Fahamu kuhusu biashara ya kuuza chakula (Mgahawa)

Sawa ila utafanyaje peke yako? Lazima usaidiwe, pia usipotoke waaminifu bado wapo
Baada ya mwaka naomba uje utuletee mrejesho hapa. Tunaosema hivi tumefanya hizi biashara na watu ambao tulijua ni waaminifu na mwisho wa siku tukaangukia pua. Kama mwaminifu sana atakula faida na mtaji utaukuta ila biashara haitakua. Hiv unafikiri huyo binti yeye hana ndoto ya kuwa na biashara yake kama wewe? Unafikiri yeye hataki kuwa bosi kama wewe?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kasema huyo dada anajua yeye atamsimamia swali atamsimamiaje na yeye yuko kazini? mama ntilie tena mpya raha uwepo mwenyewe au da rebecca unaonaje?mimi naona kodi ya miezi 3 ikiisha wanafunga biashara hawa.
Sema sijajua mazingira ya huko kwenu na ukubwa wa chumba ila kodi pia naona kama ipo juu ukiangalia na mtaji mzima ulivyo. Kama angekuwa na vitu vingne kama majiko, masufuri, friji nk na hiyo hela aliyosema iwe kwa kununua vitu vya kupika tu ingekuwa sawa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ntamwachia ntapitia hesabu coz mda mwingi ntakua kibaruani

Ungekuwa unasababisha mwenyewe ningekuwa mteja wako wa kila siku hata kama natokea mbali huku Kinyerezi, ningetia maguu tu ali mradi nikuungishe wewe.
 
Amina ushauri was busara sana dadaangu huna longolongo wala roho ya kwanini cha msingi nipate faida, hela ya kodi, mishahara nikishatoa maninuzi nipate


kibarua ndo kimenipa mtaji so kibarua ni muhim kuliko biashara, watafanya nawaamini
Hahahahaha hili ndio tatizo la waajiriwa. Kibarua ni muhimu kuliko biashara yako ningekuwa mm nisinge andika kitu kama hiki. Labda tu nisema hiki ndio kinachofanya watumishi wengi washindwe kuwa na biashara zilizofanikiwa kwani hata usipouza unajua hautalala njaa si mshahara upo sasa ya nn uhangaike kubembeleza wateja. Hivi unafikiri Mengi angeajiriwa na wakat huo huo ameanzisha IPP media yake had leo ingekuwepo?

Pia umesema wewe umeanzisha hiyo biashara kutokana na ushawishi wa huyo msichana wako that means ni wazo lake ila mtaji wako sasa tarajia akipata mtaji wake kupitia mtaji wako atakuacha na mtaji wako ukiwa ule ule au umepungua. Pia nikisoma comments zako between lines sioni kama upo serious.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ndo Ttaizo kubwa sana. Yaani hatuamini mawazo yetu ila ya watu wengine
 
Well informed

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hakika nasadiki

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tatizo dada hataki kuukumbatia huu ukweli

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hongera sana kwa wazo hili na kila la kheri.

Umefanya vizuri kuuliza hapa.Sijawahi kufanya biashara hii ila jitahidi kuwa mbunifu katika huduma na kuwajali watu wote kwa usawa.Jitahidi uwe na mtazamo wako kichwani wa namna unavyopenda biashara yako iwe halafu usimamie utekelezaji wake (Usiiache iende tuu ilimaradi). Jitahidi kujitathmini au kuitathmini maendeleo yake kila wiki (au kila wiki 2) na kufanya maboresho pale inapobidi.
 
Hapo ndo umeongea khs graph bt swala la wizi kama wanavyosema wengine weka kando, nashukuru ntamuelimisha khs hilo la graph
Dada yangu mimi nilikuwa nakuomba uyapokee maoni ya wadau wanaochangia, hata kama yatakuwa yanapingana na maoni yako " kwa sababu humu kuna watu mbali mbali ambao wanauzoefu mkubwa kwenye biashara mbali mbali na wengine pia ni wateja wa biashara hizo

So kwa namna moja maoni yao yana gusa sekta unayoizungumzia kwa sababu wana experience na sekta hizo ", bila shaka naimani moja ya malengo ya biashara yako nikuona inakua kubwa.. leo umeamua kuanza na huyo mfanyakazi mmoja kwa sababu biashara ndio inaanza so demanding yake ni low ..

. ila itakapo tokea ikakua utalazimika kuongeza wafanyakazi ---- huyu mfanyakazi wa pili huwenda akawa na tabia mbaya ambayo inaweza kumuambukiza mfanyakazi wa awali "

So maoni yangu ni kwamba'---- hiki unachoshauriwa leo sio Yote yanawez kutokea katika wakati uliopo sasa .mengine huwenda yakajiri katika wakati ujao baadae " so jitahidi kuhifadhi Hizi shauri mbali mbali unazo pewa kwaajili ya ustawi wa biashara yako na maisha yako kwa ujumla

I'm done

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hahaa dadeki ... watu kweli mnajua kutumia fursa " Mimi nilidhani gazeti lote hilo linahusiana na ushauri wa mama ntilie !!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kazi kweli kweli "--- dada ameomba ushauri huku Akiwa na majibu yake tayari mfukoni ... hahaa Jf bwana

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…