Mashambulio ya anga yanayoongozwa na Marekani dhidi ya Houthi hayawezi kumaliza mgogoro katika Bahari Nyekundu

ldleo

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
1,010
1,035
Vessel.PNG

Marekani na Uingereza zimefanya mashambulio mfululizo ya anga dhidi ya maeneo kadhaa yaliyolengwa ya kundi la Houthi la nchini Yemen hivi karibuni, lakini kundi hilo linadai kuwa, halijayumbishwa na mashambulio hayo na kuahidi kulipiza kisasi.

Wachambuzi wanasema, mashambulio hayo ya kijeshi yataongeza mapigano katika kanda hiyo, na pia, kabla ya kumaliza mgogoro wa Gaza, si rahisi kumaliza mgogoro katika Bahari Nyekundu.

Licha ya kushambulia Yemen, Marekani pia imeshambulia maeneo yaliyolengwa yanayohusiana na Iran nchini Syria na Iraq, baada ya kupata ripoti juu ya shambulio dhidi ya kambi yake ya kijeshi iliyoko Jordan, shambulio lililofanywa na ndege zisizo na rubanoi na kusababisha vifo vya askari watatu wa Marekani.

Wachambuzi wanasema, kuongezeka kwa mashambulio ya kijeshi katika kanda ya Mashariki ya Kati kutaleta changamoto mpya katika hali tete ya uchumi wa dunia unaofufuka taratibu, hususan kwa nchi ambazo zinakabiliwa na kupanda kwa gharama za maisha na zinazotegemea kwa kiasi kikubwa upatikanaji wa nishati kutoka Mashariki ya Kati kupitia Bahari Nyekundu.

Kwa mujibu wa Reuters, Makao Makuu ya Jeshi la Marekani yamesema, mashambulio ya anga yanayoongozwa na Marekani yamelenga maeneo 36 ya kundi la Houthi nchini Yemen, ikiwemo ghala la kuhifadhi silaha, mfumo wa makombora, na maeneo mengine muhimu ambayo kundi hilo linayatumia kufanya mashambulio dhidi ya meli za kibiashara katika Bahari Nyekundu.

Waziri wa Ulinzi wa Marekani Lloyd Austin amesema, kitendo hicho kinatuma ujumbe wa wazi kwa kundi la Houthi, kwamba litaendelea kushambuliwa kama halitaacha mashambulio haramu katika meli za kimataifa na kijeshi katika Bahari Nyekundu.

Lakini msemaji wa kijeshi wa kundi la Houthi, Yahya Sarea amesema, mashambulio ya Marekani hayawezi kuachwa bila ya malipizi, na kusema kuwa, mashambulio ya kundi hilo katika Bahari Nyekundu yataendelea. Ameongeza kuwa, mashambulio ya Marekani hayatalifanya kundi hilo kuachana na msimamo wake wa kimaadili, kiimani na kibinadamu katika kuunga mkono watu wa Palestina katika Ukanda wa Gaza.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani hivi karibuni amefanya ziara katika nchi za Saudi Arabia, Misri, Qatar, Israel na eneo la Magharibi mwa Mto Jordan. Sehemu kubwa ya ziara hii itahusisha wito wa kusimamisha mapigano kwa muda na kubadilishana mateka.

Hata hivyo, wachambuzi wanasema, kusimamisha mapigano kwa muda sio suluhisho la kimsingi la tatizo, kwa kuwa kusitisha mapigano kunamaanisha kuwa pande zinazohusika hazijafikia lengo lao, na kwamba mapigano yataanza tena. Sasa, wakati ikitafuta ‘kusimamisha mapigano kwa muda,’ Marekani imezuia juhudi nyingi zinazofanywa na nchi wajumbe wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa zinazojaribu kupitisha azimio la kumaliza mapigano. Kutokana na hali hiyo, maeneo mengine kama Bahari Nyekundu, yataendelea kuathirika, na hali ya sasa ya Ukanda wa Gaza haioneshi matarajio mazuri.
 
Back
Top Bottom