EWURA yatangaza bei mpya za mafuta ya Julai, 2022. Petroli, Dizeli zapanda

Lady Whistledown

JF-Expert Member
Aug 2, 2021
1,024
1,615
Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), imetangaza bei kikomo za bidhaa za mafuta ya petroli hapa nchini zitakazo anza kutumika Tarehe 6 Julai 2022 saa 6:01 usiku.

Aidha, Katika kukabiliana na ongezeko la bei za mafuta hapa nchini, Serikali imetoa ruzuku nyingine ya Shilingi billioni 100 kwa mwezi Julai 2022, iliyoelekezwa katika mafuta ya petroli na dizeli
-
EWURA imefafanua kuwa Kiasi kikubwa cha ruzuku kimeelekezwa katika mafuta ya dizeli kwa lengo la kudhibiti mfumuko wa bei nchini (inflation) kwa sababu dizeli hutumika zaidi katika shughuli za kiuchumi ikiwemo katika uzalishaji viwandani na katika usafirishaji wa mazao na bidhaa nyingine.

0003.jpg

0004.jpg

0005.jpg

0006.jpg

0007.jpg
 
Ni ujinga wa kiwango Cha SGR kudhan kwamba Ruzuku wanatotoa inaleta ahueni Kwa Watumiaji

Ukweli ni kwamba Hizo Bilion Kadhaa, ni za MAFISADI Yale yalobanwa na Magufuli miaka hiyo Sasa ndo yanarudishiwa pesa zao

Serikali ichukue jukumu la ku import Mafuta , yenyewe ndio iwauzie wafanya biashara wanaotuuzia watumiaji.

Haya masheli ya mabeberu hayatakiwi kununua mafuta ya Warusi kuogopa Vikwazo, na Mafuta ya Warusi ndio mafuta pekee ya Bei chini Dunia ,, Kwa hivo yaleyale mafuta wanayoyapata Kwa Bei ya juu kutoka Uswiswi, Uchina, India ambao na wao wanayanunua Urusi , ndio nawao wanataka kutengezenea pesa , Kwa kufanya hivo mtumiaji analazimika kutumia Pesa nyingi .

IELEWEKE BEI YA MAFUTA ITAENDELEA KUPANDA SIKU ZOTE HATA VITA YA UKRAINE IISHE LEO , BEI ITAENDELEA KUPANDA , DEFICIT YA MAFUTA ILOLETWA NA UMARUFUKU WA MAFUTA YA URUSI , UMETENGENEZA UHITAJI WA HARAKA WA MAFUTA NA KUPELEKEA BEI KUPANDA.

👉NI UTHUBUTU WA SERIKALI MAKINI PEKEEE KAMA ILIVYOKUA KWA HAYATI MAGUFULI, NDIO UNAWEZA KUPAMBANA NA HILI TATIZO KWA MAAMUZI MAGUMU.

👉TAIFA HALIPASWI KUCHUKUA MATATIZO YA WAMAGHARIBI ,KUA MATATIZO YA DUNIA NZIMA .

👉SERIKALI ISIOGOPE KUNUNUA MAFUTA YA WARUSI YENYE BEI CHEEEEEEE KISA VIKWAZO .

👉ILA KWA HIKI KICHWA TULICHONACHO KINACHOLIPA FADHILA , HILI TUSAHAU .!
 
Kwa hiki kichwa inawezekana siku moja lita ya petrol ikauzwa 10k
 
Back
Top Bottom