Exclusive Pictures: SeaFront- Imeuzwa nayo!

zambi ya ufisadi ni mbaya sana, yani hawa mafisadi wamefisadi mpaka sehemu ambayo watoto wao walikuwa wakienda kutesa na pesa zao za kifisadi.
Je sasa hivi watoto wa mafisadi wataenda beach wapi??? labda mombasa...
 
Mzee Mwanakijiji
Hizi picha ni msiba wa hali ya juu. Yaani tumefunga ukanda wote wa bahari ili watoto wetu wasome bahari kwenye atlas? Tunategemea watoto wetu wakaone bahari ulaya? Muungwana atasema hii hajauza yeye iliuzwa wakati wa Awamu ya Tatu siyo?Duh sijui hii nchi ina nini kwa kweli.
 
Nawasikitikia sana wadanganyika.

Hapa ni hivi ..you either challenge the system au you support the system.

Kwa kifupi system nzima ya utawala imeoza, kuanzia muundo wenyewe, miundombinu yake na watendaji kwa ujumla wao. Hivyo kama wameuza (niko skeptical bado na ishu ya kuuza, maana nijuavyo waTz tunakodishwa ardhi na serikali kwa kipindi maalum-hamna anayemiliki ardhi Tz zaidi ya Jamhuri) hilo eneo bila kufuata utaratibu..ni nani wa ku-crosscheck?? system haina hiyo taratibu.

Suala la EIA, nani wa ku-crosscheck.?? hamna

Suala la kupasiana pesa haram ya kampeni..Nani wa ku-crosscheck??hamna

The list continues..Kwa hiyo huwezi kupinga dalili ya ubovu wa system badala ya kuipinga system yenyewe. Huo utakuwa ukichaa.

Kwa hio bana, nionavyo mimi humu ndani kila siku tutakuwa tunapiga kelele tuuuuuuu, lakini solution tunaijua. Lazima tubadilishe mfumo wetu wa kujitawala. Kuendelea na system ya sasa hivi tusitegmee kuvuna madafu kwa kupanda chelewa.
 
Abduhalim:

I could not agree more with you!

Watanzania tunaangalia tulipodondokea, badala ya kuangalia tulipojikwaa!

Kwa sasa tunapiga kelele kupinga Tanzania kuwemo kwenye EAC, lakini Rais wetu kasaini mkataba wa kufungua mipaka ya Tanzania, na wabunge wakiidhinisha; Julai 01 2010 joto ya jiwe itakapoanza, ndipo tupige kelele kwenye forum!

Afadhali hapo Masaki wamechukua open-space! Siku hizi watu wanaondolewa kwenye nyumba zao, mradi tu ardhi yao ina thamani kuliko wao!
 
Kamanda nakubali usemayo. Vyanzo vikuu vya matatizo Tz ni

1.SYSTEM
2.SYSTEM
3.SYSTEM!

Hebu chukulia mathalan tatizo la Richmond au EPA. Kama tungekuwa na system inayowajibika it does n't take more than a single whistleblower kuweka tatizo ktk muelekeo wa kutatulika. System ingetake over from there na kuwawajibisha wahusika. Lakini sadly, hatuoni kwamba nchi inatawaliwa na genge fulani la watu. Genge hilo halipo kwa maslahi ya wavuja jasho japo linaigiza hivyo. Llinashirikiana na magenge mengine ya nje kuangalia every possibility ya kujiongezea mafao mifukoni mwao.

Unaweza kushangaa ukiambiwa chanzo cha fukuto la EAC lipo US au EU. Corporate elites wapo serikalini huko au wanakula sahani moja na akina HUssein Onyango. Hawa wana mashirika yao ambayo yamewekeza heavily in Kenya na makampuni mengine makubwa tu kama Barrick et al. Haya yanaangalia jinsi gani ya ku-control EA market, labour na raw materials. Wanajua kutakapokuwa na common denominator kwenye EA agenda itakuwa rahisi zaidi kwao ku-control EAC as an entity badala ya individual countries na haswa ukizingatia tawala zinabadilikabadilika.

Sasa ni vizuri tukamjua adui yetu ni nani mapema anayesababisha kuanguka kwetu, badala ya kama ulivyosema kuangalia tulipoangukia.
 
This is really disheartening. So sad. No decency at all? Most of Dar-es Salaam is already an eyesore. Now even the little remaining paradise is being raped!

I wonder if the late Mwalimu had any inkling of the pervasiveness of the dogs within when, in 1995, he joined the CCM campaign trail prompted by the fear of letting the country go to the dogs.
The dogs have taken it!
 
Sikujua wewe ni mtetezi wa wahindi wa bongo! Je wanakushirikisha wanaponunua majumba london kwa hela za walipa kodi za bongo...i would think twice abt siding with any of them, ajira aint shit to how much money these guys stash abroad!
Muoneee huruma huyo. Hujasoma ile topic ya Mwanakijiji? "----Wepesi wepesi!!"
 
Watanzania lazima tutambue kuwa siku si nyingi sana tutaamka hatuna kitu. Tutajiuliza what happened? Tutajifanya hatujui; tutakuwa tunashangaa na kuulizana. Ukweli ni kuwa tangu milango ya Loliondo ilipofunguliwa with impunity, watawala wetu sasa wanajua wanaweza kufanya lolote walipendalo.

Je mwajua sasa kwanini wanatetemeka sana na CCJ?
 
Yeeeh nazipta vizuri kweli....very clear hakuna chenga kabisa aiseee!

Hivi what should be done to stop this? je, ni kupiga kelele na how? na je, who approved this? na kwa manufaa ya nani?

Aliye approve mambo haya ni mzee ruksa na hata loliondo yeye ndie kaleta lile songombingo lakini kwa sasa anaonekana ni mtu safi. Uchumi wa nchi aliudidimiza na mambo mengi yaliharibikia pale. Kupiga kelele kunaweza kukasaidia sana na hasa ukizingatia kwamba bunge letu sasa lina macho na masikio tuwaambie wabunge hizo kelele zetu na kama hawatatekeleza tutishie kuwaondoa na kuwapa wale watakaoweza kuzisikia kelele zetu.Wabunge wetu wa mkoa wa dsm waambiwe hilo kwa sasa kama hawawezi huu ni muda muafaka kuwaondoa.
 
Tatizo katika ufukwe ule lilianza pale tuliporuhusu Polisi wajenge Mess yao. Hiyo kama ilivyokuwa yacht club ikawa ndiyo precedent! Wakaja wajanja wengine wakadai kujenga Hoteli, tukawaruhusu. Sasa upande mmoja iko Sea Cliff, upande wa pili Golden Tulip kwa nini basi hiyo sehemu ya kati wasiichangamkie? Kwanza watu hawaitumii kama wanavyotumia Coco beach. Nani atakayejali! Tumewapa wenyewe. Tumepindisha sheria kuwaruhusu wajenge, sasa tuvune tulichopanda. Ile sehemu itakapoanza kumomonyoka ndipo tutakapoanza kunyosheana vidole. Ukitaka kujua hasira ya bahari kaangalie Ocean Road. Kaangalie Kunduchi. Itatushikisha adabu bila shaka. Kuwalaumu wahindi ni upuuzi. Lini tumekuwa na Rais au waziri mkuu mhindi? Mhindi gani aliwahi kuwa waziri wa ardhi? Au mkurugenzi wa mipango miji ( au whatever)? Au huko NEMC kuna wahindi wangapi? Ni sisi ndiyo tunaostahili lawama na laana zote zitakazotokana na ulafi wetu. Badala ya kunyosheana vidole tushirikiane sote bila kujali tofauti zetu kupambana na kile alichokiita Abdulhalim System! Uovu huu unabidi uzuiwe, period. Ni lazima tufike mahali tuone aibu.

Amandla.......
 
MJJ tumemmis kweli kanzi pamoja na Enigma au walikuwa busy na hii kazi?
Well done timu nzima ya kanzi kwakweli tunakoelekea siko kabisa hapo wamesha gawiana mapema.
 
Mwenzenu nilishaona kulalamika hakunipi faida...hivyo dawa ni kwenda nao sambasamba...vikiuzwa na mimi nanunua. Nikiwa sina hela najipanga sehemu nyingine.

Arthi yetu ndio hii hii...tunabanana hivyo hivyo.

YY

Mkuu hebu tuambie siri hiyo au na wewe ni walelawle wa chukua chako mapema nini? MAANA HAWA JAMAA HUWEZI KUKIMBIZANA NAO MZEE AU?
 
Alhaji Ali Hassan Mwinyi hajaamua tu kuvirudisha Serikali hivyo viwanjaa? maana naona baada ya kufanya hayo maamuzi alikaa kimya kusikilizia? nakumbuka mpaka zile issue za Baghdad pale mnazi moja wakati wa Mayo Alhaji Kitwana Kondo.
 
halafu tunasema JK mbaya kumbe watangulizi wake ndo nyoka akina mzee ruksa na mkapa. Mfano hata yanayotokea Loliondo waarabu kujitwalia eneo na kuweka mtandao wao yote hayo chanzo ni mzee ruksa.

Juzi mimi na familia yangu tulipita sehemu zile tukaona pamesafishwa natukaanza kubishana kuhusu kitu kilichokuwa kinaendelea pale; mimi nikalaumu kuwa walikuwa wanaharibu mandhali ya sehemu ile kwa kukata miti na vichaka lakini wenzangu wakaamini kuwa city walikuwanafanya usafi!! Wajanja kumbe walikwishajigawia fukwe!! Ingawa inasemekana kuwa haya madudu yalifanyika enzi ya awamu ya pili ya Mzee Ruksa ,[ nakumbuka Mkapa aliahidi wakati wa kampeni yake kuwa angevifuta viwanja vya Golden Tulip, lakini alipoingia madarakani Ladwa akampoza!!], Kikwete anamamlaka ya kuweza kutengua maamuzi yaliyofanywa na waliomtangulia kama yanaathiri ustawi wa jamii; kama serikali imeweza kurudisha mgodi wa Kiwira sembuse hivi viwanja vya pwani!! It will be to Kikwete's credit if he will revoke the titles of all the beach plots that have not been developed ili wananchi na vizazi vijavyo viweze kufaidi urithi wao. Time is the essence, the sooner he acts the better!!
 
Haswa! Ingawa matumaini ni madogo kama atafanya hivyo bila kusukumwa.

Amandla........
 
...Itatusikisha adabu bila shaka. Kuwalaumu wahindi ni upuuzi. Lini tumekuwa na Rais au waziri mkuu mhindi? Mhindi gani aliwai kuwa waziri wa ardhi? Au mkurugenzi wa mipango miji ( au whatever)? Au huko NEMC kuna wahindi wangapi? Ni sisi ndiyo tunaostahili lawama na laana zote zitakazotokana na ulafi wetu. Badala ya kunyooseana vidole tushirikiane sote bila kujali tofauti zetu kupambana na kile alichokiita Abdulalim System! Uovu huu unabidi uzuiwe, period. Ni lazima tufike mahali tuone aibu.

Amandla.......

you nailed it; Watanzania kwa kupenda mepesi mepesi tunakimbilia kuwalalamikia wahindi as if awa wahindi ni wanadamu kutoka sayari nyingine. Mara tunalalamikia wachina, mara wakenya.. halafu katika wazimu wa fikra zetu kesho tunasimama na magwanda yetu ya kijani na njano tukiimba kama kasuku "nambari wani eeeh!!"
 
Hivi mnanambia kuwa hapo paliwahi kuwa na miti? Miye nilikuwa najiuliza kwanini tusipande minazi na kufanya mahali pazuri pa watu wa karibu ya maeneo hiyo kutembea nyakati za jioni n.k? Kumbe miti ilikuwepo wahuni wakakata!
 
Ubaya wa hizi internet new forms of media kama JF ni kwamba hakuna uwajibikaji wa kiasi kinachotakiwa kwajili ya uandishi wa habari ulio ethical and objectivity is non-existent. Ulianzisha thread umekuwa kama Michael Moore, mwishoe no one will take you seriously. Hizi plot ziko chini ya Manispaa na wao wametoa lease kwa watu watakao wekeza kwenye non-permanent forms za businesses on the front, after EIA zikifanyika ili kujua jinsi yakucontrol pollution of the area. Watajenga non-permanent features za kimakuti makuti... sio on a sea cliff level tho. The aim is to provide entertainment ya drive in cinema na food areas na vitu kama hivyo kwaajili ya watu kuenjoy ufukwe. Sijui kama utekelezaji utakuwa kama ilivyosemwa, perhaps not, lakini naomba tuwe objective. This is very low objectivity, kama tupo Venezuela bwana au Saddam's Iraq.lol

Najua of course this area wahindi wamemezea mate muda mrefu, ni hawa wahindi wa cinemax wamepewa amongst a few others as far as I know. Najua lazima rushwa imetembea lakini kuna employment itatokana na haya. The only major thing is that, mazingira yasiharibiwe thats all. That area kunavibaka, ni mtaa yetu wengine tunapajua vizuri. Bora watu wapate ajira bwana. Kwani kitu gani.
Nilishaamua kuacha whisky lakini kwa uchimvi huo inabidi nikatafute supu ya mawe namba wani kabisa.
 
Back
Top Bottom