Mkuu 50thebe, kwanza asante!, tangu uzi huu umeanza, wewe ndie pekee, umejua nazungumzia nini hapa!, kiukweli wengi wa members humu wamezoea kupikiwa, wapakuliwe, wawekewe kwenye sahani, walishwe, wao ibaki kutafuna tuu na kumeza, lakini sasa hata kutafuna hawawezi, hadi watafuniwe!, wao kazi yao ubaki kumeza!.
Back to the topic, kati ya finalists wa 2005, unaweza kukumbuka who were the most competent?!, unavikumbuka vigezo vya kumpitisha the most incompetent?!, "ni mwenzetu!", "anakubalika!", "anachagulika!", "ana chemo na bashasha!", "ana sura nzuri!" etc, etc, ukimpima na kumlinganisha kichwani ana nini, unakuta nothing!, aliwahi kufanya nini?, nothing!, ana track gani ya utendaji?!, nothing!.
Kuna possibility ya 2005 scenario ikajirudia 2015!, ila to play safe, hakuna ubishi, the the one and only best CCM, has ni yule "jamaa yangu", "the competent one!", wamemshauri Pinda ajitose, ili kumzuia yule "jamaa yangu" na atachinjiwa baharini asubuhi subuhi kwa kisingizio cha hatuwezi kuwapitisha ma PM wawili at the same time!, huwezi kumuacha the sitting PM ukamchukua former PM!. Hapo kuna boya la Mzanzibari pia atachagizwa kuchukua fomu, ili na yeye afanywe pace maker kumpitisha "the chosen one!", ambaye might be "incompetent", huyu Mzanzibar anayefit sana ni Dr. Gharib Bilal!.
Yule Master Minder wa JK anaitwa Jack Gotham, ndio yuko behind "la mdimu", hivyo as of now, 2005 inajirudia!.
Pasco.