Face To Face With Mhe. Benard Camilius Membe!. "Sipati Usingizi!"

Face To Face With Mhe. Benard Camilius Membe!. "Sipati Usingizi!"

Wewe timu yako ni kwa Mzee Wa unga kichwani. kwa joka la mdimu unatafuta nini? Badala ya kupanga mikakati yenu ya ushindi unabaki unapepesa macho kama ka.ha.ba la kinondoni? Bure kabisa!!
RIP BCM
P
 
Hili nalo ni neno

Pengine wakasoaji wa CCM wanaona tofauti na CCM inavyoona.

Pengine ipo haja ya kuomba miongozo wanayotumia kuteua/kupendekeza incompetent huku ikiwa-dump competent candidate.
RIP BCM
P
 
Kwa nini hukumuuliza kazi gani hiyo inayomkosesha usingizi? Mbona hatuoni matokeo yoyote si Wizarani kwake hapa nymbani wala Nje ya nchi kwenye Balozi zetu, Watz wanaoishi nje wanalalamika Ubalozi hauna msaada wowote kwao hata pasipoti tu kupata ikitokea imepotea ni ishu wakati ni haki yao, sasa sijui hiyo kazi anayofanya ni ipi labda ya majungu na mzee wa busha Ikulu usiku kucha hapo sawa lkn SIYO ya Maendeleo!
RIP BCM
P
 
Loh,
Mkuu Paaco; hili bandiko lilinipita.
Kwa namna ulivyofanya simple analysis ya kilichotokea 2005 na bandiko lako la prediction kuhusu mkuu wa kaya wa sasa, sir, I salute you.

Nadhani mhusika wa njozi aliahidi akioteshwa atasema. Bahati mbaya hajawahi kusema njozi yake ina connect vip na future ya Watanzania.

Martin Luther King alisema, I have a dream...njozi ile iliwaunganisha wazungu kwa weupe kutokuhukumiwa by colour of skin but by content of character.

Mahtma Gandhi alikiwa na njozi ya India kuwa huru pasi "violently movement"

Binafsi sijawahi kusikia njozi ya muotaji wakati anachukua form 2015 na kama njozi huenda ilinipita, basi mwangwi wake ku-connect na future ya Watanzania mil 56+ sikuwahi kuisikia waziwazi mbali na umahiri wa kazi aliyofanya kwenye ofisi iliyomuajiri baada ya kuhitumu masomo ya sekondari

Sent using Jamii Forums mobile app
RIP BCM
P
 
Mkuu Kingu, kwanza mimi sio mwanasiasa, sio mwanachama wa chama chochote, hivyo sihitaji kabisa kuaminika na yeyote kwa sababu siasa kwangu is nothing!.

Sijipendekezi kwa yoyote ila kwenye siasa kuna watu ninaowakubali sana wakiongozwa na jamaa yangu aliyeko CCM akifuatiwa na ile lulu ya Chadema!. I don't expect anything from any politician, hivyo niko free kumsupport yoyote toka chama chochote!.
Pasco.
 
Mkuu Mr. Morisi, humu jf hatuulizani, nani ni nani, humu nimejitambulisha kama Pasco wa jf. Unabidi kunitambua kama Pasco wa JF, nothing more, nothing less!. Na kwa sheria zetu, haliruhusiwi kumfananisha member yoyote wa jf na mtu mwingine yoyote, hata kama wanafanana vipi au kushabihiana kwa kiwango chochote.
Pasco
 
Wanabodi,
Habari za Jioni!.
Niko kwenye social function fulani, MC wa Sherehe hii ni mmoja wa MC wakongwe nchini na mahiri, ila aliniboa alipotangaza rasmi kuwa miongoni mwa wageni waheshimiwa sana ni viongozi wa Chama na Serikali!.

Niliboreka kwa sababu msamiati huu wa viongozi wa Chama na serikali ulifutwa rasmi baada ya Tanzania kuingia rasmi katika mfumo wa vyama vingi. Msamiati rasmi wa sasa ni "viongozi wa vyama na serikali" hata kama wote watakaokuwepo ni viongozi wa chama kimoja!.

MC anaendelea kuwataja, tunaye Mhe. Waziri, Benard Membe na kiongozi wa Chama ni Nape Mnauye!.

Ulipofika wakati wa chakula, Mhe. Membe akielekea kwenye bufee, nikamsalimia na kumwambia "tunakuombea Uoteshwe!"

Kwa wanaokumbuka kile kipindi cha Dakika 45 cha ITV, Mhe. Membe alitoa Ole kuwa tuombee asioteshwe, kugombea urais 2015!, maana akoteshwa kuna watu watahama nchi!.

Baada ya kumtania "tunakuombea Uoteshwe!", akacheka tuu, nikamuuliza inakuwaje mpaka leo hajaoteshwa?!, akajibu kilichomcheweshwa kuoteshwa ni kwa sababu "silali usingizi!". Nafanya kazi usiku na mchana hivyo sipati kabisa muda wa kulala usingizi hadi kuota ndiyo, ila siku nikipata muda wa kulala usingizi wa kuota ndoto, labda nitaota!.

Mazungumzo yetu yakaishia hapo!.
My Take.
Kwenye politics hakuna permanent friends or permanent enemies but only a common interests. Kama target ni Ikulu 2015, huyu jamaa akioteshwa msije kuwashagaa watu humu wakizihama Kambi walizo toka nazo mbali na kujiunga na timu za ushindi tarajiwa, haswa kwa kuzingatia utamaduni wa CCM siku hizi ni kuwa dump competent candidates na kuwakumbatia "the incopentent ones!.

Naomba mlisome bandiko hili with reference ya bandiko hili Mgombea wa Urais Kwa tiketi ya CCM, 2015 "Could Be" John Pombe Magufuli - JamiiForums

Pasco
Update 12 May 2023
Bernard Camilus Membe,
Umepigana vita vilivyo vitakatifu,
Imani umeitunza,
Mwendo umeumaliza!.
Bwana alileta
Bwana ametwaa
Jina lake Lihimidiwe!
Amen.
RIP Bernard Cammilus Membe
Paskali
Hii ni farewell yangu kwa huyu shujaa Buriani Benard Membe, Umepigana Vita Vilivyo Vitakatifu, Mwendo Umeumaliza, Imani Umeitunza, Madeni Yako Yaliyobakia Karma Itakulipia!
P
 
Back
Top Bottom