Face To Face With Mhe. Benard Camilius Membe!. "Sipati Usingizi!"

Face To Face With Mhe. Benard Camilius Membe!. "Sipati Usingizi!"

Pascal Mayalla

Platinum Member
Joined
Sep 22, 2008
Posts
58,930
Reaction score
132,461
Wanabodi,
Habari za Jioni!.
Niko kwenye social function fulani, MC wa Sherehe hii ni mmoja wa MC wakongwe nchini na mahiri, ila aliniboa alipotangaza rasmi kuwa miongoni mwa wageni waheshimiwa sana ni viongozi wa Chama na Serikali!.

Niliboreka kwa sababu msamiati huu wa viongozi wa Chama na serikali ulifutwa rasmi baada ya Tanzania kuingia rasmi katika mfumo wa vyama vingi. Msamiati rasmi wa sasa ni "viongozi wa vyama na serikali" hata kama wote watakaokuwepo ni viongozi wa chama kimoja!.

MC anaendelea kuwataja, tunaye Mhe. Waziri, Benard Membe na kiongozi wa Chama ni Nape Mnauye!.

Ulipofika wakati wa chakula, Mhe. Membe akielekea kwenye bufee, nikamsalimia na kumwambia "tunakuombea Uoteshwe!"

Kwa wanaokumbuka kile kipindi cha Dakika 45 cha ITV, Mhe. Membe alitoa Ole kuwa tuombee asioteshwe, kugombea urais 2015!, maana akoteshwa kuna watu watahama nchi!.

Baada ya kumtania "tunakuombea Uoteshwe!", akacheka tuu, nikamuuliza inakuwaje mpaka leo hajaoteshwa?!, akajibu kilichomcheweshwa kuoteshwa ni kwa sababu "silali usingizi!". Nafanya kazi usiku na mchana hivyo sipati kabisa muda wa kulala usingizi hadi kuota ndiyo, ila siku nikipata muda wa kulala usingizi wa kuota ndoto, labda nitaota!.

Mazungumzo yetu yakaishia hapo!.
My Take.
Kwenye politics hakuna permanent friends or permanent enemies but only a common interests. Kama target ni Ikulu 2015, huyu jamaa akioteshwa msije kuwashagaa watu humu wakizihama Kambi walizo toka nazo mbali na kujiunga na timu za ushindi tarajiwa, haswa kwa kuzingatia utamaduni wa CCM siku hizi ni kuwa dump competent candidates na kuwakumbatia "the incopentent ones!.

Naomba mlisome bandiko hili with reference ya bandiko hili Mgombea wa Urais Kwa tiketi ya CCM, 2015 "Could Be" John Pombe Magufuli - JamiiForums

Pasco
Update 12 May 2023
Bernard Camilus Membe,
Umepigana vita vilivyo vitakatifu,
Imani umeitunza,
Mwendo umeumaliza!.
Bwana alileta
Bwana ametwaa
Jina lake Lihimidiwe!
Amen.
RIP Bernard Cammilus Membe
Paskali
 
Huu ni umbeya , huoni aibu kuileta mambo yenu mliyozungumza kwenye kitchen party huko ? Unataka yajadiliwe ?
 
kwahiyo na wewe waweza kuhama aisee muda wowote? wale akina chabruma, ocampo four et al, du basi tutahamini kuwa misimamo yenu ipo tumboni na si kichwani katika kujenga nchi.
 
Pasco umempiga Membe majabali ya ukweli ila uko sawa CCM ikizidiwa ndani kwa ndani wote watarudi kuwa wamoja coz ufisadi wanaufanya wao wote. Team tofauti kwenye kutafuta Urais lkn wakibanwa wanarudi kumtafuta anayekuwa na unafuu kwa upande wao
 
Ungemuuliza pia Kwanini amepania kuwafanya Raia halali wa Nchi hii kuwa wakimbizi akishaoteshwa?
 
Njaa mbaya sana.

Pasco mjin pamekushinda lola chiukapila KAAAPI KAAAAPII...

PASCO UNINASA LOLA CHIUKAPILA kaapi kaaapi.
 
Wadau naomba mtumie lugha bUri kwa kila mtu anayeleta thread yake hapa kama mtu hajui maana ya forums ni bora akakaa kimy kuliko kushitumu.
Back to topic:
Pasco #teamlowasa membe anakua wazi kuwa ulikuwa una mbeep tu.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom