Kijakazi
Platinum Member
- Jun 26, 2007
- 9,352
- 15,070
Wanabodi,
Habari za Jioni!.
Niko kwenye social function fulani, MC wa Sherehe hii ni mmoja wa MC wakongwe nchini na mahiri, ila aliniboa alipotangaza rasmi kuwa miongoni mwa wageni waheshimiwa sana ni viongozi wa Chama na Serikali!.
Niliboreka kwa sababu msamiati huu wa viongozi wa Chama na serikali ulifutwa rasmi baada ya Tanzania kuingia rasmi katika mfumo wa vyama vingi. Msamiati rasmi wa sasa ni "viongozi wa vyama na serikali" hata kama wote watakaokuwepo ni viongozi wa chama kimoja!.
MC anaendelea kuwataja, tunaye Mhe. Waziri, Benard Membe na kiongozi wa Chama ni Nape Mnauye!.
Ulipofika wakati wa chakula, Mhe. Membe akielekea kwenye bufee, nikamsalimia na kumwambia "tunakuombea Uoteshwe!"
Kwa wanaokumbuka kile kipindi cha Dakika 45 cha ITV, Mhe. Membe alitoa Ole kuwa tuombee asioteshwe, kugombea urais 2015!, maana akoteshwa kuna watu watahama nchi!.
Baada ya kumtania "tunakuombea Uoteshwe!", akacheka tuu, nikamuuliza inakuwaje mpaka leo hajaoteshwa?!, akajibu kilichomcheweshwa kuoteshwa ni kwa sababu "silali usingizi!". Nafanya kazi usiku na mchana hivyo sipati kabisa muda wa kulala usingizi, ila siku nikipata muda wa kulala, labda nitaota!.
Mazungumzo yetu yakaishia hapo!.
My Take.
Kwenye politics hakuna permanent friends or permanent enemies but only a common interests. Kama target ni Ikulu 2015, huyu jamaa akioteshwa msije kuwashagaa watu humu wakizihama Kambi walizo toka nazo mbali na kujiunga na timu za ushindi tarajiwa, haswa kwa kuzingatia utamaduni wa CCM siku hizi ni kuwa dump competent candidates na kuwakumbatia "the incopentent ones!.
Pasco
Kwa nini hukumuuliza kazi gani hiyo inayomkosesha usingizi? Mbona hatuoni matokeo yoyote si Wizarani kwake hapa nymbani wala Nje ya nchi kwenye Balozi zetu, Watz wanaoishi nje wanalalamika Ubalozi hauna msaada wowote kwao hata pasipoti tu kupata ikitokea imepotea ni ishu wakati ni haki yao, sasa sijui hiyo kazi anayofanya ni ipi labda ya majungu na mzee wa busha Ikulu usiku kucha hapo sawa lkn SIYO ya Maendeleo!