EWURA yavifungia vituo v3 vya Mafuta, yatoa onyo

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,376
8,118
Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (Ewura), imevifungia vituo vitatu vya mafuta kwa miezi sita baada ya kubainika vilificha mafuta kati ya Julai na Agosti 2023.

Vituo hivyo ambavyo vipo katika mikoa mitatu tofauti vimekumbwa na shubiri hiyo baada ya kuthibitika vilificha mafuta na kusababisha uhaba wa nishati hiyo.

Mkurugenzi Mkuu wa Ewura, Dk James Andilile amesema hayo leo Jumanne, Septemba 18, 2023 jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu hatua walizochukua kufuatia agizo la Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk Doto Biteko.

Dk Andilile amevitaja vituo hivyo ni Camel Oil kilichopo Gairo mkoani Morogoro, Petcom cha Mbalizi, Mkoa wa Mbeya na Rashal Petroleum Ltd kilichopo Mkalama mkoani Singida.

“Pale inapotokea masharti ya leseni hayazingatiwi, hatua lazima zichukuliwe. Kuna baadhi ya vituo vya mafuta ambavyo vimethibitika vilificha mafuta kati ya Julai na Agosti kinyume na taratibu.

Tutavifungia vituo hivi kwa miezi sita kwa kukiuka kanuni pamoja na masharti ya leseni ambayo tumejiwekea,” amesema Dk Andindile.

Mkurugenzi huyo amesema pamoja na kuvifungia vituo hivyo Ewura ipo kwenye mpango wa kuangalia mfumo wa upangaji bei ili hali hiyo isijitokeze tena.

“Pia tunapitia kwa kuangalia na kuboresha masharti ya utoaji wa leseni. Nasisitiza wafanyabishara wazingatie kanuni na masharti ya leseni, hatutasita kuchukua hatua watakapokiuka,” amesema.

MWANANCHI
 
Back
Top Bottom