EWURA yatoa Msaada wa wa Mashuka 431 yenye thamani Mil 5 Vituo vya Afya

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,812
11,982
MAMLAKA ya Udhibiti wa Huduma ya Nishati na Maji (EWURA), imetoa msaada wa mashuka 431 kwa Vituo vinne vya Afya katika Jiji la Dodoma, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya wiki ya utumishi wa umma. EWURA imeona itoe msaada huo kama kurudisha mchango wake kwa jamii kwenye sekta ya afya.

“Mashuka 431 yaliyotolewa kwa Jiji la Dodoma na yataenda kwenye vituo vinne cha Makole, Hombolo, Mkonze na Kikombo”. Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka hiyo, Mhandisi Godfrey Chibulunj amesema.

EWURA imekuwa ikisaidia uboreshaji wa huduma na mara ya mwisho walitoa fedha kwa ajili ya kuboresha huduma ya mama na mtoto wanaozaliwa wakiwa njiti

Ewura.jpg

Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma 2021; Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa EWURA, Mha. Godfrey Chibulunje (kushoto) akikabidhi msaada wa mashuka 431 ya Sh 5M kwa Mganga Mkuu wa Jiji la Dodoma, Andrew Method (kulia) kwa ajili ya vituo vya afya vya Makole, Hombolo, KIkombo na Mkonzi, leo
 
Back
Top Bottom