati na bado ungeweza kupanda mazao mafupi kama maharage N.K. Unaweza kupanda idadi kubwa ya miti kwenye heka moja baada ya mika 10 na kuendelea inapozidi kubanana ndipo unapunguza mmoja mmoja ila tayari mti unakuwa umeshakupa mavuno kwa zaidi ya miaka 10 haingii akilini uwache eneo wazi kusubiri miaka 20 ibanane Duh Tusipende kukariri lazima tujiongeze tufate maelekezo ya pembejeo ila kuna mambo mengine lazima kujiongeza, India kati ya nchi zinazoongoza kwenye kilimo hicho kwa heka moja wanapanda mpaka miti 150-200 sasa wewe ndugu ukisema miti 30 Tusibweteke na aridhi tuliyokuwanayo tuangalie kuwekeza sehemu ndogo unavuna kikubwa. TEKNOLOGIA. TECHNOLOGY

LUMUMBA
 
Waweza kuniunganisha hapo ulipo nunua namimi nikanunue?
 


HABARI,
senyaba,
Karibu niwie radhi kwa kuchelewa kukujibu majukumu yalibana.Hongera kwa kwa uamuzi uliochukuwa huo ni uwekezai mkubwa sana na nimefurahi uliposema kwa kuanzia kwa hiyo una mipango ya zaidi ya heka 300 hongera.Tanga ni kati ya maeneo ya kwanza kabisa kwa ulimaji wa korosho kwa ujumla pwani yote ya bahari ya Hindi kuanzia Mtwara mpaka Tanga korosho inakubali kwenye hilo usiwe na wasiwasi na kuhusu wanunuzi hilo nalo halina shida kuna vikundi vingi vya ushiriki wewe utachagua kikundi cha kujiunga na wanunuzi ni wale tu watakaopitishwa na Serikali Nenda ofisi za mkuu wa mkoa wana taarifa zote pale.Kwa upande wa risk kweli zipo hakuna kitu kisicho na risk mojawapo ni kununua mbegu kwenye vyanzo visivyo thibitishwa hili unaweza kukuza mti usio na ubora tafuta vyanzo vizuri vya mbegu.

LUMUMBA
 

Lumumba nakuelewa sana aise! Naandaa maswali yangu 12 yakuuliza kesho! Naamini utanipa majibu yenye ujazo

Ubarikiwe sana aise.
 
Asante Lumumba, kila mtu niliekuwa namconsult alinipa hesabu ya miche 28 hadi 30 kwa ekari, hadi nikapata shamba la ekari 4 hapo mtwara nikapiga hesabu zangu nikaona ni dogo sana kwani nitavuna kiasi kidogo cha korosho.

Ningekuwa nimepata majibu kama haya na maelezo yaliyoshiba i would have decided otherwise. Nimeshangaa kuona inaweza kufika miche zaidi ya 3000 kwenye hizo ekari kumbe kwa maelezo niliyokuwa nayo mwanzo hapo hata miche 1000 haingeingia shambani.

Asante sana
 
Ndugu PatriceLumumba juzi waligawa miche nimepata miche ya kutosha shamba langu la ekari 5 miche 150 hii inayogawiwa huko lindi, swali ni je niipande hiyo hiyo au nitafute hii ya kubebeshwa? Mawazo yangu yananiambia kama nipande miche hiyo hiyo halafu niandae kitalu changu nibebeshe mwenyewe halafu nipande katikati ya hii ambayo inatangulia ili ku-Maximize profit niweze kuingiza mpaka miche angalau 80 kwa kila ekari je nakuwa nipo sahihi? naona kama msimu huu nikingojea ya kubebeshwa naweza chelewesha malengo hasa ukizingatia gharama kuinunua nataka kuminimize cost kwa kuiotesha mwenyewe na kuibebesha mwenyewe somo kwenye videos zako limenikaa vyema,

Pia ninaswali kuhusu mbolea ya kupandia kuna mtu ameshauri hii miche tupandie samadi, au mboji ila kwa vile upatikanaji wake kwa lindi ni mgumu ameshauri tutumie mbolea ya kiwandani? swali je unashauri mbolea gani na kwa vipimo vipi kwa kila mche?
nitashukuru kwa maelezo yako samahani maswali mengine yanaweza kuwa tayari yamejibiwa but it's a matter of choice, ila nilitaka ur opinion, ili nitekeleze kwangu kupitia opinions zako.
 
Lumumba nakuelewa sana aise! Naandaa maswali yangu 12 yakuuliza kesho! Naamini utanipa majibu yenye ujazo

Ubarikiwe sana aise..

HABARI,
"fungafunga,
Karibu sana na maswali yako Mkuu najua mwenyezi mungu ataniongoza nikupe majibu kwa maswali yote.
Karibu "fungafunga.

LUMUMBA
 

HABARI,
"Faza1980,
Unajua ule msemo unaosema kwenye miti hakuna wajenzi unaendana na haya mambo kwa kuwa tunaaridhi basi tunabweteka kuichezea kuna jamaa alisema hapa eti mita 12 kwa kila mti na mti nikashangaa sana wakati kwa heka ya mita 70 kwa 70 huwezi kupanda chini ya mikorosho 100 india wanapanda mpaka mikorosho 150-200 kwa heka na wanavuna wewe hujachelewa hakuna kuchelewa Duniani mpaka umeingia kaburini chukua maamuzi sasa tena maamuzi sahihi.

LUMUMBA
 
Duh aisee mkuu, umeona mbali sana
 
Swali langu. Je, kwa Heka moja inatakiwa kitaalamu upande miche mingap? Na je, ukishapanda mikorosho ni ikawa mikubwa unaweza ukapanda mahindi yakakubali au mboga mboga. Au unaweza ukaotesha nyasi za mifugo ikakubali.
 

Habari ya leo mkuu,

Hongera sana kwa kuwa na ardhi ya ukubwa huo.

Napenda kukuongezea ujuzi wa faida kidogo juu ya matumizi bora ya ardhi kuhusu kilimo mseto, iko hivi kipindi unasubiri mikorosho yako ya kisasa(hybride) ianze kutoa matunda ili upate faida takribani miaka 3-5 jaribu kupanda mahindi kwa kipindi cha misimu miwili ya mwanzo kwa hilo eneo lako ili lisipotee bure na hii itapelekea kupata faida ya zao moja under zero cost of production.

(a) gharama za uzalishaji
- Kulima ni bure kumbuka umelima kwa ajili ya korosho.
- Mbegu ni mifuko 128 kila ekari ni mifuko 4 na kila mfuko ni 12,000/=(1,536,000/=)
- Kupanda ekari moja maeneo mengi ni 30,000/=(960,000/=)
- Palizi hapa ni ile itakayotumika kupalilia mikorosho(bure)
- Siijaweka mbolea kwa sababu shamba kama ulivosema ni virgin.

Jumla ya gharama za uzalishaji/matumizi upande wa mahindi itakuwa ni Tshs 2,496,000/=

(b) mapato
Ekari moja inatoa wastani wa gunia 8-10 chini ya uangalizi mzuri kwa mtu aliezamilia kama wewe,
Hivyo basi utapata magunia 256 kwa ekari 32.

Mapato/mauzo kwa sasa ni 60,000/= kwa gunia (15,360,000/=)

Utakuwa na faida ya 12,864,000/= kumbuka hii umelima msimu mmoja tu na nimesema ulime misimu miwili ya wawli maana mikorosho inakuwa bado ni michanga na itakuwa ni sehemu ya ulinzi wa shamba kwa mifugo na watu wanaokuzunguka hivyo. 12,864,000/=x misimu 2 (25,728,000/=).

Nakutakia kazi njema mkuu kwa haya maamuzi yako mazuri.
 


Habari ya leo mkuu...!
Hongera sana kwa kuwa na ardhi ya ukubwa huo.

napenda kukuongezea ujuzi wa faida kidogo juu ya matumizi bora ya ardhi kuhusu kilimo mseto, iko hivi kipindi unasubiri mikorosho yako ya kisasa(hybride) ianze kutoa matunda ili upate faida takribani miaka 3-5 jaribu kupanda mahindi kwa kipindi cha misimu miwili ya mwanzo kwa hilo eneo lako ili lisipotee bure na hii itapelekea kupata faida ya zao moja under zero cost of production.

(a) gharama za uzalishaji
-kulima ni bure kumbuka umelima kwa ajili ya korosho.
-mbegu ni mifuko 128 kila ekari ni mifuko 4 na kila mfuko ni 12,000/=(1,536,000/=)
-kupanda ekari moja maeneo mengi ni 30,000/=(960,000/=)
-palizi hapa ni ile itakayotumika kupalilia mikorosho(bure)
-sijaweka mbolea kwa sababu shamba kama ulivosema ni virgin.
Jumla ya gharama za uzalishaji/matumizi upande wa mahindi itakuwa ni Tshs 2,496,000/=

(b) mapato.
Ekari moja inatoa wastani wa gunia 8-10 chini ya uangalizi mzuri kwa mtu aliezamilia kama wewe,
Hivyo basi utapata magunia 256 kwa ekari 32.

mapato/mauzo kwa sasa ni 60,000/= kwa gunia (15,360,000/=)

utakuwa na faida ya 12,864,000/= kumbuka hii umelima msimu mmoja tu na nimesema ulime misimu miwili ya wawli maana mikorosho inakuwa bado ni michanga na itakuwa ni sehemu ya ulinzi wa shamba kwa mifugo na watu wanaokuzunguka hivyo. 12,864,000/=x misimu 2 (25,728,000/=).

Nakutakia kazi njema mkuu kwa haya maamuzi yako mazuri.
 


Hongera sana mkuu kwa kumpa taarifa sahihi na anwani sahihi, pia namshauri kabla hajaanza kulima afike ofisi ya kilimo katika halmashauri ambako shamba lake linapatikana ili iwe rahisi kupata huduma za kitaalamu wakishirikiana na hicho kitu cha utafiti. Nakumbuka mwaka jana zimetolewa miche kwa wakulima wa mikorosho bure, naamini akienda na wazo lake atapokelewa na kupata huduma yenye tija maana kaingia wakati mwafaka.
 

Hivi, how long does it take kuanza kuvuna tangu upande miti ya mikorosho.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…