Mimi najiita mzalendo na naipenda nchi yangu TANZANIA; yote mambo anayofanya MAGUFULI hapa nchini kuleta maendeleo nayakubali na namsifu kwamfano vita dhidi ya rushwa , ujenzi wa miundo mbinu na pia ujenzi wa viwanda [ ingawa sikubaliani nae kujenga viwanda bila kuweka mkazo vile vile wa kuendeleza kilimo]. Mahala ninapotofautiana nae ni pale anapokuwa inconsistent katika maamuzi yake; huwezi kuamua kuwa sehemu za kanda ya ziwa wasivunjiwe nyumba zao hata kama wamekiuka sheria ili mradi eti walimpigia kura wa yeye kuwa RAIS at the same time watu wa mikoa mingine waliokiuka sheria zile zile wao nyumba zao zibomolewe!! Maamuzi kama haya huharibu umoja wa nchi kwa kuwatenganisha watu kutokana na kule wanakotoka.
Katika mambo ya uwekezaji ,napata shida sana kwa mfano pale anapoamua kununua ndege na kulipa hela zote kwa mkupuo mmoja[ cash]!! Angeweza kutumia fedha hizo hizo kununua ndege na pia kujenga shule na hospitali hapa nchini kama angefanya utaratibu wa kuwalipa watengenezaji Kidogo kidogo kwa makubaliano wakati ndege hizo zingekuwa zinafanya kazi!! Duniani kote hakuna nchi inayonunua ndege cash!! Katika miradi yetu ya miundo mbinu inaelekea tunaweka mkazo wa kumaliza hiyo miradi kwa muda mfupi bila kuangalia viwango vya utendaji; mifano ni barabara tunazojenga ambazo kila mara zinaharibiwa na mvua wakati wa masika hivyo kutumia tena fedha nyingi kurudia kuzitenegeneza.
Magufuli kweli ana nia njema na nchi yake lakini je haya lote anayotekeleza yasingeweza kufanywa bila kukandamiza haki za msingi za wananchi? Je isingwezekana kupata haya mafanikio bila kuwakandamiza vyama vya upinzani, kupiga marufuku magazeti yanayokosoa sera zake , kuwateka na wananchi kupotea? Tukumbuke kuwa tunapozungumzia maendeleo ya nchi hatuzungmzii idadi ya Barbara na magari yanayotembea barabarani bali inabidi tuzungumzie hali na ustawi wa wananchi kwa ujumla wake!!