Fahamu juu ya mgogoro wa Cuba na Marekani 1962

Mpinzire

JF-Expert Member
Jan 18, 2013
7,225
12,948
1962 uliibuka mgogoro ambao ulitaka kupelekea vita kati ya nchi ya Cuba na Marekani mara baada nchi ya Marekani kugundua kuwa USSR inaweka makombora ya Nuklia nchini Cuba, Nchi ya Cuba chini Fidel castro ilikuwa ni mshirika wa karibu sana wa Umoja wa Kisovieti (USSR).

Chanzo hasa kilichopelekea USSR kuweka makombora hayo nchini Cuba kilikuwa USSR kugundua kuwa Marekani alikuwa ameweka makombora ya Nyuklia kwa siri nchini Uturuki kitu ambacho alikiona kitisho kwake naye akaamua kufanya hivohivo nchini Cuba.

Mgogoro huu uliisha baada ya Marekani na USSR kukubaliana kwa pamoja kila mmoja kuondoa siraha za Nyuklia katika nchi zilikowekwa, yaani Urusi aondoe Cuba na Marekani aziondoe pale Uturuki, jambo hili lilimghabisha Rais wa Cuba wa wakai uo Rais Fidel Castrol ambaye yeye alikuwa anataka Marekani apigwe tu!

Kwasasa tunaona Marekani akishinikiza NATO kujitanua kuelekea Russia, Nato inatumika kama mwamvuli kwa marekani kusambaza silaha zake karibu na Urusi. Mbali zaidi Finland ambae mara baada ya vita ya pili ya Dunia aliamua kutofungamana kwenye upande wowote kitu ambacho kilipelekea mpaka wake na Urusi kuwa moja ya mipaka salama zaidi Duniani! Finland kwasasa imegeuka imeenda kujiunga NATO, Kwa maana kwasasa Marekani anaweza kuitumia Finland kuifanyia ujasusi Russia kitu ambacho kinakuja kuzalisha mgogoro mkubwa kati yake na Urusi. Finland inashare mpaka na Urusi wenye urefu wa KM 1,340.

Tutarajie Urusi kuunda muungano wa kijeshi utakaoenda sambamba na BRICS huku akifikisha makombora yake karibu na Marekani kupitia nchi kama Mexico na Cuba?

Unauona usalama wa dunia kwa % ikitokea hivi kwa pande zote mbili?
Cuba.jpg


 
... kwa sasa Castro yumo kwenye kakibubu amehifadhiwa kabatini kwenye makumbusho! Huyu Mungu huyu sifa na utukufu hakika ni vyake.
 
Marekani walikodishiwa bila ukomo Guantanamo Bay mwaka 1903 na serikali ya Cuba kwa matumizi yao ya kijeshi baada ya kuwasaidia Wa Cuba kuwaondoa wakoloni wa Hispania katika vita.
Nje ya mada inakuwaje USA ana ile Guantanamo Bay camp nchini Cuba wakati tunajua hawapatani,ilikuwa kuwaje
 
Marekani walikodishiwa bila ukomo Guantanamo Bay mwaka 1903 na serikali ya Cuba kwa matumizi yao ya kijeshi baada ya kuwasaidia Wa Cuba kuwaondoa wakoloni wa Hispania katika vita.
Sawa
 
Kachelewa sn ajiandae kupigwa pingu kama Trump ambaye ss hv yupo courtroom kujibu tuhuma zake za ngono.

Usa hakuna kinachoshindikana
 
Back
Top Bottom