Fahamu kwanini mbwa hatumiwi na wachawi

Fahamu kwanini mbwa hatumiwi na wachawi

mbwaa anao uwezo wa kuona msiba katika mtaa usika ndan ya week mbili hadi mwezi mbele kwa kutoa mlio huu kwa mda wa dk kadhaa mlio huo ni huu hapa jaribu kukamata melod nadhan unaujua kishavufanye utafit uuuuuuuuuuooowh uuuuuuuuooooouuuuhw uuuuuuuuuuhw nilijchunguza hii tokea nikiwa mdogo nomethibitisha ni kweli bibi yangu ndio alirnieleza hii kitu nikaifanyia tafit
Dah mkuu appoh
 
Mkuu mngewachunguza vizuri waliowapa hii teknolojia huenda wakawa walikuwa wahusika wa michezo yote na hivyo walikuwa wanawaandaa kisaikolojia.
NB..msini 'quote' vibaya.
Umenena hasa
 
Kati ya viumbe vilivyopewa uwezo Wa kuona majini na mashetan ni
_Jogoo
_Mbwa
_Punda
 
Kuna ukweli kwa hili maana huku kwetu Kuna siku mbwa wanabweka mji mzima na ukitoka nje huoni kitu lkn mbwa atabweka hata masaa 3
 
Enyi wadau!
KWANINI PAKA HUTUMIKA

katika viumbe vya kufugwa na mwanadam,Paka hawezi muona mchawi, ni kipofu kabisa, ndo maana anatumwa, Paka ameonekana kuwa kiumbe kinachotumiwa sana na wachawi na washirikina hii ni kwasababu Paka ana kichwa chepesi, anaelewa haraka na kukariri, paka anaweza tumwa chochote nyumbani kwako, paka anaweza kuja kukuchunguza maisha yako kichawi, mtakubaliana na mimi inaweza ukawa umejifungia ndani au umeleta kitu kwa siri ndani kwako ila utashangaa kibibi kichawi kinakwambia naona umenunua kitu fulani mjukuu wangu. sasa ndo ujiulize kimejuaje wakati kinakaa mtaa wa pili na wewe umeleta kwa siri? paka anao uwezo wa kukamata vitu kwa haraka,wengine watumwao ni ndege njiwa na bundi maana hawaoni uchawi.
MBWA JE YUKOJE?
kwa mbwa ni kinyume kidogo, mbwa anaona wachawi, anauwezo mkubwa sana wakuona uchawi, anakichwa kizito, hawezi tumwa na wachawi maana ataharibu kabisa kwakuwa anaona wachawi wengine, mbwa hafai, wengine hadi humwita mbwa ni najisi, hili ni kwasababu mbwa havumilii kuona majini au wachawi wanakatiza lazima atabweka! mbwa ameonekana kufaa katika ulinzi kwasababu anaona usiku wezi na wachawi. ukiona mbwa anabweka sana usiku nyumbani kwako usipuuzie chunguza lazima utakuta kuna tatizo.wengine wenye uwezo wa kuona ni KUKU na BATA ...hao wanaouwezo wa kumwona mchawi...hakikisha unawatumia wanyama wako kukurinda kwa kusikiliza milio yao.
Asante mkuu
 
Oooho kumbe ndiyo maana yule bibi wa pale chini hapendi wajukuu zake wafuge mbwa..... katakuwa kachawi kale kabibi kudadeki...
 
Mbwa wangu wawili kuamkia juzi Mnamo majirani ya saa saba hivi usiku walibweka sana wakielekea kwenye geti kubwa la nyumba yangu, nilipowachungulia dirishani niliwaona wapo busy wakiendelea kubweka wakitamani geti lifunguliwe ili watoke nje wakapambane na kitu. ..! Asub. kulipokucha nilikwenda fungua geti ili kutazama kulikoni? Nilichokikuta na kukiona kilinifanya niamini kuwa mbwa ni walinzi wazuri sana kwetu binadamu. ..!! Nilikuta dawa nyeusi imemwagwa nje ya geti. ..!! Nilirudi ndani nikachukua maji ya baraka nikaenda kukemea zile dawa.
 
Duh kumbe.saivi nikiskia wanabweka tu natoka na maji ya baraka namwaga kila upande.nikimdaka mchawi namzibua vibao vya kutosha
 
Duh kumbe.saivi nikiskia wanabweka tu natoka na maji ya baraka namwaga kila upande.nikimdaka mchawi namzibua vibao vya kutosha
Mbwa wana akili sana mkuu, kadri unavyowatunza vizuri ndivyo wanavyozidi kuwajibika. ...na ukiwasikia wanabweka wewe toka nje haraka hapo utakuwa unazidi kuwahamasisha kuwa kila wanapoona tukio baya usiku lazima wabweke ili wewe utoke.
 
mbwaa anao uwezo wa kuona msiba katika mtaa usika ndan ya week mbili hadi mwezi mbele kwa kutoa mlio huu kwa mda wa dk kadhaa mlio huo ni huu hapa jaribu kukamata melod nadhan unaujua kishavufanye utafit uuuuuuuuuuooowh uuuuuuuuooooouuuuhw uuuuuuuuuuhw nilijchunguza hii tokea nikiwa mdogo nomethibitisha ni kweli bibi yangu ndio alirnieleza hii kitu nikaifanyia tafit

We utakua mchawi tu,
 
Back
Top Bottom