Fahamu kuhusu biashara ya kuuza chakula (Mgahawa)

Wangari Maathai

JF-Expert Member
Aug 13, 2018
35,078
2,000
Hahahahaha hili ndio tatizo la waajiriwa. Kibarua ni muhimu kuliko biashara yako ningekuwa mm nisinge andika kitu kama hiki. Labda tu nisema hiki ndio kinachofanya watumishi wengi washindwe kuwa na biashara zilizofanikiwa kwani hata usipouza unajua hautalala njaa si mshahara upo sasa ya nn uhangaike kubembeleza wateja. Hivi unafikiri Mengi angeajiriwa na wakat huo huo ameanzisha IPP media yake had leo ingekuwepo?

Pia umesema wewe umeanzisha hiyo biashara kutokana na ushawishi wa huyo msichana wako that means ni wazo lake ila mtaji wako sasa tarajia akipata mtaji wake kupitia mtaji wako atakuacha na mtaji wako ukiwa ule ule au umepungua. Pia nikisoma comments zako between lines sioni kama upo serious.

Sent using Jamii Forums mobile app

Una jicho kama langu..!andika tu unaoba huyu hana commitment kbs
 
Extrovert

JF-Expert Member
Feb 29, 2016
39,773
2,000
Yeye ndo sababu ya Mimi kutafuta fremu coz namuamini na ni reliable nlikaa nae sana namfaham A to Z esp uchapakazi na uaminifu ni ngumu sana kumuamini mtu nsiemfaham pia reliability ina matter sio Leo umefungua kesho haji umefunga mimi masuala ya kupika sijui mzee au inakuaje hapo nishauri vinginevyo naweza sema ndio kama sio yeye nsingepanga kufungua fremu,Ila nna imani ntakavyokua nafanya nae biashara ntawagundua wengine wachapakazi na waaminifu. So kwa sasa yes yeye ndio chanzo mpaka nimetafuta fremu ni bora nianze naye, ndio nimepewa ushauri humu bt siwezi sema niache kazi nimsimamie mtu nsiemfaham ntakua naruka mkojo nakanyaga mavi
Kwahiyo wewe ni mwanamke usiyejua kufanya lolote jikoni zaidi ya kuchemsha chai na maji ya kuoga ama? Hujaolewa bado?
 
Extrovert

JF-Expert Member
Feb 29, 2016
39,773
2,000
so ww huwez kushika usukani kbs umeamua kumuamini zaidi huyo
Huyu mshamba wa biashara, na hii business yenyewe kaamua kuianzisha kwa mhemko tu ila hana passion nayo thats why anategemea mwenzake amenyeke kumuendeshea biashara kwa faida kwa vile ni mtu experienced, anamuamini ama rafiki yake sana sijui blah blah. Hakunaga mtu anafanyaga biashara ya mtu baki kwa moyo, hata huko kazini watu wanapoenda kuna muda wanaspend kuchat na kupiga story bila kujali kwamba wanalipwa mshahara, badala ya kufanya kazi kwa bidii ili wamchangie CEO aongeze nyumba na magari zaidi hapa mjini!

Biashara ina stage 4 (introduction,growth,maturity na decline stage). Inatakiwa kusimamiwa kwa uchungu mpaka pale itakapofikia maturity stage. Kuanzia hapo una struggle kuhakikisha unafanya maboresho kila uchao ili graph isiporomoke kwenda decline, ukiskia matajiri hawalali vizuri hiko ndio kinawatesaga sana.

Sasa huyu mwenzetu yeye biashara hana uzoefu nayo ila ni mjuaji. Cha kufanya mwacheni hio 1m ikiteketea bila maelezo ya kueleweka atatia akili vizuri na huo ushoga wao ndipo utakapokufa.
 
😂😂😂Umeongea kwa machungu sana. Kifupi umewakilisha mawazo yangu. Tufanye mengine
 
DIVIDEND

JF-Expert Member
Jan 15, 2017
1,897
2,000
Haimaanishi sitapatembelea kabisa ntakua naenda weekend tena jumamosi tu inatosha kbs comments nyingine atapokea yeye
Hu hu hu hu hu biashara ya usimamizi wa simu. Basi kuwa mfanyakazi wa sehemu km hii raha sana, hata ukiniambia utanilipa elfu 10 kwa mwezi.
 
DIVIDEND

JF-Expert Member
Jan 15, 2017
1,897
2,000
Huyu mshamba wa biashara, na hii business yenyewe kaamua kuianzisha kwa mhemko tu ila hana passion nayo thats why anategemea mwenzake amenyeke kumuendeshea biashara kwa faida kwa vile ni mtu experienced, anamuamini ama rafiki yake sana sijui blah blah. Hakunaga mtu anafanyaga biashara ya mtu baki kwa moyo, hata huko kazini watu wanapoenda kuna muda wanaspend kuchat na kupiga story bila kujali kwamba wanalipwa mshahara, badala ya kufanya kazi kwa bidii ili wamchangie CEO aongeze nyumba na magari zaidi hapa mjini!

Biashara ina stage 4 (introduction,growth,maturity na decline stage). Inatakiwa kusimamiwa kwa uchungu mpaka pale itakapofikia maturity stage. Kuanzia hapo una struggle kuhakikisha unafanya maboresho kila uchao ili graph isiporomoke kwenda decline, ukiskia matajiri hawalali vizuri hiko ndio kinawatesaga sana.

Sasa huyu mwenzetu yeye biashara hana uzoefu nayo ila ni mjuaji. Cha kufanya mwacheni hio 1m ikiteketea bila maelezo ya kueleweka atatia akili vizuri na huo ushoga wao ndipo utakapokufa.
Achana na maturity huko mbali, kwenye introduction penyewe ndio panapoamua uelekeo wa biashara. Ndio maana unaona kuna biashara zinakufa zikiwa na miezi michache tu. Sasa huyu introduction hataki kupasimamia maturity huko atafika.
 
Extrovert

JF-Expert Member
Feb 29, 2016
39,773
2,000
Achana na maturity huko mbali, kwenye introduction penyewe ndio panapoamua uelekeo wa biashara.
Ndio maana unaona kuna biashara zinakufa zikiwa na miezi michache tu.
Sasa huyu introduction hataki kupasimamia, maturity huko atafika
Ndio maana nikasema ni katika hatua ambazo inabidi mtu akaze sana. Yani introduction, growth hadi kufikia maturity. Akichemka hapo tu hio biashara haita survive!
 
ommy15

JF-Expert Member
Jan 23, 2011
642
1,000
Baada ya miez sita yaani mwezi wa nane tutarudi hapa kupata mrejesho. Ila kwa uzoefu wangu hauwezi panda farasi wawil kwa wakati mmoja i.e hauwez kuajiriwa na kujiajiri na ukafanikiwa kote. Utatakiwa utoroke kazin uende kwenye ofisi yako kitu ambacho mwajiri hata kubali unaweza poteza huku. Na ukishindwa kutoroka basi jua kwenye biashara yako kutakuwa na uhuru wa manyani.

Kitu kingine ni kamba sio kila biashara inayofungwa au kufilisika basi wafanyakazi au mfanyakazi wako amekuibia. Mara nyingi wafanyakazi waaminifu huwa wanaingiza hasara kwa kutojua thaman halisi ya biashara kwa maana mtaji,faida na nini watumie na nn wasitumie. Kwa mfano mfanyakazi wako anaweza laza mauzo ya sh. 200,000/ kwa siku akaona ni hela nyingi sana nae anaamua kujiponheza kwa kazi nzuri atajiwekea bando la elfu tano kwenye smu, atanunua na kiatu cha 15,000/ akiamini anajipongeza lakin kumbe katika hayo mauzo ya laki mbili faida ni 30,000/ tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Extrovert

JF-Expert Member
Feb 29, 2016
39,773
2,000
Mojawapo ya sababu ya wahindi kufanikiwa sana kwenye biashara ni kwamba wahindi huwa wanamchukulia kila mtu wanayemuajiri kuwa ni potential "mwizi". Hata siku moja mhindi hamuamini mfanyakazi wake kwenye pesa.

Ukiwa unaenda jioni tu tayari unawapa mwanya wafanyakazi wako wa kujifanyia watakavyo. Wanaweza wasikuibie pesa lakini wakahonga chakula, kufanya uvivu, kutokutumia lugha nzuri kwa wateja etc.

Be there yourself to set the standards you require. Kama umeshindwa kabisa kufanya hivyo basi show up unexpectedly, usiwe na muda maalum.

Define kundi unalotaka liwe wateja wako halafu wapikie chakula cha bei na flavour zinazoendana na matakwa yao.

Hongera sana kwa kutoa ajira.

Kitendo cha kuanza ni uthibitisho tosha kuwa unaweza. Just get closer to your business and "spy" your employees.

Teua kiongozi kati yao, halafu mwingine ongea naye chamber kuwa yeye ni "spy" wako kwa wengine - be ready to reward his work. Watatu aliyebaki tafuta mbinu ajione ana bidii na thamani kuliko wengine. That way unapunguza uwezekano wa wao kushirikiana kukuibia au kufanya uzembe.
Hahah hii tabia ya Kanji kabisa. Anatengeneza urafiki wa siri na kila mmoja wenu ili kuwa spy. Kila mmoja atajikuta anamsnitch mwenzie hivyo mtaishia kuwa mnachukiana tu. Hamuwezi kushirikiana kumfilisi!
 
Extrovert

JF-Expert Member
Feb 29, 2016
39,773
2,000
Ni mbinu nzuri ya biashara sema waswahili hatujui tu
hata magari unakuta Toyota, wanaotengeneza vioo wengine, matairi wengine,viti wengine
gearbox wengine na kadhalika, yeye anatengeneza kitu kimoja au viwili anaunga tu.

Ukijaribu fanya kila kitu unapoteza nguvu sana na mda na quality inakuwa sio ya uhakika.

Mwenzio akitengeneza mashati, wewe tengeneza vifungo, kila mtu anatazama quality ya bidhaa yake
Mshua umetoa wazo la akili sana.
 
Extrovert

JF-Expert Member
Feb 29, 2016
39,773
2,000
Bei cheap inategemea na eneo! Kama unauza kinondoni huwezi uza sahani ya wali 1,500/= mzee baba. Dar chakula watu wanauziana mpaka sh.10000 kwa sahani. The least niliowahi kuona ni 3,500 kwa maeneo ya mijini.
Aisee Hili wazo limenikaa sana kichwani mwangu Ila nashindwa namna ya kuanzia....japo sijawahi kuifanya Ila ndiyo biashara ninayokaribia kuifanya.Katika uchunguzi wangu nimegundua siri 3 ya biashara Hii.
1)Usafi
2)Chakula kitamu
3)Bei cheap
4) Huduma nzuri kwa Wateja.
Ukicontrol hayo lazima utoboe.
 
Extrovert

JF-Expert Member
Feb 29, 2016
39,773
2,000
Mim simkatishi mtu tamaa ila hii biashara ni biashara ngumu sana, Utaianza vizuri haipiti miezi 6 ushaumia, labla usiwe na biashara moja, usiitengemee kama ndiyo biashara kuu inayo kuingizia hela
Sio hii tu, biashara yeyote usipokuwa strategic hutoboi!
 
nusuhela

JF-Expert Member
Jan 26, 2014
5,500
2,000
Habari zenu wandugu,

Samahani, leo nimeamua kuja kwenu baada ya muda mrefu kufanya mpango wa kuanzisha biashara. Hivi karibuni nimefanikiwa kupata mtaji kiasi cha sh milioni tano (5,000,000) za Kitanzania. Hamu yangu kubwa ni kumiliki mgahawa.
Maeneo niliyopo ni Dar es Salaam.

Kabla sijaanza hii biashara ningependa kujua machache kutoka kwa wazoefu wa hii biashara.

Kati ya mambo ambayo ningependa kuyajua ni:

1. Je, kwa mtaji huo nitaweza kuendesha biashara hiyo na kupata faida?

2. Ni changamoto zipi nitakutana nazo pindi tu nitakapoanza hii biashara.

3. Ni vitu gani vya kuzingatia wakati wa kuendesha hii biashara.

4. Ni maeneo gani kwa mtaji huu yatafaa kuendeshea hii biashara nikapata faida ya kuridhisha.

Ahsanteni sana
 
Dharra

JF-Expert Member
Jun 23, 2017
1,667
2,000
Habari zenu wandugu.
Samahani, leo nimeamua kuja kwenu baada ya muda mrefu kufanya mpango wa kuanzisha biashara.
Hivi karibuni nimefanikiwa kupata mtaji kiasi cha sh milioni tano (5,000,000) za kitanzania.
Hamu yangu kubwa ni kumiliki mgahawa.
Maeneo niliyopo ni dar es salaam.

Kabla sijaanza hii biashara ningependa kujua machache kutoka kwa wazoefu wa hii biashara.

Kati ya mambo ambayo ningependa kuyajua ni
1. Je, kwa mtaji huo nitaweza kuendesha biashara hiyo na kupata faida?

Jibu ni ndio kwa mtaji wa milioni tano unaweza kuendesha biashara na kupata faida

2. Ni changamoto zipi nitakutana nazo pindi tu nitakapoanza hii biashara.

Kwanza uwe tayari ku run biashara yako kwa siku kadhaa bila ya wateja, pili kama huna certificate ya FDA tegemea kusumbuliwa sana, tatu tegemea kukosa hiki na kile wakati wa kuanza (hii unaweza kununua vifaa kidogo kidogo kadri muda unavyoenda), tegemea malalamiko kwa hao wateja wachache watakao tumia huduma.

3. Ni vitu gani vya kuzingatia wakati wa kuendesha hii biashara.
Zingatia, sana sana usafi, usafi wamazingira na watoa huduma hii ni muhimu sana, huwezi kuendesha biashara ya mgahawa bila ya kuwa na mpishi ambae ni muelewa na ako na uzoefu wa kutosha, tatizo watu wa aina hio wengi tayari wana ajira zao kwa hio ni kitu cha kumtoa sehemu alipo na kumleta kwako itakugharimu kidogo, tahadhari hapa usichukue wapishi wa vichochoroni ama wale wanaopika pilau kwenye sherehe mitaani itakugharimu sana biashara nzuri kwa chakula ni ile inayo range kati na kati

4. Ni maeneo gani kwa mtaji huu yatafaa kuendeshea hii biashara nikapata faida ya kuridhisha.

Popote pale unaweza kuanzisha biashara ya mgahawa na ikaenda vizuri kutegemea na kundi gani unalilenga. Maeneo yenye movement kubwa ya watu kama mbangala, tandika, temeke mwisho na mengine kama hayo unaweza kuanzisha hio kitu. Zingatio, jikurupushe sokoni, feri na maeneo ya minada kwa kupata vitu bei nafuu alfajiri mapema
Ahsanteni sana
 
essy sensei

JF-Expert Member
Feb 11, 2017
251
500
Tatizo sio mtaji kuwa wa kutosha au kutotosha.

Kitu muhimu ni taarifa muhimu/sahihi kwa unachotaka kukifanya, na taarifa utazipata kwa kuzifanyia utafiti wa hicho unachotaka kufanya.

Nakushauri

1) Jua aina ya biashara unayotaka kufanya na kwa ubora gani,
2) Jua walengwa wako kina nani,
Na wanapatikana maeneo gani, na hapa ndio utajua ukafungue wapi biashara yako.
3) wafuate walengwa wako japo kwa uchache ujue wanahitaji nini
4) Pita kwenye biashara za wengine jua wanafanyaje
5) Pitia social media za biashara za wenzio pitia comments itakusaidia kujua pia nini kinalalamikiwa au kusifiwa nawe ukavifanyie kazi katika maandalizi yako ya kwanza hiyo biashara.
Nakutakia heri.
 
nusuhela

JF-Expert Member
Jan 26, 2014
5,500
2,000
Tatizo sio mtaji kuwa wa kutosha au kutotosha

Kitu muhimu ni taarifa muhimu/sahihi kwa unachotaka kukifanya, na taarifa utazipata kwa kuzifanyia utafiti wa hicho unachotaka kufanya

Nakushauri

1) Jua aina ya biashara unayotaka kufanya na kwa ubora gani,
2) Jua walengwa wako kina nani,
Na wanapatikana maeneo gani, na hapa ndio utajua ukafungue wapi biashara yako.
3) wafuate walengwa wako japo kwa uchache ujue wanahitaji nini
4) Pita kwenye biashara za wengine jua wanafanyaje
5) Pitia social media za biashara za wenzio pitia comments itakusaidia kujua pia nini kinalalamikiwa au kusifiwa nawe ukavifanyie kazi katika maandalizi yako ya kwanza hiyo biashara.
Nakutakia heri.
Ahsante sana
 
milionea wa kesho

JF-Expert Member
Dec 28, 2015
331
1,000
Tafuta location ambayo utaweza kuuza chakula kwa bei ya juu mfano wali nyama kuanzia 3000/=

Chini ya hapo usifanye biashara hii kabisa.
 
Alvajumaa

JF-Expert Member
Jul 5, 2018
3,839
2,000
Mtaji unatosha kabisa, issue hapo location.

Kama utapata sehemu nzuri ambayo chakula unaweza kuuza Tsh 2000, ongeza na vinywaji baridi, pia weka na kijana wa chips maana wadada wengi ndo chakula chao.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom