Burkinabe
JF-Expert Member
- Feb 12, 2023
- 1,893
- 3,200
Kuna hii kitu inaitwa "Deep State", ambayo inadaiwa iko kila nchi duniani.
Baadhi huamini kwamba "Deep State" ipo kwa ajili ya maslahi mapana ya nchi na wananchi walio wengi.
Lakini binafsi naamini kwamba "Deep State" iko kwa ajili ya kulinda maslahi ya watu wachache tu wakiwamo wao.
Hii inathibitishwa na ukweli kuwa, viongozi wengi na wanaharakati ambao husimamia maslahi ya nchi zao na kuwatetea wanyonge, huwa hawachukui muda mrefu wanaondolewa au wanaondoka katika mazingira ya kutatanisha! Na mara nyingi ukifuatilia kwa undani, kuondoka kwao kunahusishwa na hao "Deep State".
Hivyo, inakatisha tamaa sana kuona chombo ambacho kilipaswa kuwa cha kupigania maslahi ya nchi na wananchi walio wengi, kinakuwa cha kulinda, kutetea na kupigania maslahi ya kikundi au vikundi vya watu wachache ambao mara nyingi huwa wabadhilifu na mafisadi wa mali za Umma.
Deep State, kama mpo kweli, mtangulize maslahi ya nchi zenu badala ya kuhangaika na viongozi wanaotetea maslahi ya wananchi wanyonge ili na wao angalau waishi maisha mazuri na kufaidi keki ya Taifa lao.