Paul Makonda informer wa Benard Membe katika ya Utawala Magufuli

Suzy Elias

JF-Expert Member
Nov 9, 2021
1,067
6,193
Ipo habari msisimko isiyofahamika na wengi kumhusu Aliyewahi kuwa W NJ ndugu Benard Membe aliyetangulia mbele za haki na ndugu Paul Makonda aliyepata kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam. Nyuma ya pazia, wawili hao wana hadithi nzuri na yenye fundisho ndaniye. Kwa sababu wahusika wakuu hatunao tena, yaani JPM na BM acha leo niwashirikishe.

Ikumbukwe, Makonda kabla ya ujio wa kishindo wa Magufuli Mamlakani alikuwa timu Membe tena mwandani kabisa! Na Membe ndiye aliye mshawishi Kikwete amteue Makonda kuwa DC wa Kinondoni. Lengo la BM kumwombea uteuzi mtoto mpendwa tena kwenye Wilaya yenye hadhi ya Jiji ilikuwa kumwandalia/ kumsafishia njia bwana Makonda ili baadae imuwie u rahisi kugombea Jimbo la Kinondoni mwaka 2015 kwenye Uchaguzi Mkuu. Na ndoto ilikuwa BM angefanikiwa kuwa Rais ndiposa angelimteua Makonda kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi ( W MNN) ndoto iliyoyeyushwa na ujio wa bahati wa JPM.

Kutokana na JPM kutoka Kanda pendwa kama ilivyo kwa Makonda na kuelewana lugha, na kwa sababu nyingine ambayo ni nyeti aliyomtonya JPM na baada ya tonyo lile kuja kuwa la kweli; bwana Makonda akaaminiwa na JPM hakika. Hali ya kuaminiwa ghafla na Boss mpya ilipelekea ateuliwe kuwa RC wa Jiji Kuu la Dar es Salaam. Kilichofuatia baina ya wawili hao, ni historia!

Sasa basi, pamoja na uswahiba wa kufa na kuzikana baina ya Makonda na JPM, bado Makonda alikuwa mwaminifu kwa BM. Lakini, baada ya JPM na BM kuwa maadui wakubwa BM alimpa uhuru Makonda wa kumponda huku akiendelea kumtonya za ndaniii kabisa ambazo JPM alikusudia kumtendea BM.

Mikakati yote ambayo ilipangwa kumhusu BM ilianzia kwa mtoto pendwa na kabla ya utekelezaji wake mtoto pendwa alimtonya BM kupitia namna ya mawasiliano yao waliyokuwa wameyafanya kuwa rasmi.

Mlishajiuliza kwa nini BM alikuwa anasanua kila mpango pangwa kwake? Jibu ni mnyetishaji alikuwa mtoto pendwa na JPM asingeweza kung'amua hilo kwa namna alivyokuwa anamwamini dogo na ilifikia wakati hata alikuwa anaenda mwenyewe kutekeleza mission bila awaye na kupitia mwanya huo alikuwa akikutana na mtu kati baina yake na BM kumpa mpango utarajiwao kumuumiza ili ajinasue.

ULISHAJIULIZA KWA NINI BM ALIKUWA AKIMZODOA JPM KWAMBA CHOCHOTE ANACHOKIPANGA IWE USINGIZINI AMA NDOTONI YEYE ANAKIFAHAMU?! JIBU NI MTOTO PENDWA ALIKUWA ANAVUJISHA SIRI.

Pamoja na mikakati yote iliyopangwa kwa ajili ya kumnyamazisha BM alikuwa mshirika, lakini dogo alihakikisha BM anatonywa ili aweze kujinasua. Hiyo yote ilitokana na wema aliotendewa na BM kabla ya JPM kuibuka ghafla.

BM alishamwepusha na hatari nyingi Makonda zilizokuwa zikipangwa na timu mamvi na R kipindi akiwashambulia kwa tuhuma za ufisadi. Lowasa na Rostam walichukizwa mno na Makonda kwa namna ambayo kwao ilikuwa inawachafua na walishuhudia kupitia mashambulizi ya Makonda twasira yao kisiasa, inaharibiwa. Ikumbukwe, bwana Lowasa alikuwa kinara wa mbio za kuutaka u Rais.

Pamoja na uswahiba wa yeye ( Makonda) na JPM lakini bado kwa namna yeyote aliapa kulipa fadhira kwa kumwepusha BM na dhahama yeyote ile.

Ujanja wote wa Membe na kiburi chote ndani ya Utawala wa JPM ulihisaniwa na Makonda ambaye ndiye alikuwa mwandani wa kufa na JPM.

Paul haishi Masaki kwa bahati mbaya. Paul ni CHUNGU NA TAMU KWA WATAWALA! Paul yupo, atakuwepo hadi mwenyezi Mungu ATAKAVYOAMUA VINGINEVYO.

Na siku USA watakapomwondolea Makonda tuhuma walizo mtuhumu, amini nawaambia mtoto pendwa atarejeshwa kesho yake katika Ufalme wa 🇹🇿.

IMANI YA JPM KWA MAKONDA NDIYO ILIYOMWEPUSHA NA HATARI NYINGI BM.

NB: ZIMWI LIKUJUALO....
 
IMG_6822.jpg
 
Ipo habari msisimko isiyofahamika na wengi kumhusu Aliyewahi kuwa W NJ ndugu Benard Membe aliyetangulia mbele za haki mapema juzi na ndugu Paul Makonda aliyepata kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam nyuma ya pazia.

Ikumbukwe, Makonda kabla ya ujio wa kishindo wa Magufuli Mamlakani alikuwa timu Membe tena mwandani kabisa na Membe ndiye aliye mshawishi Kikwete amteue Makonda kuwa DC wa Kinondoni ili hapo baadae Makonda imuwie u rahisi kugombea Jimbo la Kinondoni mwaka 2015 kwenye uchaguzi mkuu na ndoto ilikuwa BM angekuwa Rais na ndiposa Makonda angeteuliwa na BM kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi ndoto iliyoyeyushwa na ujio wa bahati wa JPM.

Kwa sababu ya kuelewana lugha na kwa sababu nyingine ambayo ni nyeti aliyomtonya JPM na baada ya tonyo lile kuja kuwa la kweli bwana Makonda akaaminiwa na JPM hakika hali iliyopelekea ateuliwe kuwa RC Dar es Salaam na kilichofuatia baina ya wawili hao ni historia.

Sasa basi, pamoja na uswahiba wa kufa na kupona baina ya Makonda na JPM lakini bado Makonda alikuwa mwaminifu kwa BM japokuwa sasa baada ya JPM na BM kuwa maadui wakubwa BM alimpa uhuru Makonda wa kumponda huku akiendelea kumtonya za ndaniii kabisa ambazo JPM anazikusudia kumfanyia BM.

Hatari zote ambazo zilipangwa za kumhusu BM zilianzia kwa mtoto pendwa na kabla ya utekelezaji wake mtoto pendwa alimtonya BM kupitia namna ya mawasiliano yao waliyokuwa wameyafanya kuwa rasmi.

Mlishajiuliza kwa nini BM alikuwa anasanua kila mpango pangwa kwake? Jibu ni mnyetishaji alikuwa mtoto pendwa na JPM asingeweza kung'amua hilo kwa namna alivyokuwa anamwamini dogo na ilifikia wakati hata alikuwa anaenda mwenyewe kutekeleza mission bila awaye na kupitia mwanya huo alikuwa akikutana na mtu kati baina yake na BM kumpa mpango utarajiwao kumuumiza ili ajinasue.

ULISHAJIULIZA KWA NINI BM ALIKUWA AKIMZODOA JPM KWAMBA CHOCHOTE ANACHOKIPANGA IWE USINGIZINI AMA NDOTONI YEYE ANAKIFAHAMU?!

Makonda alikuwa hawezi kabisa kukubali mipango yeyote ya kumuumiza BM kwa sababu ya wema aliotendewa na BM kabla ya JPM kuibuka ghafla.

BM alishamwepusha na hatari nyingi Makonda zilizokuwa zikipangwa na timu mamvi na R kipindi akiwashambulia kwa tuhuma za ufisadi Lowasa na Rostam na kwalo pamoja na uswahiba wa yeye na JPM lakini bado kwa namna yeyote aliapa kulipa fadhira kwa kumwepusha BM na dhahama yeyote ile.

Ujanja wote wa Membe na kiburi chote ndani ya Utawala wa JPM ulihisaniwa na Makonda ambaye ndiye alikuwa mwandani wa kufa na JPM.

IMANI YA JPM KWA MAKONDA NDIYO ILIYOMWEPUSHA NA HATARI NYINGI BM.

NB: ZIMWI LIKUJUALO....
Sijaamimi hii....
 
Back
Top Bottom