Fahamu kuhusu " Deep State " ilivyo na inavyofanya kazi

Upepo wa Pesa

Upepo wa Pesa

JF-Expert Member
Joined
Aug 8, 2015
Messages
12,951
Points
2,000
Upepo wa Pesa

Upepo wa Pesa

JF-Expert Member
Joined Aug 8, 2015
12,951 2,000
Deep state huweza kutikisa nchi kwa kuhujumu uongozi ulio madarakani kama ikidhihirika walikosea katika kumpitisha kiongozi husika au wakipoteza nguzo inayowalinda ambayo ni uhai wa taifa. Nchini Tanzania kundi la “deep state” halizidi watu 50 katika wakati wowote.
Najaribu kuunda doti.
 
Kilele9

Kilele9

JF-Expert Member
Joined
Jun 1, 2017
Messages
769
Points
1,000
Kilele9

Kilele9

JF-Expert Member
Joined Jun 1, 2017
769 1,000
Kudhihiridha uwepo wa deep state, Trump atakuwa Rais wa awamu moja tu.
Kama unamsema wa kwetu kwa mafumbo umekosea. Atafanya awamu mbili na afya ikimruhusu tutamuongezea ya tatu.
 
K

komamgo

JF-Expert Member
Joined
Sep 14, 2012
Messages
1,347
Points
2,000
K

komamgo

JF-Expert Member
Joined Sep 14, 2012
1,347 2,000
Deep State kwa tafsiri isiyo rasmi ni “Waundaji na Waendeleza Taifa”. Tanzania neno “System” (Mfumo) huwa linatumiwa sana kumaanisha deep state lakini kiuhalisia deep state sio system. System ni mojawapo ya zao dogo tu la deep state na inaweza kusambaratishwa wakati wowote.

Deep State ni kundi lisilo rasmi la kiintelijensia ambalo hujumuisha makundi mbalimbali. Hujumuisha baadhi ya watu waliopo katika utumishi na wastaafu na hata marehemu (maandishi yao) katika intelijensia ya jeshi, usalama wa taifa na hawa huja pamoja si kwa kuambiwa au kuelekezwa bali kwa yale ambayo wao wanayaamini kimapokeo kuwa ni misingi ya uhai wa taifa.

Watu hawa huamua nani awe mgombea Urais kwa mfano, nani awe Makamu wake, nani awe Waziri Mkuu, nani awe tajiri mkubwa (kwa nchi nyingi za Afrika kwa mfano matajiri wengi wamefanikiwa kwa kupitia kazi za miradi ya umma) kadhalika. Maamuzi haya hayafanywi usiku mmoja, wakati mwingine huchukua miaka wakitumia njia zote zinazowezekana kuhakikisha nani anafikia nafasi ya juu kabisa ya uongozi wa nchi au sehemu fulani nyeti na nani hafiki.

Wakiamua wewe hutakaa uwe Rais wa nchi kwa mfano, huwezi kuwa. Huwa hawana upendeleo, wana roho ngumu, maamuzi magumu, hakuna anayemzidi mwingine kwa uzito na umuhimu wa maoni na hutazama mustakabali wa nchi kwa miaka mingi mbele, tofauti na wanasiasa ambao wao hutaka tu kushinda chaguzi. Ifahamike kuwa inawezekana hata Rais aliye madarakani asifahamu kwa hakika watu hao wote kwa ujumla wao. Hii hutokea hasa katika nchi zinazofanya chaguzi kila baada ya miaka michache.

Waasisi wengi wa mataifa huwa ni sehemu ya deep state mfano Mwalimu Nyerere ambaye maandiko yake ndicho chanzo cha Waziri Kiongozi wa zamani wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad kufungwa gerezani na hadi leo kuendelea kuota ndoto za kuwa Rais wa Zanzibar ambazo huenda anakwenda nazo kaburini. Deep state huwa ni kama jini, wakati mwingine unaweza kusema halipo ni maneno tu.

Deep state huweza kutikisa nchi kwa kuhujumu uongozi ulio madarakani kama ikidhihirika walikosea katika kumpitisha kiongozi husika au wakipoteza nguzo inayowalinda ambayo ni uhai wa taifa. Nchini Tanzania kundi la “deep state” halizidi watu 50 katika wakati wowote.

Itaendelea...
Very interesting
 
mjumbe wa bwana

mjumbe wa bwana

JF-Expert Member
Joined
Sep 19, 2016
Messages
3,595
Points
2,000
mjumbe wa bwana

mjumbe wa bwana

JF-Expert Member
Joined Sep 19, 2016
3,595 2,000
Duh au ndio walipanga 2020 kusiwe na upinzani
 
Niccolo Machiavelli

Niccolo Machiavelli

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2017
Messages
1,428
Points
2,000
Niccolo Machiavelli

Niccolo Machiavelli

JF-Expert Member
Joined Feb 7, 2017
1,428 2,000
Balali/deep-state-nchini-tanzania-1290dec9a064View attachment 1101563View attachment 1101564
Hahahah.....hapo kwenye “itaendelea” nadhan anamsikilizia Balali kama naye atapost tena!
 
Chakwale

Chakwale

JF-Expert Member
Joined
May 17, 2015
Messages
804
Points
1,000
Chakwale

Chakwale

JF-Expert Member
Joined May 17, 2015
804 1,000
Muendelezo uko wapi Mkuu??

Mungu Ibariki Tanzania
Mungu Ibariki Chakwale
Mungu Ibariki Morogoro
 

Forum statistics

Threads 1,336,217
Members 512,562
Posts 32,531,042
Top